Ndago 360 degree - nani yuko nyuma ya mauaji - nchemba au ccm?? Cdm au polisi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndago 360 degree - nani yuko nyuma ya mauaji - nchemba au ccm?? Cdm au polisi???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Jul 17, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,236
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Viongozi wa serikali, vyama vya siasa, wananchi, wanachama wa vyama mbalimbali kila mmoja amebaki anaduwaa na kila mmoja analaani kilichotokea Ndago.

  Sio mara ya Kwanza mauaji na kuumizwa kwa wananchi kutokea kwenye mikusanyiko au harakati za siasa Tanzania mpaka sasa inaanza kuwa ni kama jambo la kawaida.

  Igunga tulishuhudia wananchi wakiumizwa, wakiuwawa, Meru nako mauaji yamekuwa yakitokea kipindi cha harakati za siasa na watu kupoteza maisha eti kwa sababu watu wanataka kushinda uchaguzi.

  Mimi moja kwa moja nawalaumu polisi, usalama wa taifa, DPP na viongozi wote wa serikali, hatuwezi kuendelea kuuwawa na kuteswa ili watu waendelee kufanya siasa vile watakavyo. Tangia vifo hivi vimeanza kutokea sijasikia aliyefungwa kwa kuuwa wananchi wasio na hatia na wale wote waliondaa vikundi vya kuleta fujo kurusha mawe, mishale, kutumia mapanga na risasi kwa sababu yeyote ile.

  Singida inasadikika Mweka hazina wa CCM Mwigulu Nchemba yuko nyuma ya mauji wa kada ya chama chake baada ya kuwatumia vijana ili kuvuruga kwa makusudi mkutano wa CDM. Swali hapa ambalo linanikwaza je usalama wa Taifa walikuwa wapi mbinu hizi zikipangwa iwe ni kweli au ni kikundi kingine?? Je Polisi walikuwa wapi kulinda usalama ikizingatiwa wanahitajika kuwepo kila mikutano hii ikifanywa ili kulinda amani na kukamata wahalifu pamoja na hawa warusha mawe na kuuwa wananchi??

  Kwa nini kila anapohusishwa Mwigulu watu wanakufa ?? Kila aliposhika mikoba ya CCM kusaidia kushinda wamekufa watu??? Je kwa nini uchunguzi usifanywe ili ijulikane na watu waache tabia ya kuhisiana ???

  Nani kweli yuko nyuma ya mauji haya ya Singida??? Kweli Polisi na CCM hawajui??? Kweli CDM hawajui??? Kweli usalama wa Taifa hawajui???

  Ninalaani kwa nguvu zangu zote kifo cha kada wa CCM na nina muomba Mungu yeyote aliyehusika kwa kushawishi, kulipa wananchi au vijana kuwapa vijana bangi, pombe ama kitu chochote au maneno yeyote ili walete fujo zilizozaa mauji haya aadhibiwe na hiyo siasa iwe mwisho wake.

  Amani ya kweli na upendo havitajengwa kama tutaendelea kupandikza chuki baina ya jamii, Jirani kwa jirani nk.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 15,709
  Likes Received: 8,507
  Trophy Points: 280
  Mkwawa uzi wako mbele ya mwana ccm ni sawa na almasi puani mwa nguruwe! Hawezi kuiona thamani ndani yake!!!!!
  Kama kiongozi wao (ccm) anaweza kusema "LIWALO NA LIWE" tena bungeni! Unatarajia huko ccm kuna kichwa kimesalia na akili kidogo? LINALOKUWA NDIO LINAKUWA!!!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. M

  Mwanantala Senior Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mauaji yamefanyika mbele ya ulinzi wa polisi, hivyo wauaji ni polisi.
   
 4. m

  manucho JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwigulu, CCM, Polisi, Usalama wa taifa, Serikali wote lao ni moja.
  Mwigulu always anatangulizwa mbele pembeni usalama na polisi order kutoka serikalini na CCM.
  Mwigulu na wenzake wote wanaona ni kama masihara ila damu ya mtu haimwagiki bure muda si mrefu mwigulu atakuwa mfano kwa kuonyesha matokeo ya damu anayomwaga.
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ni uzembe wa Polisi tu. Kama walijua kwamba kuna watu wanataka kufanya, fujo wangejipanga tu. mbona wananchi waliwaondoa na mkutano uka endelea. Suali ni kwamba, Polisi wanaonekana wangefurahi ule mkutano kusambaratishwa na kundi la wahuni wa kigulu.
   
 6. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,734
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aliuwawa na Chadema!
   
Loading...