Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama tawala, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kuwa Serikali ijayo itaimarisha mfumo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi ili kuhakikisha kero na mahitaji ya msingi ya Wananchi yanashughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana Septemba 9, Mjini Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, Dkt. Nchimbi amesema kuwa imebainika kuwa wananchi wengi wana matatizo na changamoto za msingi, lakini mara nyingi hawapati majibu ya haraka kutoka kwa viongozi au mamlaka husika.
“Tumegundua kuwa sehemu kubwa ya changamoto zinazowakabili wananchi zinasababishwa na udhaifu katika mfumo wa mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao, tunakwenda kulibadilisha hilo kwa kuhakikisha kila kero inasikilizwa na kushughulikiwa kwa wakati,” alisema Dkt. Nchimbi.
Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa serikali yao itaweka mifumo madhubuti ya uwajibikaji ili viongozi walioko kwenye ngazi mbalimbali wawe karibu zaidi na wananchi na wawajibike moja kwa moja kwa changamoto zinazowakabili watu waliowachagua.