Ukitaka kujua jeshi la polisi lina weledi kiasi gani angalai linavyofanya kazi wakati wa vurugu, dharura, au pale ambapo mmojawao anaumizwa. Mambo ambayo yanadaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi na wale wa JWTZ dhidi ya wananchi ni mambo yanayoita watu kuwajibishwa.
Kwamba kuna nyumba zimechomwa na polisi wametoa adhabu ya jumla (collective punishment) wakiingia kwenye majumba ya watu na kusababisha hali ya hofu kwa wananchi badala ya kuonesha weledi na amani toka mwanzo - kwani jambo hili lilijulikana kabla!
Tumeshasema mara nyingi huko nyuma wengine wanaobebwa hawabebeki... Wasije kudhania kuwa kulazimisha amani kwa nguvu namna hii kunawafanya watu wageuka na kuwapenda zaidi... wanachofanya wao wenyewe wanazidi kupandikiza chuki, sumu ya chuki inanyonywa na watoto katika matiti ya mama zao...
Binafsi sielewi kabisa kwanini Nchimbi ni Waziri! I have never understood kwanini ameendelea kuwa Waziri licha ya kuboronga wizara zote alizopitia.. kitu pekee alichowahi kuwa mzuri kwacho (kama naweza kusifikia) ni kuwa Katibu ya Umoja wa Vijana wa CCM... nje ya hapo sijui! KUhusu Mwema ndio wala sitaki ksuema maana nishasema vya kutosha... ingekuwa nchi nyingine angetimuliwa miaka minne nyuma... !
Vuai bado sijajua maana ningependa kusikia kauli yake ya kuhusika kwa JWTZ katika kadhia iliyotokea Mtwara.
ADUI wa jeshi ni wa ndani ya nchi au nje ya nchi?
na wala sio kwamba walivumilia bali walitaka wavuke benchmark yao, na ndicho walichokifanya.Kwa hii kadhia ya Mtwara nadhani Polisi wamejitahidi sana kuwa wavumilivu hadi ikaonekana kama wameshindwa kitu ambacho si kweli.
hivi Nchimbi yye personaly alitakiwa afanyeje?? na je yawezekana kabisa katika utawala wa sheria ukamwajibisha mtawala mmoja ilihali huyu mmoja hatoi maamuzi peke yake??Kwa kweli Nchimbi ni majanga!
Kwa hii kadhia ya Mtwara nadhani Polisi wamejitahidi sana kuwa wavumilivu hadi ikaonekana kama wameshindwa kitu ambacho si kweli.
Kwa kweli Nchimbi ni majanga!
Mzee Mwanakijiji,
Kupitia mada zako, umekuwa ukitoa ushauri mwingi, mzuri na unaoeleweka kwa urahisi sana kama mlengwa ni mtu mwenye nia njema kwa yale ayafanyayo. Said Mwema, Nchimbi na wengineo ndani ya utwala wa Kikwete wanatoa taswira ya aina ya Serikali tuliyonayo na Rais wa nchi kwa ujumla. Kumshauri ama kumwambia Kikwete awawajibishe hao watu ni sawa na kumwambia ajiwajibishe mwenyewe.
Tusitarajie hata siku moja Kikwete kuwawajibisha hao mawaziri na watendaji ndani ya utwala wake ambao wengi hatujui alitumia vigezo gani katika kufikia uamuzi wa kuwateua na kuwapa hizo nafasi. Kigezo kikubwa pengine ni kufahamiana, urafiki ama pengine kuna nguvu ama ushawishi wa pembeni kuwa nafasi fulani mweke fulani.
Si vyema kuacha kushauri pale inapobidi lakini kwa Kikwete tusitarajie lolote la tofauti hata angeshushwa mshauri kutoka sayari nyingine
Utaonaje kipya wakati uwezo wako wa kufikiri ni mdogo? watoto wadogo wanaonyonya ambao wamechomewa makazi yao walifanya uhalifu gani? Polisi wamepata wapi kibali cha kutoa adhabu? kwanini walianza kupora simu na mali za watu ambao wengi walikuwa wapita njia! polisi sasa wanaongoza kwa uhalifu, lakini wewe nawe kwa kuwa unaasili ya uhalifu bila aibu unawapokeza wahalifu wenzio!Sijaona kipya kwenye post yako mkuu,wewe unataka polisi wakae na kucheka na watu ambao ni waharifu hayo mawazo yako siyo varid pengine na wewe ni miongoni mwa hawa wachochezi kwa nini hujasema chochote juu wanasiasa waliochochea na wale wanaofanya hizo vurugu,acha mambo ya ajabu.
Mbona Kikwete ameiba twiga akapeleka uarabuni na wakamchekea? Mbona Pinda alituma watu wa usalama wa majambazi kwenda kumwuua dr. Ulimboka na wakacheka nae!Sijaona kipya kwenye post yako mkuu,wewe unataka polisi wakae na kucheka na watu ambao ni waharifu hayo mawazo yako siyo varid pengine na wewe ni miongoni mwa hawa wachochezi kwa nini hujasema chochote juu wanasiasa waliochochea na wale wanaofanya hizo vurugu,acha mambo ya ajabu.
Na nyie kazi yenu si kubwabwaja tuuu hakuna hata mwenye akili akawasiliana na mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa mtasemaje wamebakia yatima halafu mnachonga tuuuu au ndo mnawalilia hao cdm wenu nilishasema hakuna mwenye shibe aliyewahi kuleta ukombozi mahali popote duniani mnadanganyika bure mtaleta fujo kufurahisha walioshiba lakini zitakuwa ndio kaburi lenu chungeni sana maneno ya Nchimbi serikali sio bibi yako ukacheze nae cha ndimuKinachoendelea Mtwara ni uhalifu kwa wananchi na kibaya kuliko vyote wamebaki yatima bila utetezi wa nguvu sasa.