GE2025 Nchimbi: Mwambieni Mpina arudi CCM haraka. Akirudi nitampokea mwenyewe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amemtaka aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpiga kurejea CCM haraka.

Hivyo, amewaagiza wananchi wa Kisesa mkoani Simiyu kumfikishia salamu hizo Mpina, kwamba siku ya kurudi atampokea mwenyewe ( Dk. Nchimbi) na kumkabidhi kadi.

Ametoa agizo hilo leo alipofika katika Jimbo la Kisesa akielekea wilayani Meatu mkoani Simiyu kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

"Mwambieni Mpina kaka yako (Dk.Nchimbi) alipita hapa. Tena mwambieni akachukue kadi ya CCM na siku anayoichukua nitampokea mimi mwenyewe. Utaratibu wa CCM unafahamika ukiondooa ni lazima urudi. Kwa hiyo mfikishieni salamu zangu" amesema Mpina.

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuomba Luhaga Mpina arudi haraka kwenye Chama chake cha awali CCM na ameahidi atampokea kwa mikono yote miwili.

Akiongea akiwa katika Jimbo la Kisesa Mkoani Simiyu leo September 02,2025, Nchimbi amesema “Atakayempigia simu Mpina amwambie Kaka yake mkubwa alipita hapa na mwambieni hasiponipigia kura atakuwa amekosa adabu ya kisukuma kabisa maana nilipopita si aliwaambia kwamba Mimi Kaka yake, mwambie Kaka yako alipita hapa na anasubiri akirudi tena anataka urudishe hiyo kadi ya Chama chako kipya urudi CCM na Mimi nitapokea kadi ya Mpina Mimi mwenyewe simtumi Mtu yoyote”

Mpina alikuwa Mbunge wa Kisesa kupitia CCM ambapo baadaye alishindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na akahamia ACT Wazalendo ambako aliteuliwa na Chama hicho kugombea Urais lakini Msajili wa Vyama vya Siasa amemzuia kugombea baada ya Mwanachama wa ACT Monalisa Ndala kupeleka malalamiko akidai Mpina hajatimiza vigezo vya kugombea na sasa kesi ya suala hilo ipo Mahakamani.
 
Kiburi cha madaraka bhana!
 
Kama Gambo, Mpina hakuruhusiwa kuingia hata kwenye kura ya maoni.
 
Mnataka na Mpina hawe Polepole mwengine!! mjidai kumvisha kofia ya Ukombozi!!
 
Back
Top Bottom