Nchimbi, Kova wawakwepa Kibanda, Dk. Ulimboka

Nchimbi, Kova wawakwepa Kibanda, Dk. Ulimboka

yegella

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
3,113
Reaction score
1,105
JESHI la Polisi limeonyesha wazi kuwa halina dhamira ya dhati ya kuwasaka na kuwatia
nguvuni wahalifu waliowateka, kuwatesa na kuwaumiza vibaya Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri nchini (TEF), Absalom Kibanda, na Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari, Dk.
Steven Ulimboka.

Ni zaidi ya mwaka mmoja na miezi minne tangu Dk. Ulimboka atendewe unyama huo
lakini hadi leo suala hilo limegeuzwa sinema na jeshi hilo kwa kumkamata mtu asiyehusika
ambaye baadaye walilazimika kumwachia huru. Hivi ndivyo imetokea pia kwa Kibanda ambaye
ni Mahriri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006), kwani tangu ateswe na kung'olewa
jicho, kucha, meno na kukatwa kidole, hakuna mtuhumiwa hata mmoja aliyekamatwa ikiwa ni
zaidi ya miezi saba sasa. Lakini jana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, akiongozana na maofisa wengine wa jeshi hilo akiwemo Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, waliitisha mkutano na waandishi kuwataja ‘vibaka' waliokamatwa
wakihusishwa kumshambulia na kumwibia Dk. Sengondo Mvungi.

Dk. Mvungi ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye alivamiwa na majambazi hao
takriban wiki mbili zilizopita na kukatwa mapanga na kuporwa kompyuta mpakato (laptop) na fedha.
Kwa sasa hali yake ni mbaya akiwa bado hajitambui na hivyo kulazimika kupelekwa nchini Afrika Kusini kujaribu kuokoa maisha yake. Hatua ya Waziri Nchimbi kujitokeza jana kuzungumzia tukio hilo na kuonyesha juhudi za haraka za kuwanasa watuhumiwa, iliwasukuma waandishi wa habari kuhoji kulikoni matukio ya Ulimboka na Kibanda yamewekwa kiporo. Kama kawaida yake, Kamishna Suleiman Kova alijibu kuwa kila tukio lina mazingira yake, hivyo tukio la Mvungi halifanani la Kibanda
wala Dk. Ulimboka na kueleza kuwa mfumo wa suala hilo kiupelelezi unakwenda vizuri.

"Tukio la Mvungi na la kina Kibanda na Ulimboka mazingira yake ni tofauti; unapeleleza halafu unatuhumiwa wewe mwenyewe, ila watapatikana," alisema Kova.
Katika taarifa yao hiyo, Dk. Nchimbi na Kova walisema kuwa wamekamatwa watuhumiwa
wengine watatu zaidi wanaodaiwa kumvamia, kumjeruhi kwa mapanga na kumpora mali Dk.
Mvungi. Kova alisema kuwa operesheni ya kuwasaka waliomshambulia Dk.Mvungi imefanikiwa kwa
asilimia zaidi ya 80 ambapo mpaka sasa wamekamatwa watu tisa wakiwa na vifaa walivyotendea uhalifu huo ambavyo ni mapanga matano, simu ya mkononi na kigoda. Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Msigwa Kopelo, Chibango Magozi, Ahmed Ally, Zakaria Rafael (23) dereva wa boda boda, Manda Salowaa ( 40), Paulo Jailos (29), Juma Hamisi (29), Longishu Semaliki(29) muuza ugoro
Vingunguti na Masunga Makenza (40).

Dk. Mvungi ambaye pia ni mshauri wa masuala ya kisheria wa Chama cha NCCR-Mageuzi alipatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia Novemba 3, mwaka huu, akiwa nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Baada ya kumjeruhi waliiba sh milioni moja, bastola, simu mbili za mkononi na kompyuta mpakato (laptop). Utendaji huu wa jeshi la polisi unaacha mashaka makubwa hasa kwa matukio makubwa ya utekaji na utesaji ambayo ni mageni nchini, kwani uchunguzi wake wa kuwasaka watuhumiwa unalegalega.

Itakumbukwa kuwa mara tu baada ya tukio la Dk. Ulimboka Julai 26 mwaka jana, jeshi hilo liliunda kikosi kazi kilichowashirikisha wataalamu mbalimbali wa kanda maalumu na makao makuu. Hadi sasa ripoti yake haikuwahi kutolewa hadharani kama Kova alivyojigamba wakati akiitangaza, badala yake hivi karibuni amekuwa akitupiana mpira na wakuu wake kuhusu ripoti hiyo.

Dk. Ulimboka kwa kiapo aliwataja watu aliowatuhumu kuhusika na tukio hilo, mmoja wao akiwa ni ofisa usalama wa taifa-Ikulu lakini hakuwahi kufanyiwa gwaride la utambuzi wala kuhojiwa na kamati hiyo ya uchunguzi. Siku chache kabla ya Dk. Ulimboka kumtaja ofisa huyo, gazeti la MwanaHalisi lilichapisha habari iliyoeleza tukio zima lakini serikali ikalifungia kwa muda usiojulikana kwa kile kinachoitwa kosa la uchochezi. Tukio hilo la Dk. Ulimboka limekuwa kama sinema kwani hata mtuhumiwa pekee raia wa Kenya, Joshua Mulundi, aliyekuwa amekamatwa na kuwekwa ndani kwa muda kadhaa na kufunguliwa kesi, ukamatwaji wake ulikuwa wa kutia mashaka.

Wakati vinywa vya wananchi vikiwa bado vinatafakari unyama huo, tasnia ya habari nayo iliingiliwa kwa kushambuliwa kiongozi wa wahariri katika tukio kama lilelile la Dk. Ulimboka. Matukio haya ni kama ya kupangwa kutokana na kufanyika kwa ustadi wa hali ya juu na kwa muda mfupi tena bila wahusika kuchukua chochote kwa mteswaji. Kama ilivyokuwa kwa Dk. Ulimboka, pia kwa Kibanda, iliundwa kamati ya uchunguzi iliyoongozwa na wataalam wakiwemo walewale walioshindwa kuwakamata watesaji wa Dk. Ulimboka.

Hadi leo hakuna mtuhumiwa hata mmoja ametiwa nguvumi na jeshi la polisi ambalo kila siku viongozi wake wamekuwa wakijinasibu kuwa na intelijensia ya hali ya juu inayobaini matukio ya kihalifu kabla ya kutokea, mathalani kuzuia maandamano na mikutano ya vyama kwa madai ya kuepusha vurugu..
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::

wauwaji wa Dr. Sengondo Mvungi ndiyo walio wateka Kibanda na Dr. Ulimboka sijawahi mlevi wa gongo avamie mahali asitake simu wala pesa atake laptop tu, hii hata tahira atajua kabisa wahusika ni nani...
 
Mleta uzi, kwani wewe hujuwi wahusika wakuu wa hayo matukio ni hao hao policcm? Sasa iweje wajikamate wenyewe????
 
Mleta uzi, kwani wewe hujuwi wahusika wakuu wa hayo matukio ni hao hao policcm? Sasa iweje wajikamate wenyewe????

basi kama ni hivyo wauza ugoro ja wanywa gongo wanatabu kwenye utawala huu yaani kuua aue tiss kukamatwa akamatwe muuza ugoro..
 
Yule Mkenya aliyemtesa Dr ulimboka hajakamtwa tena na kuhusishwa na mauwaji ya DR Mvungi?
 
Nahisi nimekosa mtililiko wa matukio sehemu Fulani. Dr. Mvungi alikuwa na tofauti gani na serikali mpaka utekwaji wake uhusishwe kwa ukaribu na matukio ya akina Kibanda na Dr. Ulimboka? Mi nilihisi watekaji wake ni waganga njaa waliokuwa wanatafuta namna ya kuishi mjini maana utekwaji wa Dr. Ulimboka na Bwana Kibanda haukuhusisha upolaji wa vitu kama ilivyokuwa kwa Dr. Mvungi ambapo wavamizi walichukua at least some valuable items kama hiyo laptop, simu na pia cash M1. Pia watekaji wa Dr. Mvungi hawakuwa na haja ya kung'oa meno, kucha, au macho kama ilivyokuwa kwenye matukio ya either Dr. Ulimboka au Bwana Kibanda. Bado Napata shida kuwahusisha watesaji wa Dr. Mvungi na wale wa matukio ya akina Kibanda. Tafadhali nielimisheni.
 
Waliomjeruhi dr mvungi na hatimaye kupatwa na umauti wameshakamatwa na wanafikia 9. Dereva wake ndie aliyepanga na kuratibu tukio zima
 
KADA MAARUFU WA CHADEMA ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUMMWAGIA TINDIKALI USONI KADA WA CCM WAKATI WA UCHAGUZI WA IGUNGA


MUSA TESHA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI


Kada maarufu wa CHADEMA Shinyanga mjini,Bwana Oscar Kaijage,Jumamosi alikamatwa na askari polisi na kuzuiwa kituo cha kati na jana Jumatatu alisafirishwa kwenda Tabora na kukabidhiwa kwa askari wa huko.


Sababu kuu ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa Tesha 9 Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge ambapo mgombea wa CCM bwana Peter Kafumu alimshinda mgombea wa CHADEMA bwana Joseph Kashinde.


Bwana Oscar alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi ya Shinyanga mjini mnamo saa 9 mchana na askari nane ambao hawakuvaa sare.


Baada ya mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo wasogee ili wawe mashuhuda wakati wanampekua.


Hata hivyo,polisi hao hawakukuta kitu chochote walichokihitaji na kuamua kuondoka naye kwenda kumpekua nyumbani kwake ambako nako pia hawakuambulia kitu.




Taarifa iliyopatikana jana mchana kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora kwenda kufunguliwa mashitaka.
 
6 wakamatwa sakata la kujeruhiwa kwa Mvungi
Tuesday, November 05, 2013 5:48 PM
JESHI LA POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kumvamia na kumjeruhi kwa mapanga Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova amesema, watu hao wamekamatwa baada ya msako mkali uliofanywa na jeshi hilo kwa ushirikiano na raia




Amesema kutokana na ushirikiano huo walifanikiwa kuwakamata watu hao na msako unaendelea kuwakamata wengine zaidi


Amesema watu hao majina yao kwa sasa hayatawekwa hadharani kwa sababu za kiupelelezi


Dkt. Mvungi alivamiwa juzi na watu hao na kabla ya kujeruhiwa watu hao walifanikiwa kuiba fedha taslimu, simu na kompyuta mpakato


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema, hali ya Dk. Mvungi inatia matumaini kwa kuwa kuna mabadiliko kidogo katika hali yake japo hajapata fahamu


Amesema wamepanga misa maalum ya kumuombea Dk. Mvungi inatarajiwa kufanyika leo jioni katika Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam..sare za chadema pia zilikamatwa
 
KADA MAARUFU WA CHADEMA ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUMMWAGIA TINDIKALI USONI KADA WA CCM WAKATI WA UCHAGUZI WA IGUNGA


MUSA TESHA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI


Kada maarufu wa CHADEMA Shinyanga mjini,Bwana Oscar Kaijage,Jumamosi alikamatwa na askari polisi na kuzuiwa kituo cha kati na jana Jumatatu alisafirishwa kwenda Tabora na kukabidhiwa kwa askari wa huko.


Sababu kuu ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa Tesha 9 Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge ambapo mgombea wa CCM bwana Peter Kafumu alimshinda mgombea wa CHADEMA bwana Joseph Kashinde.


Bwana Oscar alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi ya Shinyanga mjini mnamo saa 9 mchana na askari nane ambao hawakuvaa sare.


Baada ya mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo wasogee ili wawe mashuhuda wakati wanampekua.


Hata hivyo,polisi hao hawakukuta kitu chochote walichokihitaji na kuamua kuondoka naye kwenda kumpekua nyumbani kwake ambako nako pia hawakuambulia kitu.




Taarifa iliyopatikana jana mchana kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora kwenda kufunguliwa mashitaka.

Huyu ndiyo mtanzania mwenyewe akili timamu.
Tumekwisha.
 
yegella katiba itakayokuja kwa ajili ya referendum kwa kuwa na sura ya CCM kura yangu itakuwa hapana, najua watachakachua lakini wajue kila tolerance ina limit. Kwanza walitaka tume ivunjwe mara baada ya kukabidhi rasimu ili wafanye madudu yao, imeshindikana, sasa wameamua kuanza kuwaondoa wanatume duniani. Ndani ya tume na sekretariati yake kuna watu wenye hila mbaya, hayo majambawazi yalijuaje kuwa marehemu ndio alikuwa jikoni?
 
Last edited by a moderator:
Nahisi nimekosa mtililiko wa matukio sehemu Fulani. Dr. Mvungi alikuwa na tofauti gani na serikali mpaka utekwaji wake uhusishwe kwa ukaribu na matukio ya akina Kibanda na Dr. Ulimboka? Mi nilihisi watekaji wake ni waganga njaa waliokuwa wanatafuta namna ya kuishi mjini maana utekwaji wa Dr. Ulimboka na Bwana Kibanda haukuhusisha upolaji wa vitu kama ilivyokuwa kwa Dr. Mvungi ambapo wavamizi walichukua at least some valuable items kama hiyo laptop, simu na pia cash M1. Pia watekaji wa Dr. Mvungi hawakuwa na haja ya kung'oa meno, kucha, au macho kama ilivyokuwa kwenye matukio ya either Dr. Ulimboka au Bwana Kibanda. Bado Napata shida kuwahusisha watesaji wa Dr. Mvungi na wale wa matukio ya akina Kibanda. Tafadhali nielimisheni.


wauaji wana mbinu za kupoteza ushahidi, ili wasisthukiwe,iyo kuchukua fedha na simu ni mbinu tu ili kuonyesha waliofanya jambo ilo ni vibaka waganga njaa.
kwenye tukio hili lazima mtu alikuwa afe au laptop ioondoke au vyote viwili kwa pamoja,wamefanikiwa kwa vyote viwili,sasa jiulize kwa nini nimesema laptop ilikuwa inaitajika
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova amesema, watu hao wamekamatwa baada ya msako mkali uliofanywa na jeshi hilo kwa ushirikiano na raia




Amesema kutokana na ushirikiano huo walifanikiwa kuwakamata watu hao na msako unaendelea kuwakamata wengine zaidi


Amesema watu hao majina yao kwa sasa hayatawekwa hadharani kwa sababu za kiupelelezi


Dkt. Mvungi alivamiwa juzi na watu hao na kabla ya kujeruhiwa watu hao walifanikiwa kuiba fedha taslimu, simu na kompyuta mpakato


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema, hali ya Dk. Mvungi inatia matumaini kwa kuwa kuna mabadiliko kidogo katika hali yake japo hajapata fahamu


Amesema wamepanga misa maalum ya kumuombea Dk. Mvungi inatarajiwa kufanyika leo jioni katika Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam..sare za chadema pia zilikamatwa

mkuu mbona kama unajikunakuna makalio kwani tayari imebumbulukiwa kuwa maccm yamechezesha dili!
 
katiba itakayokuja kwa ajili ya referendum kwa kuwa na sura ya CCM kura yangu itakuwa hapana, najua watachakachua lakini wajue kila tolerance ina limit. Kwanza walitaka tume ivunjwe mara baada ya kukabidhi rasimu ili wafanye madudu yao, imeshindikana, sasa wameamua kuanza kuwaondoa wanatume duniani. Ndani ya tume na sekretariati yake kuna watu wenye hila mbaya, hayo majambawazi yalijuaje kuwa marehemu ndio alikuwa jikoni?

Ndio hivyo mkuu, hawa hawa ndio wauaji na wachunguzi. Angalia aina ya watu waliokamatwa, muuza ugoro? Je wamepona ule ugonjwa wa "habitual liars"
 
wauaji wana mbinu za kupoteza ushahidi, ili wasisthukiwe,iyo kuchukua fedha na simu ni mbinu tu ili kuonyesha waliofanya jambo ilo ni vibaka waganga njaa.
kwenye tukio hili lazima mtu alikuwa afe au laptop ioondoke au vyote viwili kwa pamoja,wamefanikiwa kwa vyote viwili,sasa jiulize kwa nini nimesema laptop ilikuwa inaitajika
moes, waswahili wanasema panapovuka moshi pana moto, inaonekana ndo hicho ulichotaka kuniambia kwenye jibu lako hili, kama ndo hivyo nimekupata ila sijajua ni kwa nini kwani kama shida ilikuwa ni kuondoa kumbukumbu furani zilizokuwa kwenye laptop, bado sioni kama kuchukua laptop ilikuwa ndo suluhisho maana kwa karne ya 21 na kwa mtu mwenye elimu kama daktari Mvungi asingeweza kutunza infor. sensitive ndani ya laptop peke yake. Pengine angeweza kuwa na same copy ya infor. kwenye data storage gadgets zingine na akawa nayo kwa matumizi yaliyokusudiwa hata baada ya kupotea kwa laptop yake. Funguka zaidi kamanda niko Keen sana!
 
Last edited by a moderator:
Nahisi nimekosa mtililiko wa matukio sehemu Fulani. Dr. Mvungi alikuwa na tofauti gani na serikali mpaka utekwaji wake uhusishwe kwa ukaribu na matukio ya akina Kibanda na Dr. Ulimboka? Mi nilihisi watekaji wake ni waganga njaa waliokuwa wanatafuta namna ya kuishi mjini maana utekwaji wa Dr. Ulimboka na Bwana Kibanda haukuhusisha upolaji wa vitu kama ilivyokuwa kwa Dr. Mvungi ambapo wavamizi walichukua at least some valuable items kama hiyo laptop, simu na pia cash M1. Pia watekaji wa Dr. Mvungi hawakuwa na haja ya kung'oa meno, kucha, au macho kama ilivyokuwa kwenye matukio ya either Dr. Ulimboka au Bwana Kibanda. Bado Napata shida kuwahusisha watesaji wa Dr. Mvungi na wale wa matukio ya akina Kibanda. Tafadhali nielimisheni.

Ndugu Mganga Njaa awezi Kuiba Bastola wakati fani yake ni Mapanga. Hawa wameiba bastola, Milioni Moja na Simu Mbili na Laptop Juu.

Nijuavyo mimi ukiba simu haichukui hata Siku mbili lazima wakupate na kwa vyovyote hao jamaa walienda na simu zao hapo sasa inashindika nini kupata number mpya za simu zilizoonekana mtaa huo kwa Usiku Huuo? Hata kama kulikuwa na wageni 100 Kibamba siku hiyo wiki mbili sasa wangesha chuja na kuwajua wauaji.

Pili jamaa wameiba na kuharibu vitu inamaana hawajaacha alama za vidole hapo kwenye eneo la tukio? Kama wameacha ni kweli hawana Leseni ya Gari hao? Kama wanayo, Kupitia System ya TRA wanashindwa nini kumjua huyo Mualifu? Mbona ni suala dakika Sifuri tu?

Hii ni aibu mtu unakwenda kukamata wanywa gongo na wala Ugoro unasema ndio wahalifu.

MACCM wanahusika na nahisi huyu ni RaMA mwingine maana Rama alikuwa anashindwa kuua ila huyu mpya ni noma anapiga kunako maana marehemu ajawahi kupata ufahamu tokea apigwe na hii ni Mapigo ya Kitaalum tu ndio yana)oweza kufanya hivi.

Tusubiri mengi na hakika watakufa wengi.

Kingine tujiulize kwanini waondoke na simu?

Mimi nahisi walimpigia simu kwa vyovyote kujua yupo wapi na hakika ukifuatilia number zake na simu alizopokea siku chache kabla ya Tukio hakika unaweza ukakakuta Number ya Rama au muuaji aliyehusika.
 
moes, waswahili wanasema panapovuka moshi pana moto, inaonekana ndo hicho ulichotaka kuniambia kwenye jibu lako hili, kama ndo hivyo nimekupata ila sijajua ni kwa nini kwani kama shida ilikuwa ni kuondoa kumbukumbu furani zilizokuwa kwenye laptop, bado sioni kama kuchukua laptop ilikuwa ndo suluhisho maana kwa karne ya 21 na kwa mtu mwenye elimu kama daktari Mvungi asingeweza kutunza infor. sensitive ndani ya laptop peke yake. Pengine angeweza kuwa na same copy ya infor. kwenye data storage gadgets zingine na akawa nayo kwa matumizi yaliyokusudiwa hata baada ya kupotea kwa laptop yake. Funguka zaidi kamanda niko Keen sana!

upo sahihi mkuu,lakini wauaji ni watu wenye akili kubwa sana wanaweza kutumia weakness yako ndogo kukumaliza,unaweza ukatunza information zako kwenye data storage gadgets tofautitofauti,lakini only one folder ukajisahau likawa kwenye laptop tu(wauaji wanasoma mazingira kwa umakini nakujua kwa undani kila kitu kabla ya kutekeleza)
ndio maana nimesema kitu kimojawapo au zaidi ya hivi vingefanikisha malengo yao 1 kuua 2 kuiba laptop 3 au vyote 1&2.
kama angepona dr mvungi bado wauaji wangekuwa wamefanikisha kwa kiasi kikubwa lengo lao(kuondoka na laptop yenye information za muhimu,ambazo kuzipata tena it cost long time.
 
Nahisi nimekosa mtililiko wa matukio sehemu Fulani. Dr. Mvungi alikuwa na tofauti gani na serikali mpaka utekwaji wake uhusishwe kwa ukaribu na matukio ya akina Kibanda na Dr. Ulimboka? Mi nilihisi watekaji wake ni waganga njaa waliokuwa wanatafuta namna ya kuishi mjini maana utekwaji wa Dr. Ulimboka na Bwana Kibanda haukuhusisha upolaji wa vitu kama ilivyokuwa kwa Dr. Mvungi ambapo wavamizi walichukua at least some valuable items kama hiyo laptop, simu na pia cash M1. Pia watekaji wa Dr. Mvungi hawakuwa na haja ya kung'oa meno, kucha, au macho kama ilivyokuwa kwenye matukio ya either Dr. Ulimboka au Bwana Kibanda. Bado Napata shida kuwahusisha watesaji wa Dr. Mvungi na wale wa matukio ya akina Kibanda. Tafadhali nielimisheni.

wahusika ni wale wale ila wamebadili mfumo wa kutesa na kuua, sasa wanachukua na vitu ili kupoteza mwelekeo
 
Back
Top Bottom