GE2025 Nchimbi atoa ahadi upanuzi maegesho kivuko cha magogoni pamoja na kigamboni, kudhibiti msongamano

GE2025 Nchimbi atoa ahadi upanuzi maegesho kivuko cha magogoni pamoja na kigamboni, kudhibiti msongamano

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi leo Septemba 28, 2025 ametoa ahadi ya Upanuzi kwenye maegesho ya Kivuko cha Magogoni na Kigamboni Shabaha ikiwa ni kuondoa foleni pamoja na kuboresha huduma katika kivuko hicho.

Dkt Nchimbi ametoa ahadi hiyo leo akizungumza na Wananchi wa Kigamboni katika mkutano wa Hadhara wa Kampeni za Urais kuelekea Oktoba 29.

"Lakini vile vile katika miaka hii mitano, tumedhamiria kuhakikisha matengenezo ya Vivuko vyetu vya MV Magogoni na MV Kigamboni yanafanyika haraka" amesema Dkt Nchimbi.

Dkt Emmanuel John Nchimbi ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi mkuu wa 2025 wakipeperusha Bendera ya CCM, ambapo mkoa wa Dar es Salaam unakuwa wa 15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za Ushindi kwa Chama hicho Tawala.​
 
Tunajua anaweza kufanya hivyo hiyo ni ahadi ndogo sana kwake kuliko masirahi atakayoyapata wakisha uchaguzi, itoshe kusema kwamba tumechoka kuendelea kula mimea ya kijani ni wakati sasa wa kubadili vyakula ikiwezekana tule hata kachori za langi na si majani tena.
 
Back
Top Bottom