Nchi za magharibi ni zipi?

Nchi za magharibi ni zipi?

mwambojoke

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
1,090
Reaction score
653
Napata utata kidogo katika tafsiri ya 'Nchi za magharibi' hasa pale linpokuja suala la kuzijumuisha nchi za ulaya na Amerika.kimsingi utata zaidi unakuja nikihusianisha jiografia ya nchi hizi na jina lenyewe ' Nchi za Magharibi' .Kwa anayejua jua hasa tafsiri hii anisaidie hili.
 
Una compass hapo nikuelekeze vizuri jinsi zilivyo ?
 
Napata utata kidogo katika tafsiri ya 'Nchi za magharibi' hasa pale linpokuja suala la kuzijumuisha nchi za ulaya na Amerika.kimsingi utata zaidi unakuja nikihusianisha jiografia ya nchi hizi na jina lenyewe ' Nchi za Magharibi' .Kwa anayejua jua hasa tafsiri hii anisaidie hili.

Inategemea wewe uko wapi.
 
SWALI ZURI!! na mimi nauliza kwa nini nchi kama Tanzania inaitwa nchi dunia ya tatu "third world country"?? je kuna dunia tatu?? na je "second world countries" ni zipi?
 
Kadiri unavyopunguza uwezo wa kutafiti ndivyo unavyoongeza uwezo wa kutegemea.
 
LORDVILLE wakati unachagua avatar yako ulizingatia masharti na vigezo gani?
 
Last edited by a moderator:
Napata utata kidogo katika tafsiri ya 'Nchi za magharibi' hasa pale linpokuja suala la kuzijumuisha nchi za ulaya na Amerika.kimsingi utata zaidi unakuja nikihusianisha jiografia ya nchi hizi na jina lenyewe ' Nchi za Magharibi' .Kwa anayejua jua hasa tafsiri hii anisaidie hili.

Haina uhusiano wowote na geographical positioning, isipokuwa ni jina linalotumiwa zaidi kulingana na mtazamo wa kiuchumi au mlengo wa kisiasa.
 
Inategemea wewe uko wapi.

Sawa kabisa!
Ukiwa Tz kwa kuelekea Kaskazi nchizako za Magharibi ni Congo, Nigeria, Ghana.
Ukiwa Ujerumani, U.k ni nchi yako ya magharibi!
Teh teh teh!
 
Napata utata kidogo katika tafsiri ya 'Nchi za magharibi' hasa pale linpokuja suala la kuzijumuisha nchi za ulaya na Amerika.kimsingi utata zaidi unakuja nikihusianisha jiografia ya nchi hizi na jina lenyewe ' Nchi za Magharibi' .Kwa anayejua jua hasa tafsiri hii anisaidie hili.

SWALI ZURI!! na mimi nauliza kwa nini nchi kama Tanzania inaitwa nchi dunia ya tatu "third world country"?? je kuna dunia tatu?? na je "second world countries" ni zipi?

je na mtu aliye location tofauti na yetu nae atasema ni nchi za magharibi?

Inategemea yuko wapi, japo kijiografia itabaki vile vile

Sawa kabisa!
Ukiwa Tz kwa kuelekea Kaskazi nchizako za Magharibi ni Congo, Nigeria, Ghana.
Ukiwa Ujerumani, U.k ni nchi yako ya magharibi!
Teh teh teh!

wakuu, kwa elimu yangu ya darasa la tatu la enzi hizo na uzoefu wangu kidogo wa mambo ya kisiasa na kiuchumi, nchi za magharibu "western countries" zinajulikana hivyo si kwa sababu za kijiografia ila ni kwa kwa sababu za kimaendeleo - hapo kuna akina G8, G20 na kadhalika (sifahamu zinanatkiwa kuwa na GDP ya kiasi gani) ila nchi za magharibu ni zile nchi Tajiri kiuchumi na kimaendeleo, wababe, na ambao wakikohoa tu wewe ka...ja,,,mb,,,a nani unapata hofu, hizi ni developed countries .
Ili hali nchi za kusini: ni nchi ambazo kwa kusema ukweli zinaishi kwa kumtegemea Mungu tu, na ambazo zipo hoi kiuchumi na kimaendeleo ya namna yoyote - hizi ni ndizo huitwa LDC ambazo GDP yake naona hata aibu kuisema ila kwa ufupi Tanzania tumo pamoja na nchi nyingi za kiafrica, Karibiani na Latin Amerika.
Na kwa mfumo huu nadhani hatuna nchi za kaskazini wala mashariki
 
Hebu na mimi niongeze langu la moyoni,,,,,,,,,,,
Tanzania kwa upande wa Mashariki inazungukwa na Bahari.Ambayo Inaitwa Bahari ya Hindi(INDIA OCEAN)
Sasa kwanini Bahari hii isiitwe bahari ya Tanganyika,Tanzania au hata Zanzibar.Ni kipi haswa/au kigezo gani kilichotumika kuiita bahari ya Hindi.?
Ufafanuzi na Maelezo tafadhali
hasante!
 
Back
Top Bottom