nchi za BRICS kuanzisha benki yao

nchi za BRICS kuanzisha benki yao

mhalisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
1,181
Reaction score
322
nchi tano duniani ambazo uchumi wao unakuwa kwa kasi zimeazimia kuanzisha benki yao ya maendeleo ambayo itakuwa na mtaji wa dola za kimarekani bilioni 50.
nchi hizo zinazounda umoja unaoitwa Brics ni Brazil, China, India, Urusi na Afrika Kusini.
_76286877_tv023169010.jpg
 
Ni mtaji wa USD 100 Bilioni na sio 50 na lengo lao ni kupambna na WB na IMF ambazo inaonekana ni za kimagharibi
 
Development Bank hii lengo lake kubwa ni kukopesha mikopo yenye riba nafuu,kufadhiri miradi ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea kwa nia ya kuziendeleza nchi zozote zitakazo hitaji mikopo ya binki hiyo. tofauti na WB na IMF ambazo huzinyonya nchi zinzoendelea badala ya kuziendeleza.Ni benki itakayo kuwa na hadhi sawa au malengo sawa na World Bank na IMF lakini yenye masharti rahisi kuliko WB na IMF.
 
Ni mtaji wa USD 100 Bilioni na sio 50 na lengo lao ni kupambna na WB na IMF ambazo inaonekana ni za kimagharibi

mkuu sidhani kama ni kupambana au kuonekana kama ni za ki magharibi,bali kwa miaka mingi WB na IMF zimekuwa ni taasisi za kuzinyonya nchi maskini ,nchi zinazoendelea na zimekua ni fimbo ya kuzitia adabu nchi zinazotofautiana na Mabeberu wa dunia.Mbali na hayo Taasisi hizi zimekua na faida zaidi kiuchumi kwa Marekani na majambazi wenzake.
 
Kiwango chachini kufungua a/c ni beigani? Name nikafungue crdb nimewachoka.
 
Kiwango chachini kufungua a/c ni beigani? Name nikafungue crdb nimewachoka.

Najua unafanya masihara,lakini unajua majirani zetu wakisoma mchango wako kwa kuwa hawajui kua unatania watazidi kuamini kuwa ni kweli Watanzania tuna IQ ndogo sana.Mimi nimekuelewa kua unatania ila sijui kama wote watakuelewa.na inawezekana hata baadhi ya watanzania wengine wasikuelewe.
 
Back
Top Bottom