Mnyonge Namba1
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 402
- 81
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitabiri yote haya! Alisema kitu kama hiki:-
Itafika hatua watu watagawanyika mpaka kwenye ngazi ya familia. Mtaanza kusema sisi ni wazawa wa kwanza na wao wa pili. Sisi wa Baba na wao wa Mama. Tunapoelekea huku tutaanza "Sisi ni JF Premium Member, wao ni Junior Member na hawalipii.Yanayotuunganisha ni makubwa kuliko yanayotutenganisha.
Swali lingine ni kwa nini mwaka jana wakati wazanzbari wanajadili muungano na kuamua kuuvunja kwa kutambua Zanzbar kuwa nchi JK alikaa kimya, lakini inapofika muda watanganyika nao wajadili tunawekewa mipaka? Hadi sasa katiba ya Zanzbar inacontradict katiba ya muungano. kazi iliyopo ni kuliweka sawa hilo. Na ili kuliweka sawa hilo options ni mbili tu! kuirejesha serikali ya Tanganyika au kufuta kipengele kinachoitambua Zanzbar kuwa ni nchi ili tubaki na Tanzania moja tuMimi kama MtanganyikaHALIS Napenda nipate zaidi response ya wazenj km Katiba Mpya na wengineo.Je Zenji mnaona ufahari sana kututawala kiaina sie tuliodanganyika na huu muungano feki?.
Swali lingine ni kwa nini mwaka jana wakati wazanzbari wanajadili muungano na kuamua kuuvunja kwa kutambua Zanzbar kuwa nchi JK alikaa kimya, lakini inapofika muda watanganyika nao wajadili tunawekewa mipaka? Hadi sasa katiba ya Zanzbar inacontradict katiba ya muungano. kazi iliyopo ni kuliweka sawa hilo. Na ili kuliweka sawa hilo options ni mbili tu! kuirejesha serikali ya Tanganyika au kufuta kipengele kinachoitambua Zanzbar kuwa ni nchi ili tubaki na Tanzania moja tu
tunastahili kuidai tanganyika yetu kwa nguvu zote; wazenji ni watu wasio na fadhila kwa watu bara
Mimi naomba Serikali zote mbili kama wanavyosema wanasiasa waitishe KURA ZA MONI kwa watanzania kama muungano uwepo au usiwepo, kuanzia hapo hatutalalamika teeenaaa!!. Happy Muungano
Nasikia mara ohhhh, wabara wanatuonea, wabara wanatudharau. Sisi si wabara, ni watanganyika bana!
Muungwana haachi asili. Nia yangu si kuanzisha thread ya kupinga muungano, bali sipendi kuitwa mbara na ndio maana ninasema sisi sio wabara, ni watanganyika. Ukisema Tanganyika ni jina la kikoloni, basi kataa pia majina ya Tabora, Mwanza, Dar es salaam, Tanga na mengine mengi yanayopatikana katika ramani iliyochorwa na mkoloni.
So captivated in fantasy!mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui
nilizaliwa Tanzania,
nilizaliwa Afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu
kwa hiyo;
mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu
maana ya Tanzania, najua
maana ya Afrika, najua
maana ya Dunia, najua
maana ya mwandamu, najua
nawauliza wazanzibari,
nini maana ya Zanzibari,
nani aliipa jina Zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
kwa nini wasijivunie utanzania?
So captivated in fantasy!
Inapendeza sana sisi wa-TANGANYIKA muda si mrefu tutapata taifa letu tupambane na hao Al-shabaab