Nchi yangu Tanzania

Nchi yangu Tanzania

dabluz

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
2,455
Reaction score
1,676
Wana baraza naombeni mnisaidie kupata nyimbo zote za kuisifia Nchi yetu Tanzania, nina mtoto wangu ndio kaanza nursery sasa nataka nimwandae kuipenda Nchi yake kwa nyimbo zakuhamasisha. Naombeni mniwekee hapa verse zake na ikiwezekana majina ya vitabu nikavitafute..
Nakumbuka sisi tuliimba sana na ndio uzalendo unapoanzia hapo.
Nasubiria wanaboard.
 
Naye baba Nyerere ndiye wetu mnini sijui.
Tena yeye ndiye aliyeleta uhuru.
Tanzania yetu ni nchi ya furaha!
 
Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo (Tanzania Nakupenda) na Tazama ramani
 
Mkuu brainia89 nimekusoma, tayari picha nimepata lakini vipi kuhusu lyrics zote maana nimegoogle lakini sijapata.
Asanteni kwa msaada ila bado nasubiria wadau.
 
Mungu ibariki Afrika
Wabariki Viongozi wake
Hekima Umoja na Amani
Hizi ni ngao zetu
Afrika na watu wake.
Chorus:
Ibariki Afrika, Ibariki Afrika
Tubariki watoto wa Afrika.
Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na Umoja
Wake kwa Waume na Watoto
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
Chorus:
Ibariki Tanzania, Ibariki Tanzania
Tubariki watoto wa Tanzania.
 
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
 
Back
Top Bottom