Nchi ya waongeaji bila vitendo

Nchi ya waongeaji bila vitendo

LuciusKaisery

Member
Joined
Feb 19, 2018
Posts
18
Reaction score
31
  1. Alipigwa risasi Tundu Lissu
    Watanzania wengi waliongea wengine wa waka-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tukaishia hapo. Hakuna hatua inayochukuliwa.
2.Kapotea Ben Saa Nane.

3. Kapotea Azory mwandishi wa habari ya Mwananchi.

4. Msimu wa Makonda
Watanzania wengi waliongea wengine wa waka-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tukaishia hapo. Vyombo vya kutetea haki za vyombo vya habari vikaalani vikali vikaishia hapo. Hakuna hatua inayochukuliwa.

5. Kifo cha Aquelina Akwilini
Watanzania wengi wanaongea wengine wa wana-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tunaishia hapo. Wengine wanataka Mwigulu Nchemba ajiudhuru tutaishia hapo. Hakuna hatua itayochukuliwa.

6. Serikali awamu ya tano na usimikaji wa mfumo wa chama kimoja.

Watanzania tunaongea bila kuchukua hatua yoyote. Vyama pinzani nchini vinakandamizwa, kuwa mpinzani nchini ni jinai au hatia. Tuna kila sababu ya kusema chama tawala kinanunua viongozi wa vyama pinzani na moja kwa moja serikali inahusika. Kwa nini tunasema serikali inahusika? Serikali kama inaridhia kutoa pesa za kurudia chaguzi ndogo ndogo maana inafurahiswa na swala hilo. Bado wakishinda chaguzi ndogo ndogo wanafurahi, chaguzi sio za haki na huru kuna furaha ya kweli hapo? Unapigana na mtu umempatia panga wewe una bunduki nawe unasema ulipambana kweli kweli? Mpe bunduki nae.

Sisi tutakuwa nchi ya aina gani? Kuzungumza ndio suluhisho tosha? Ina maana hatujui mizizi ya matatizo yetu? Hatujui chanzo cha matatizo yetu?

Kwa nini tunashindwa kuungana watanzania? Kupelekea tunakuwa nchi ya waongeaji.

Tunakubali kugawanya na vyama vya siasa vyetu.Vyama vya siasa visitugawe tukashindwa kukemea na kutatua matatizo yetu na tukumbuke hamna tatizo la mtanzania mmoja mmoja bali kuna tatizo la watanzania.

Huenda ungekuwa wewe au mimi tungepigwa risasi au kutekwa utasemaje ni tatizo la mtanzania mmoja mmoja.

Kuwa mfuasi wa CCM ndio isiwe serikali ikikkosea au inapokosea au inapoiminya katiba ndio ushindwe kuungana na wengine au ushindwe kukosoa kisa tu wewe ni mkereketwa wa CCM hivyo hivyo kwa vyama pinzani.

CCM si zaidi ya utaifa wetu au Upinzani si zaidi ya Utanzania wetu au Utanganyika wetu au Unzanzibari wetu. Au tushindwe kuungana tutatue matatizo yetu ya Tanzania yetu kisa vyama vyetu vya siasa. Tanganyika au Zanzibari ilikuwepo kabla ya vyama vya siasa vyote nchini.

Jambo baya ni baya tu haijalisha nani amefanya awe babaako au mamako au ndugu yako litabaki kuwa baya tu.

Kifo cha Aquelina Akwilini tunajua tatizo ni nini, lakini tunatupiana lawama. CHADEMA walikuwa wanatumia haki ya msingi kikatiba ya MAANDANO HURU NA YA AMANI. Ni kosa kutumia haki yako kikatiba? CHADEMA ndio waliopiga risasi? Au Aquelina Akwilini alikuwa miongoni mwa waandamanaji wa CHADEMA?

POLISI ndio waliopiga risasi kwa mgongo wa kuzuia maandamano, Unazuia maandamano kwa kupiga risasi? Waandamanaji walikuwa na silaha? Halafu tunataka kuzui matumizi mabovu ya silaha au kuzuia maandaamano?

Mfano hili jambo lipo wazi tutataka kuleta uhusikaji wa vyama vya siasa, lakini chama tawala kinazungumzia upande mmoja kukishtumu CHADEMA. Lakini chama tawala kinasahau kuwa ndio chanzo cha matatizo yote.

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC si taasisi huru ipo chini ya chama tawala, NEC inashirikiana moja kwa moja na chama tawala. NEC nayo inapaswa kuwajibishwa, Lakini wa kuwa-wajibisha nani? Serikali au Bunge au Mahakama? Mihimili yote ni chama tawala, vinatumika na chama tawala na viko chini ya chama tawala.

Serikali inasema haina hela lakini inapata wapi mabilioni ya kurudia chaguzi ndogo ndogo hizi? Kwenye kuongeza mshahara wa mwalimu serikali inasema haina pesa, kwenye mambo ya msingi serikali inasema haina pesa.

Tuache siasa, tuache kuzungumza zungumza na tuache kulopoka lopoka tuchukue hatua ya vitendo stahiki.
 
Hapna sisi tunatekeleza wajibu wetu ipasavyo, kwani sisi wajibu wetu ni kukaa katika mitandao kuhamaishisha watu waandamane, kisha tunakaa katika TV kuangalia matunda ya kazi yetu huku baadhi ya tuliowachochea wamevunjwa miguu. Hao walioandamana Kinondoni wote hawana akili timamu, maana wangekuwa na akili timamu Mtulia alipoingia madarakani watu waliumizwa, leo yuko wapi? Kuandama kunihitaji watu ambao ni mentally retarded kwa hapa Tanzania
 
wananchi wa taifa hili kwa umbea tu kalagabhaho..wapo radhi wakose huduma muhimu zakijamii lakini washinde na kufuatilia umbea ...halafu mtoa mada kuna kitu bado hujakijua .
sis tuliopo humu mitandaoni ni sehemu ya watu wachache mno tuliopo ktk hili taifa ..naktika sis ambao tupo mitandaoni tumegawanyika kuna baadhi wanajitambua lkini wengine ni wafu wafikra..
sasa ukirejea huko mitaani daahhh hii mijadala inayoendelea humu huwezi kuikuta huko kabisa .mitaa imejaza vilaza kibao yaani kuna watu wao wanajionea sawa tu ilimradi jua linakuchwa na kuzama haya mengine yanapaswa kuamua hatima zao na vizazi vyao hawataki kujishghulisha nayo kabisa yaani ..in short nivilaza ..na hapo ndio watawala walipotuwza. kwa sbabu wanatambua kuwa wanatawala wafu wanaotembea
 
Picha ya woga watanzania tunayoitoa ni ishara mbaya kwa maadui au watu wanaoweza kuwa maadui zetu kutoka nje. Kuna mzee mmoja wa Kikurya aliwahi kuniambia jinsi Watanzania wengi walivyokuwa waoga wakati wa vita vya Kagera (sina uthibitisho wa maelezo yake).

Suluhisho ni maafikiano yatakayofanyika bila vyote vya habari au mitandao ya kijamii kujua. Makubaliano hayo yawe ni kuunda mfumo mpya wa kupata na kuendesha tume ya uchaguzi, mfumo mpya wa TAKUKURU kufanya kazi zake, mfumo mpya wa Jeshi la Polisi pamoja na usimamizi na uwajibikaji wake na ningependa na hata Mkaguzi wa fedha za Serikali apewe uhuru zaidi na hii itaanzia kwa jinsi anavyopatikana. Futa vyeo vya DC na RC. Kama ni mambo ya usalama wa wilaya na mikoa, muundo mpya wa jeshi la Polisi utalizingatia.

Kama umenotice sijaongelea katiba. Tanzania sheria zipo ila zaidi tunahitaji hasa vyombo imara na huru vya kusimamia sheria hizo vinavyofanya kazi bila upendeleo au uonevu kwa kundi fulani. Na kikubwa pia kuwe na utaratibu unaoeleweka kirahisi wa jinsi wa kuwajibisha vyombo hivyo vinapokiuka kanuni na sheria zinazoviongoza.

Nimegusia wazo la maafikiano hapa:
Njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani ni hii
 
wananchi wa taifa hili kwa umbea tu kalagabhaho..wapo radhi wakose huduma muhimu zakijamii lakini washinde na kufuatilia umbea ...halafu mtoa mada kuna kitu bado hujakijua .
sis tuliopo humu mitandaoni ni sehemu ya watu wachache mno tuliopo ktk hili taifa ..naktika sis ambao tupo mitandaoni tumegawanyika kuna baadhi wanajitambua lkini wengine ni wafu wafikra..
sasa ukirejea huko mitaani daahhh hii mijadala inayoendelea humu huwezi kuikuta huko kabisa .mitaa imejaza vilaza kibao yaani kuna watu wao wanajionea sawa tu ilimradi jua linakuchwa na kuzama haya mengine yanapaswa kuamua hatima zao na vizazi vyao hawataki kujishghulisha nayo kabisa yaani ..in short nivilaza ..na hapo ndio watawala walipotuwza. kwa sbabu wanatambua kuwa wanatawala wafu wanaotembea
Wapo bize na habar ya diamond na Zarri/ Nchi ya wajinga hii
 
Hata wewe utaishia hapo tu maana hakuna hatua utachukua mkuu
 
  1. Alipigwa risasi Tundu Lissu
    Watanzania wengi waliongea wengine wa waka-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tukaishia hapo. Hakuna hatua inayochukuliwa.
2.Kapotea Ben Saa Nane.
Watanzania wengi waliongea wengine wa waka-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tukaishia hapo. Hakuna hatua inayochukuliwa.

3. Kapotea Azory mwandishi wa habari ya Mwananchi.
Watanzania wengi waliongea wengine wa waka-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tukaishia hapo. Hakuna hatua inayochukuliwa.

4. Msimu wa Makonda
Watanzania wengi waliongea wengine wa waka-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tukaishia hapo. Vyombo vya kutetea haki za vyombo vya habari vikaalani vikali vikaishia hapo. Hakuna hatua inayochukuliwa.

5. Kifo cha Aquelina Akwilini
Watanzania wengi wanaongea wengine wa wana-post mitandaoni twitter, facebook, instagram tunaishia hapo. Wengine wanataka Mwigulu Nchemba ajiudhuru tutaishia hapo. Hakuna hatua itayochukuliwa.

6. Serikali awamu ya tano na usimikaji wa mfumo wa chama kimoja.

Watanzania tunaongea bila kuchukua hatua yoyote. Vyama pinzani nchini vinakandamizwa, kuwa mpinzani nchini ni jinai au hatia. Tuna kila sababu ya kusema chama tawala kinanunua viongozi wa vyama pinzani na moja kwa moja serikali inahusika. Kwa nini tunasema serikali inahusika? Serikali kama inaridhia kutoa pesa za kurudia chaguzi ndogo ndogo maana inafurahiswa na swala hilo. Bado wakishinda chaguzi ndogo ndogo wanafurahi, chaguzi sio za haki na huru kuna furaha ya kweli hapo? Unapigana na mtu umempatia panga wewe una bunduki nawe unasema ulipambana kweli kweli? Mpe bunduki nae.

Sisi tutakuwa nchi ya aina gani? Kuzungumza ndio suluhisho tosha? Ina maana hatujui mizizi ya matatizo yetu? Hatujui chanzo cha matatizo yetu?

Kwa nini tunashindwa kuungana watanzania? Kupelekea tunakuwa nchi ya waongeaji.

Tunakubali kugawanya na vyama vya siasa vyetu.Vyama vya siasa visitugawe tukashindwa kukemea na kutatua matatizo yetu na tukumbuke hamna tatizo la mtanzania mmoja mmoja bali kuna tatizo la watanzania.

Huenda ungekuwa wewe au mimi tungepigwa risasi au kutekwa utasemaje ni tatizo la mtanzania mmoja mmoja.

Kuwa mfuasi wa CCM ndio isiwe serikali ikikkosea au inapokosea au inapoiminya katiba ndio ushindwe kuungana na wengine au ushindwe kukosoa kisa tu wewe ni mkereketwa wa CCM hivyo hivyo kwa vyama pinzani.

CCM si zaidi ya utaifa wetu au Upinzani si zaidi ya Utanzania wetu au Utanganyika wetu au Unzanzibari wetu. Au tushindwe kuungana tutatue matatizo yetu ya Tanzania yetu kisa vyama vyetu vya siasa. Tanganyika au Zanzibari ilikuwepo kabla ya vyama vya siasa vyote nchini.

Jambo baya ni baya tu haijalisha nani amefanya awe babaako au mamako au ndugu yako litabaki kuwa baya tu.

Kifo cha Aquelina Akwilini tunajua tatizo ni nini, lakini tunatupiana lawama. CHADEMA walikuwa wanatumia haki ya msingi kikatiba ya MAANDANO HURU NA YA AMANI. Ni kosa kutumia haki yako kikatiba? CHADEMA ndio waliopiga risasi? Au Aquelina Akwilini alikuwa miongoni mwa waandamanaji wa CHADEMA?

POLISI ndio waliopiga risasi kwa mgongo wa kuzuia maandamano, Unazuia maandamano kwa kupiga risasi? Waandamanaji walikuwa na silaha? Halafu tunataka kuzui matumizi mabovu ya silaha au kuzuia maandaamano?

Mfano hili jambo lipo wazi tutataka kuleta uhusikaji wa vyama vya siasa, lakini chama tawala kinazungumzia upande mmoja kukishtumu CHADEMA. Lakini chama tawala kinasahau kuwa ndio chanzo cha matatizo yote.

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC si taasisi huru ipo chini ya chama tawala, NEC inashirikiana moja kwa moja na chama tawala. NEC nayo inapaswa kuwajibishwa, Lakini wa kuwa-wajibisha nani? Serikali au Bunge au Mahakama? Mihimili yote ni chama tawala, vinatumika na chama tawala na viko chini ya chama tawala.

Serikali inasema haina hela lakini inapata wapi mabilioni ya kurudia chaguzi ndogo ndogo hizi? Kwenye kuongeza mshahara wa mwalimu serikali inasema haina pesa, kwenye mambo ya msingi serikali inasema haina pesa.

Tuache siasa, tuache kuzungumza zungumza na tuache kulopoka lopoka tuchukue hatua ya vitendo stahiki.
Nataka nikueleze kitu mkuu watu wenye moyo wakujitoa muhanga niwachache zaidi ya waongeaji wengi.

Nini kifanyike hapa ishu ni "organization "hawa wachache mnakutanaje naniwapi mimi nipo Mara wewe upo iringa yule yupo mbeya?

Hii ishu kwa nchi kama tz ningumu sana kutokea tatzo elimu watu bado bado sana mno nahii ndiyo advantage ya ma ccm yanajua fika kabisa watanzania wengi ni zero.

Mtu anauwawa utasikia aliyataka mwenyewe au mimi hayanihusu ufisadi unafanyika utasikia atawakija wengine nao wataiba tu.yaani hayajui ata haki zamenyewe.
So my take😛unguza jaziba lafiki yangu kiukweli mimi binafsi sinaga msaada na mwana ccm yeyoto yule.
 
Back
Top Bottom