Nchi ya waalimu na madaktari wa mahakama

masumbwe

Senior Member
Oct 17, 2012
116
18
Wanabodi, ninayofuraha tena kuleta mada hii mbele yenu,ni nidra sana kusikia kuwa nchi inakuwa na walimu na madaktari wa mahakama.

Kauli hii imesikika siku za hivi karibuni hasa baada ya matokeo yasiyiridhisha ya vijana wetu wa darasa la saba na hivi sasa kidato cha iv, nami kama mwanajamvi nikaona niifuatilie kuona nini hasa kinachomaanishwa na wasemaji wa kauli hii na je kuna ukweli ndani ya kauli hii.

Ukiiangalia kwa undani kauli hii ina maanisha kuwa walimu na madaktari sasa wanafanya kazi kutokana na amri ya mahakama ambazo kwa nyakati tofauti mahakama ziliamua walimu warudi kazini na kusitisha mgomo kwa maana ni batili vilevile kwa madaktari, maamuzi hayo kwa kiasi kikubwa hayakuwaridhisha au hayakutoa suluhisho la madai yalikuwa yanatakwa na pande hizi mbili yaani walimu na madaktari kwa upande mwingine.

Hivi karibuni Rais wa chama cha walimu alinukuliwa na magazeti akisema mahakama iliamua serikali na walimu wakae katika meza ya mazungumzo lakini mpaka sasa serikali sikivu haijafanya hivo, ni kwa msingi kama huo sasa walimu wanafanya kazi si kwa utashi na dhamira ya dhati ya kuwasaidia watoto bali kutimiza wajibu na hivyo inakuwa bora liende.

Hli hii ni hatari sana hasa mfanyakazi anapofanya kazi katika mazingira yasiyommotisha (Motivation theories).

Kama mdau wa elimu nimekuwa najiuliza nini ugumu uliopo kwa serikali kukaa meza moja na madaktari au walimu na kwa pamoja wakatizama kapuni kuna nini na hawa watu wakapewa kulingana na kile kilichomo kapuni lakini majibu ya viongozi wakuu ya kwamba serikali haiwezi kulipa kiasi kinachodaiwa si kauli sahihi sana ambazo wakati mwingine husababisha sasa hao wanaojiona hawasikilizwi kutafuta njia mbadala ili kuonesha kuwa kumbe wao ni nao ni watu muhimu katika jamii fulani.

Mara nyingi madhara yake huwa ni makubwa, mengine yaweza kuonekana kwa wakati ule ule kulingana kada husika mfano kwa madakrari madhara yake yaweza kuonekana ndani ya kipindi cha muda mfupi lakini kwa walimu madhara yake yanaonekana katika kipindi kirefu kidogo kama haya yanayoonekana sasa ni matokeo ya kuwapuuza walimu kwa muda mrefu .

Na hili la kufeli ni kiapande kidogo tu cha madhara makubwa yanatarajiwa kulikumba taifa kutokana na walimu kutofanya kazi yao kwa usahihi, madhara mengine ni pamoja na kuwa na taifa lisilokuwa na watoto wenye maadili mema kwa kuwa walimu waliokata tamaa hawana muda wa kuwafundisha maadili mema ya kitanzania watoto hawa,mojawapo ya kazi ya mwalimu ni kumlea mtoto kimwili,kiakili na kiroho haya mambo matatu ni muhimu sana katika ustawi wa taifa lolote.

Lakini unapokuwa na walimu wa mahakama ambao wanasubiri tu mwisho wa mwezi ufike ni hatari.

Ukosefu wa malezi katika mambo hayo matatu niliyobainisha hapo juu unaweza kuleta taifa la vijana watumia madawa ya kulevya, wabakaji,wasiokuwa na utii bila shuruti,wezi wa mali ya umma,wasio wazalendo kwa nchi yao hata ukimwabia aende kupata mafunzo ya kuua watanzania wenzake somalia ataenda kwa kuwa uzalendo kwake ni sifuri na hajafundishwa shuleni.

W
atakumbuka waliosoma zamani ni kwa jinsi gani shule zilichangia kuwajengea moyo wa uzalendo wanafunzi.

Mwisho nafikiri mahakama kutumika kupoozesha manung'uniko ya wafanyakazi si suluhisho jema kwani tatizo linakuwa halijatatuliwa, ni vema serikali ikatumia majadiliano yenye maslahi kwa pande zote yaani watumishi na serikali kwa upande mwingine na ikumbukwe kuwa wanaounmia ni watoto wa maskini ambao wakati mwingine hata kulipa pesa ya kulisiti mitihani hawana hivyo mtoto anapofeli kwa mara ya kwanza ndiyo mwisho wa safari yake ndefu ya kutafuta elimu.
 
Ukweli ni kwamba walimu wamefanya makusudi tu wanafunzi wafeli ili serikali itie akili. Hapa walimu wameishika pabaya serikali.
 
Ukiangalia kiundani serikali haina fikra kabisa kwan huwez mtu yule yule mwenye mgogoro nawe ukamtumia kwa kazi na ukategemea jipya kutoka kwake au kazi nzuri hayo wameyataka na yatazidi kutokea. Hongereni walimu kwa kufanya kazi kwa shuruti ya mahakama mbinu ni nzuri songeni mbele
 
Kwa hapa tatizo siyo serikali bali mahakama imeshindwa kutoa haki sababu ya kuogopa waliowaajiri.Kwa maana hiyi Mahakimu angalieni mlichokifanya kma kesi ya waalimu na Madaktari mngeziamua kwa haki haya yasingetokea.

Hakuna wajibu bila haki.
 
kawambwa hakujua haya ndiyo maaana hata majibu yake hayakueleweka. taasisi yoyote mbali na kuwekeza katika rasilimali zingine, ni lazima tena si hiari iwekeze ipasavyo katika rasilimali watu maana ndio wanao-organise vyote katika taasisi ili vifanye kazi na kile kilichokusudiwa kipatikane. Katika elimu, walimundiyo haswa wanapaswa kuangaliwa vinginevyo mtapiga makelele sana na hakuna kitu kitakachobadilika. Serikali wasikilizeni walimu madai yao. maabala, vitabu, majengo na kila kitu kingine bila kuwasikiliza walimu ni bure.
 
Back
Top Bottom