sir. Mwasongwe
Senior Member
- May 30, 2015
- 106
- 76
NCHI YA UPEPO
Ni hadithi fupi iliyotungwa Na Isack Mwasongwe mhitimu wa chuo kikuu mwaka 2015 chuo kikuu cha Eckernforde Tanga.
NCHI YA UPEPO.
si shwari katika nchi ya upepo iliyozungukwa na milima na mabonde ardhi iliyojaa rutuba yenye madini ndani yake na dhahabu tele kila kona na misitu mikubwa iliyobeba kila aina miti, wanyama, na kila aina ya viumbe watishao na wasiotisha, watalii hujimwaga katika mbuga za wanyama na maeneo mengi yanayovutia. Upepo huvuma pande zote za miji na kusababisha mvua nyingi baadhi ya maeneo na kufanya kukosa mvua kabisa mvua ambayo husababisha wakulima na kuvuna mavuno mengi na kuendesha maisha yao raha mstarehe na wengine kukosa mavuno kutokana na mvua kupita kiasi. Nchi hii ya upepo iliongozwa na kiongozi aitwae Ndele kiongozi huyu alitwaa madaraka kutoka kwa kiongozi aliyejali sana maisha ya wananchi wake aliowaongoza na viongozi wake wasaidizi pia walifanya kazi kwa moyo mkuu kwa kuhakikisha huduma bora zinapatikana na kukidhi mahitaji yote. Uongozi huo uliopita ukaachia madaraka na kumkabidhi Ndele kwani ndiye aliyeshinda wakati wa uchaguzi.
Pungapunga ni kijana aliyekuwa mzalendo aliyefuzu masomo ya chuo kikuu, alijitolea kuhakikisha kwamba anatumia elimu na ujuzi alioupata kwani alisomea masomo ya sheria hivyo alikua amebobea katika fani ya sheria lengo lake la kusomea fani hiyo ilikua ni kutetea haki za wanyonge. Licha ya kusomea fani hiyo na kuwa mtetezi wa wanyonge alikumbana na misukosuko mikubwa sana na hatimaye kumwagiwa tindikali usoni baada ya uongozi huo kuona jitihada za pungapunga zikiwa zinasonga mbele kwa mafanikio makubwa kwani alitetea taifa lake hususani wanyonge kama vile mama mjane ambaye alikuwa anajishughulisha na ujasiliamali na kujipatia fedha ambazo alilisha familia na kusomesha wanawe, mama mjane pia alikuwa na klabu aliyokuwa akiuza pombe ya kienyeji pia mama huyu alikuwa na shamba kubwa aliloachiwa na mumewe baada ya kifo chake lakini shamba hilo lilinyang’anywa na wenye mifuko mirefu.
Viongozi wa nchi ya upepo ikiongozwa na Ndele walijadiliana namna ya kuongoza na kutawala nchi hiyo ya upepo wakishilikiana na wafanyabiashara maarufu wenye mifuko mirefu miongoni mwa hao ni Chidumu ambaye alimiliki mali nyingi sana nchini hapo miongoni mwa mali alizozimiliki ni baa kubwa na maarufu iliyojulikana kwa jina la ‘katakiu shusha pumzi’ ambayo ilitumiwa na viongozi wakubwa hapa nchini kama Ndele, Mbwiga nawingine wengi. Katika baa hiyo kuna ukumbi ambao ulitumika kufanyia vikao mbalimbali na kusaini mikataba mbalimbali huku wakijipatia vinywaji mabalimbali na kuchangamsha akili kuiweka sawa.
Radi ngurumo na mweko mweko wa upepo ulizuia vijana kuona mbele, wazee walionekana kupapasa kwa sababu ya vumbi zito lililopeperushwa na upepo huo, wakina mama waliziba nyuso zao kwa vilemba vyao ili kuzuia takataka zilizokuwa zimebebwa na upepo zisiwaingie machoni mwao, sauti za vilio zilizoashilia machungu ziliendelea kusikika toka kila mahali. Zingine zilielekea kufifia na zingine zilizimika kwa maumivu makali yawapatao watoto. Nchi ilighubikwa kwa gugumizi la sintofahamu. Pungapunga anazunguka zunguka huku akijisemesha nchi ya upepohata lini itakuwa nchi ya..… tumechoka tumechoka!
Sauti toka ndani ya gugumizi hilo la sintofahamu ilisikika ikiwatia watu moyo kusonga mbele kwa hatua shupavu ili kuepa msukosuko wa upepo, sauti ya Pungapunga haikukoma hata wakati ngurumo zilipopasua ngoma za masikio ya watu. Sauti ya mama mjane ikasikika ikisema tujipe moyo na tuhimeni wim,a ikiwaamrisha watoto, wazee na vijana na wamama, ikiendelea kusema nyamaza nyamaza tazama mbele kule mbali pokea pokea pokea mafanikio yako ni mafanikio yaliyo kuwa yakisukwa sukwa angani kwa nguvu za upepo mkali, mashavu yaliyokuwa yamechorwa michilizi ya machozi, midomo iliyoachwa wazi na pua zikiendelea kuchuruzisha kamasi zilionyesha matumain ya nyuso zao za kupaa kwa mbawa kuyanyakua mafanikio angani.
Kama ilivyo ada ni asubuhi nyingine ya mwisho wa mwezi ambapo wafanyakazi wengi wa serikarin hawaendi kazini kwa sababu ya mapumziko maalumu ya mwisho wa mwezi. Hapo ndipo mjomba anajikuta yupo sehemu nzuri ya kupata kinywaji na marafiki zake katika baa ya ‘katakiu shusha pumzi’ na sauti yake iliyo kuwa nzito kama sauti ya simba dume, na nyuso za bashasha zinazo shabihana na mifuko yao zikionyesha uhai wa mifuko yao kwani wafanyakazi walikuwa wamevuna mavuno ya mwezi. Ikawa ni siku nzuri pia kwa mkuu wa nchi ya upepo kutumia mda huo kuwasiliana na askari wa nchi ya upepo kwa njia ya simu ya upepo kama dakika moja hivi kuwaamuru kuwakamata wanakijiji watatu.
Mama mjane akiwa hana mbele wala nyuma akisikia sauti ya mwanawe wa kike akisema alaaniweee sauti hii ilimgusa mama mjane na kumsogelea mwanawe wakaketi chini ya mti wenye kivuli murua na kasha akasogeza kilago ambacho ndicho kitanda chao na wakakalia wakitazamana. Mwanawe alikua analia sauti ya chini sana mama mjane akamnyamazisha. Mama mjane akapiga ngumi shina la mti na kufoka “huyu Ndele ni nani?” mwanawe alimueleza kuhusu kukamatwa kwa washahidi wa kesi yao waliofungua baada ya kuuzwa kwa shamba lao kubwa lililokuwa pembezoni mwa mji mkuu wa nchi hiyo. Alikua ni Ndele mkubwa wa nchi ambapo alipokea kitita cha pesa kama billioni tatu na nusu hivi toka kwa kizito ambaye alinunua shamba la mama mjane ambalo alikabidhiwa baada ya kifo cha mumewe aliyelimiliki kwa mda mrefu sana baada ya nyaraka za serikari za uhalali wa mmiliki mmoja wa shamba lilelile hatimaye akafanikiwa kulitwaa na kuwa mmiliki halali.
Ni masaa machache tangu mjomba aingie baa na kujumuika na jamaa zake katika baa ya ‘katakiu shusha pumzi’ wakiendelea kupata vinywaji mbalimbali na kuchangamsha akili ghafla mjomba anaitwa kwa nguvu na askali njoo tupo huku, sasa wanajikuta wapo watatu, Pungapunga akauliza mbona umechelewa? Askali alisikika akisema Ndelechanzo mjomba alirukia kwa maswali… kafanya nini? Na ulikua naye? Nilikua na mzungumzo naye na…... lakini subiri ni shushe chupa mbili tatu hapa, wote wakacheka. Baada ya mda kidogo aliinuka na kucheza mziki kidogo ulikuwa ni wimbo uliopigwa siku akikabidhiwa majukumu na Ndele zilikuwemo Pesa nyingi ambazo kazi ya pesa hizo ni kuwaangamiza wale wote waliojitokeza kutetea haki za mama mjane ya shamba alilonyang’anywa. Hali hii ilimkera sana Pungapunga kusikia hivyo na alijisemea moyoni nina haki ya kutetea haki ya wanyonge inayodhurumiwa na baadhi ya wenye nguvu za kifedha hapa nchini. Alihapa kupambana kufa na kupona. Yule askari akaendelea kuwaambia wajivinjari bila wasiwasi kwani yeye kama mtetezi wa serikali katika kesi hiyo ya mama mjane amepewa mtonyo na bosi huyo ambaye anapesa za kuajiri watu wa kila aina kwa ajiri ya kuhudumiwa kila wanachokihitaji hapa duniani.
Sasa mama mjane anafuraha kubwa ameshinda kesi kwa mgongo wa Pungapunga na maisha mapya yanaanza kwa mama mjane, hakika kila mwananchi alimsifu Pungapunga kwa kutetea haki za wanyonge kama mama mjane wasio na mifuko ya fedha. Ama kweli tazama mara moja nyuma ukirudia mara ya pili upepo wa nchi utakutimulia vumbi. Pungapunga alipambana na upepo huo hakujali vumbi alilotimuliwa hatimaye alifanikiwa kutetea haki za wanyonge zinazo dhurumiwa na kuchukuliwa na wenye mifuko mirefu ya pesa. Mama mjane akizungukwa na wateja wake wa pombe wengine wanaimba baada ya kulewa pombe za kienyeji …jua lile litelemke mama, ayayaa yaa iya mamaa nyota nazo zitelemke mama ayayaa yaa iyaa mama….. na wengine wanampongeza kwa upishi wa pombe kali. Kando ya kibanda chake makuti kilichokandikwa kwa matope yalioanza kubomoka wameketi watoto waliosheheni michirizi ya machozi mashavuni, pua zinazoendelea kudodonsha makamasi na mzozo wa nzi unawazunguka. Watoto hawajala wala kunywa yapata saa 11 jioni. Mama mjane anawaagiza waondoe rapurapu lililotupwa kwenye kibao kilichoandikwa ‘never miss bar’ nyoyo za watoto zikaanza kughubikwa na tamaa ya matarajio wakati mataya yakiumia kwa miayo waliyopiga kila mara.
Ikiwa asubuhi na mapema jua linaanza kuchomoza kuashiria kuanza siku mpya sauti za ndege wakifurahia siku hiyo zilisikika, pia watu walisikika wakihabariana na kujuliana hali. Pungapunga alikua akijinyoosha nyosha juu ya ‘teremka tukaze’ huku amelala kifudifudi akipanga kile na kupangua hiki bila kufikia hitimisho huku akiwa katika dimbwi kubwa na zito la mawazo mara mlango uligongwa na Mbwiga aliingia bila kusubilia welcome akisema mshikaji mbona umeuchapa hadi saizi? Mbwiga aliuliza, Pungapunga akajibu si unajua upepo jana ulikua mkali mithili ya mbogo aliyejeruhiwa msituni joka la mdimu hulinda watundao… vipi kwani kuna ishu gani? Punda anabebeshwa mzigo lakini anatandikwa mijeredi na kupe akiendelea kunyonya ndo habari ya leo mchizi.
Mnyonge hana haki chini ya jua umezaliwa masikini, unaishi kimasikini, unakufa kimasikini na kuzikwa kimasikini… duu na leo biashara hakuna na yule askari na leo ataleta miguu yake hajali kama umeuza au laa! (alilopoka maneno yote bila kujali kama wateja wanamsikiliza) Pungapunga akamuuliza mama mjane mbona unaachia makombola makubwa makubwa na mazito? hadi tonge lanikwama! Mama mjane akasema daa! koti zito lakini hawalijali wamelimwagia maji bila ha….. Pungapunga akasema haki kakimbia katuachia majabari yakibirukabiruka! lakini leo mama haupo normal. Ni kweli mwanangumaji yamezidi unga kila kukicha ni afadhari ya jana biashara imezorota sokoni hapaendeki ushu….. hee wale wanakuja tena! Asalalee! Nimekwisha nitafanya nini masikini mimi leo sina kitu na watoto wamefukuzwa shule walee!, askari “hebushika risiti yako kabla hatuja kubeba na kibanda chako. Mama mjane baba yangu leo sijauza biashara mbovu nitatoa wapi shilingi 500 mi mama mjane…. hatuhitaji maelezo yako tupe chetu unafikiri sisi tutakula wapi? Mama mjane kajitetea sana naombeni mje machweo, wewe mama usituletee longolongo tutakupeleka sero, kweli baba zangu nitawapa na cha miguu, aya baadaye usituletee longolongo pumbavu mkubwa wewe. Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni.
Ndere na Mjomba wakiwa ofisini wakijadiliana mambo kadha wa kadha kuhusu mipango yao huku wakijipongeza kwa jinsi nchi ya upepo inavyo vuma kama kimbunga, iking’oa majabari makubwa na kuzamisha ngalawa zinazozuka kama kichuguu cha mchwa. Upepo unavyo ezua vijumba vya buibui na kujenga kiota. Upepo wenye makucha ya kumlarua kila mtu mwenye kiburi.
Mjomba hebu mwite mbwiga kuna faili hajaniletea hapa, ndiyo mkuu (mjomba aliitikia kwa heshima huku akimuogopa mkuu wa nchi ya upepo), mbwiga niletee faili la invoice na hakikisha kila kitu umerekodi kwa ufasaha, sawa mkuu bwiga aliitika huku akitetemeka akimtetemekea Ndele na kumnyenyekea kama Mungu. sasa mjomba agiza kila askari akusanye ushuru kama inavyo stahili bila kumuonea huruma mtu wala kumuonea haya bila hivyo upepo wa Ndele utampitia na utampeperusha kama makapi utampeleka hadi nchi ya saba na kumrarua rarua vibaya kama radi iraruavyo mti. Sawa mkuu mbwiga anasikiliza maagizo kwa makini sana, maagizo yote mjomba aliyapokea na Ndele akafurahi sana kwani amepata habari mpya ya kumwambia Pungapunga kwani yeye anapenda kuonekana mtu wa habari mpya.
Lakini Ndele kunawatu ambao hawataweza kumudu ushuru huo? Nitafanyaje? Wewe umesha anza upumbavu upumbavu, nitakupeperusha ning’oe visiki vilivyoota katika akili yako. Nani kakuambia nchi ya upepo kunamajadiliano au hapanahujui sheria za nchi ya upepo, hujui…. hujui…. hujui? Ndele alionekana mwenye hasira sana mjomba alimuomba msamaha na kumwahidi kuwa atatekeleza maagizo yote.
Ok! Ok! na vipi kuhusu wale wafanyabiashara hasa yule Chidumu anavuna vizuri sana udongo mwekundu, ndiyo mkuu. Mara Chidumu anaingia akiwa na briefcase yake . Ooh! Karibu sana hatuja onana, kuna jambo lolote jipya kuhusu udongo mwekundu? Anakaa vizuri kwenye kiti huku akijitengeneza tai yake kwa madaha, ndiyo bwana mkubwa nina habari nzuri sana. Ooh! yes habari gani unakuja na kitu kidogo, ndiyo mkuu nahitaji uniongeze eneo la kuchimba udongo mwekundu (anafungua briefcase yake na kumuonyesha ndele manoti ya pesa Ndele macho yanamtoka midomo inatetemeka) a-a-aah! Umefanya vizuri sana si unanijua mimi huwa sibabaishi, kweli bwana basi jioni nitakuja kwenye baa yako nitakupa jibu kamili. Asante bwana mkubwa.
Pungapunga anafika nyumbani na kujitupa chini huku akiwa na mawazo mengi, ubongo wake ukifikiri na maswali haya na yale kuhusu nchi ya upepo inapoelekea. Pungapunga anasimama wima na kuanza kuropoka “lazima mapinduzi yafanyike mapinduzi ya kung’oa umasikini, mapinduzi ya kuvua koti la umasikini nooo.... mapinduzi ya kungoa majabari ya kubiruabirua milima, mapinduzi ya kuzamisha meli na kuokoa ngalawa, mapinduzi ya kung’oa mikuyu na kutawanyisha upepoooo! Aaah aaah aaah. Pungapunga alicheka sana huku machozi yakimtoka kama maji pua nazo hazikuwa nyuma zikashiriki uchungu naye kwa kutiririsha makamasi. Akajigonga kwenye ukuta bila kujijua akadondoka chini puuuu kama embe lililooza likianguka toka mtini na kisha akapitiwa na usingizi hapohapo. Pungapunga alilala fofofo huku damu zikimtoka kwenye paji la uso wake alilala kwa mda mrefu sana.
Mbwiga aligonga mlango kwa mda mrefu sana bila kuonekana dalili yoyote ya mwenyeji kuwepo kufungua mlango huku roho yake ikirukaruka kwa habari alizokuwanazo alitamani kumuona rafiki yake kumpa habari. Aliamua kusukuma mlango kwa hasira na kumgonga Pungapunga aliyekuwa amelala chini. Pungapunga alijizoazoa hapo chini na kujaribu kukaa huku jitihada zake zikishidwa ndipo akasaidiwa na mbwiga ndipo akasimama. Mbwiga alishangaa vipi mshikaji mbona unauchapa usingizi tena chini au siku hizi kitanda kinaripiwa ushuru? Aah mshikaji yule Mazi wamemtia hasira sana wamemburuta yule mother pale kijiweni daah! Mazi yupi? Pungapunga aliuliza, mazi wapi si wale askari wasiojielewadaah1 mshikaji nina info si unajua mimi ni mzee wa manews tu.
Kunanini? (pungapunga aliuliza) Bwana na wewe kwa kujisifia si Ndere ameaagiza wale mazi wakusanye ushuru alafu amepokea bonge la kitita toka kwa Chidumu yule mmiliki wa baa ya ‘kata kiu shusha pumzi’ ili amuongezee udongo mwekundu. Pungapunga akaropoka huku akinyanyua mikono juu ishara ya kuomba ujasiri kwa Mungu mapinduzi mapinduzi lazima tufanye mapinduzi lazima tujifunge mkanda tupigane kufa na kupona, kulivua koti la umasikini kutafuta mbiu ya haki. Sasa rafiki yangu mbona kama paji lako la uso linavuja damu? damu! damu! damu! ya kusafisha umasikini alama ya mnyonge, damu ya kusambaratisha upepo. Kesho tukutane na washikaji pale kijiweni mwambie na yule askari wetu aje tumpatie maagizo ya kufanya mapinduzi na njia zote za kuzifuata ili kufanikisha lengo letu.
Hellow! Ndiyo ndo mimi Chidumu, ok ok jaribu kuwaweka vijana vizuri, usijali mimi ndo Chidumu huwa sibabaishi nikiamua kufanya kitu lazima kifanikiwe, ok kesho njoo kwangu.
Ooh! bwana karibu, karibu sana, leta vinywaji vya kutosha akimwamlisha mhudumu, nadhani ni wewe nilikuwa nakusubiri nadhani umekuja na ujumbe mzuri, ndiyo nimekuja nao ujumbe…. hebu ongeza vinywaji hapa, bwana Ndere mwongezee Chidumu sehemu kubwa ya kuchimba udongo mkubwa ambao upo kwenye rutuba nzuri. Chidumu alitabasamu huku kitambi chake kikimtoka kulia kushoto akifurahia kupatiwa sehemu kubwa zaidi. Wanakunywa sana huku wakijipongeza mara mjomba na mbwiga wanaingia na kujiunga na kunywa sana. Punde si punde warembo watatu wakiwa wamevaa vimini vilivyoishia juu ya magoti huku vibrauzi vyao vikiwa vimeacha mgongo wazi na matombo yao yakiwa wazi hayajasitiriwa kisawasawa na kuwachanganya viongozi hao waliokuwa wakipata vinyaji waliingia pale walipokuwa wakipata vinywaji wakaambatana nao huku macho yakitamani kutupia neno na huku mate yakiwadondoka kama mbwa aliyechoka. Chidumu akawapa kumbato motomoto na mabusu tele na kuanza kupiga story za kimahaba na hatimaye viongozi wale waliokuwa na Chimudu pale wakagawana na kuelekea gest house iliyopo pepmbezoni mwa baa hiyo wakaendelea na kila mmoja na chumba chake wakafurahi huko na kupeana wanavyopeana. Chimudu na wenzake walipo amka asubuhi wakajikuta wapo pekeyao na kila kitu hakipo kwani wale warembo walijipatia fedha na simu za kisasa.
Pungapunga akiwa katika mkutano alioitisha na askari wao akiwa pembeni kuhakikisha ulinzi ukiwepo pale kijiweni. Pungapunga akawa anahutubia huku machozi yakimtoka jamani masikini wenzangu nchi hii ya upepo imekuwa ikiendeshwa kwa kutunyanyasa sana ukiangalia viongozi wanateuana kiurafiki tuu hebu angalia waziri mkuu ambaye ndiye mtendaji mkuu ni rafiki yake mkubwa sana Ndere, ukiangalia kiongozi wa wa ujenzi wamesoma naye na wengine wengi lakini kutokana na muda hautoshi nisiendelee sana. Sasa ndugu zangu nchi hii ya upepo tutavumilia hadi lini maana hata udongo wetu tunanyang’anywa na wenye mifuko mirefu watoto wetu hawapati elimu bora bali bora elimu kwasababu majengo ni mengi ya kusomea lakini wakufunzi hawajitoshelezi ukiangalia watoto wa viongozi wa nchi hii ya upepo hawasomi katika majengo haya ndiyo maana watoto wetu wanapata bora elimu na… mama mjane akadakia na kuanza kusema hebu angalieni jamani mimi mwenyewe nimenyang’anywa udongo wangu tena sina hata pa kuchimbia mhogo mwee! nitaishi vipi na watoto wangu na wanasoma shule hivi leo wamefukuzwa shule sina karo ya kulipia na kila siku ushuru wanachukua hatakama sijauza hawanielewi sasa mimi ninaamua kuungana na Pungapunga kupigania haki yetu kwa kila njia ili tuishi kwa amani kama wenyewe wanavyoishi.
Pomole naye hakuwa nyuma na wenzake akasema yake mengi sana jamani viongozi wetu wapo hanimuni hadi leo hii maana huduma bora hakuna maji kila siku tunahangaika tunateka maji mbali sana takribani kilometa 11 ukienda kuteka katika bomba la kijiji foleni kubwa na tunachajiwa pesa wakati ushuru tunatoa, barabara zenyewe hazieleweki mashimo matupu kila siku magari yanapaki barabarani kwa kuvunjika spring za gari na mapancha mengi yanatokea kwasababu ya mashimo haya na viongozi wenyewe wanatumia ndege kusafiria hawajui athari za huku kwetu, hata muwakilishi wetu mwenyewe hana mchango wowote kwetu kwani hadi leo hajaja kijijini tangu apate uongozi hataki kuja kuangalia hali ya wananchi wake pia hosipitali zenyewe hazieleweki wake zetu wanakufa kwa kucheleweshwa kupatiwa huduma hii ni shida wakati ushuru tunatoa mkubwa sana, pia umeme wametuahidi ni miaka mitatu sasa tangu waingie madarakani hakuna kitu chochote hata mashimo ya kusimika nguzo hamna, ukifika muda wa kuchagua uongozi utawaona wanasogeza miguu yao taratibu kama bata aliyepigwa shoti ya umeme nakuanza kuturubuni tena mimi sioni haja ya kuendelea kupoteza muda tena hapa tuondokeni tufanyeni maandamano jamani ajira wametuahidi lakini hadi leo tupo mitaani tukidaiwa ushuru wakati hatuna ajira zinazoeleweka ni maonezi matupu yani.
Mama ntiliye akamung’unya maneno chini kwa chini na kisha akasema kwa sauti kubwa jamani hali si shwari kabisa mimi na mume wangu Ponjola tumeoana ni miaka nane yapata, lakini hali hii ya maisha imekuwa mbaya sana tumeshidwa kuzaa watoto wengi kwasababu hatuna chakula udongo mwekundu wote umenyang’anywa na Ndele na serikali yake na kuwapatia wale wageni eti wanakuza uchumi wa nchi ya upepo lakini hawalipi ushuru hata kidogo halafu sisi tuliporwa udongo wetu hatuna udongo tunalipa kodi , haya ni maonezi makubwa na kamwe siwezi kukubaliana na hali hii hata ki… eti ‘mgeni njoo mwenyeji apone’ sasa tumepona vipi hapo matatizo chungu mzima yanaatuandama na huku wao wakiwa wanaishi maisha ya mkoyeko.
Mbwiga akadakia na kusema jamani mimi kama mnavyojua ni kiongozi tupo pamoja na ni mtu wa manews kama kawaida sasa hata mimi huwa naumia sana watu wanakamatwa hovyo pasipo sababu kwa mfano kuna vijana wamekamatwa jana wapo ndani kwa kosa la kuuza sigara kubwa wakati wapo viongozi tupo nao ofisini kwangu wanasafirisha cocaine toka Jamaica, malasya na nchi nyingine lakini hawakamatwi na wala hawalipi ushuru na askari wanajua hilo yaani na…….. tuungane tuweni kitu kimoja tupiganie haki zetu tumechoka kudanganywa danganywa na viongozi hawa ahadi zao ni za uongo hakuna ukweli hata kidogo. Mfano mkuu wa nchi hii ya upepo anaposafiri anatumia bilioni kumi na mbili kwenda na kurudi ni bilioni ishirini na nne. Hiyo ni safari ya nchi jirani tuu hapo huu ni wizi na ukizingatia ni ushuru wetu jamani. Natusimame hima tunaweza endapo tuta kuwaa na umoja lakini tusipokua na umoja hatuwezi hata kidogo. Andongolile akaunga mkono na akasema hivi jamani nani anataka kuendelea kuwa masikini?, nani anapenda kuonewa? Nani hataki mabadiliko? Nani hataki watoto wetu wapate elimu bora na si bora elimu? Nani anataka kwenda rokapu pasipo sababu maalumu? Nani anataka udongo wake unyang’anywe kama mama mjane alivyo nyang’anywa na wengine wengi walioonewa na kuwapatia wageni na wenye mifuko mirefu ya fedha?.. Andongolile alipo uliza maswali haya alikaa kimya na wengine wakiwa wanatafakari huku vichwa vyao vimeinama chini kama mwanamke aliyefumaniwa akiona aibu. Watu sifufu walitiririka kama maji ya mto yatiririkavyo kuelekea baharini huku wengine wakiwa wamevaa pajama kwani walichanganyikiwa baada ya kusikia kerere za shangwe zikilindima kijiweni ambako walikutana kupanga mikakati ya ukombozi wa nchi yao.
Ndipo vijana na wazee kwa rika zote wanajikusanya pale kijiweni na kupanga mipango madhubuti ya kufanya mapinduzi wakakaa kimakundi makundi vijana walikuwa wengi sana kama utitiri kwasababu hawana ajira japokuwa wana elimu ya juu, wakiwa wamechoka sana sura zao kwa sababu ya kupeperushwa na upepo mkali wanajikusanya na kufanya mipango wote wanakubaliana kufanya maandamano na kuandika vipeperushi vinavyoweza kufikisha ujumbe kwa majabari kazi hiyo ya kuandika hizo jumbe alipewa mbwiga mara askari wanatokea wakipita njiani wakiwa ndani ya karandinga wakaanza kuwapiga mawe huku wakiimba mapinduzi! mapinduzi! mapinduzi! , masikini lazima awe tajiri na tajiri awe masikini ooh! nchi ya upepo. Hapo hapo wanawake waliingia, wazee walikuwa wanaenda mashambani wakatupa majembe chini na kujiunga huku wakiimba na kufanya mashambulizi kwa wale askari kwani walikuwa na hasira namna wanavyokusanya ushuru kwa maonezi makubwana askari pia wakaanza kuwapiga wale wananchi kwa mabomu na mijeredi ililindima katika miili yao lakini walishikamana kama siafu wavukapo mto wakawa kitu kimoja wanafunzi, walimu, na mama ntilie nao wakajiunga. Upepo mkali ukavuma hadi miamba ikaanza kuachana, majabari yakatetemeka, upepo ukawa mkali ukaitwa kimbunga..... .
Itaendelea wakati mwingine.. 0758978644