Nchi ya kitu kidogo

Ni nchi ya watu wadogo. Juzi natoka Lushoto nimefika Korogwe-maili kumi kuna viji askari vikanisimamisha, nikapaki vizuri kabisaaaa. Akaniomba akaniomba akague gari nikamkubalia. Akataka leseni nikampa. akataka fire ext nikamwambia tangu nilipie TRA hawajanipa.....akashtuka kidogo. Akaniambia Mzee toa basi chochote aaaggg nikamwambia kijana sina kitu labda parachichi maana natoka home. Alivyomjinga eti akasema nipe basi ambayo yameiva ili tule kabisa.......vina njaaa hadi vinatia kinyaaa
 
Mwenye njaa usimnyime chakula, Mola atakujazi...

Nakuunga mkono mkuu wana njaa sana hawa, hata ujeuri wanaotufanyiaga ni kutokana na njaa inayowasumbua. Wengine ukitazama hata mavazi/sare walizovaa zimechakaa zinatia huruma. Bila matumizi ya sanduku la kura 2015 maisha yatazidi ugumu.
 
Hivi mshahara wao ni shs ngapi? Yaani kwa asiye na cheo.

To move the world we must first move ourselves - Socrates
 
Dawa yao hawa ongea nao ung'eng'e wataishia kukutakia safe journey, ishanisaidia sana hiyo.



Walishanikamata nikatumia njia hiyo walikuwa wanne,nikawasikia wanasukumiziana wewe si unajua
kiingereza ongea naye basi jamaa akaniamboa sorry sir,mimi huyo nikaishia zangu huku kicheko kimanikaba nikaenda kuchekea mbele ya safari...
 



Umenichekesha sana kaka nikikumbuka wale jamaa wanaosimama kabla hujaffika Mdaula walishanisimamisha wakaanza kuniuliza maswali yao nikawapa kila walichotaka mmoja akaniambia hebu washa redio nikajiuliza sasa redio yangu inahusiana vipi nikawasha mwisho kabisa jamaa ananiambia tuachie basi hata ya chai kaka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…