Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 761
- 1,482
Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa madini. Kiwango cha kuitwa "Bara tajiri zaidi". Siasa haijakaa kando katika suala zima la madini ambapo kwa baadhi ya nchi imeleta mfumo wa maendeleo ya kiuchumi na baadhi ya maeneo imekuwa laana kutokana na mifumo mibovu ya kisisasa.
Swali ni kuwa je kiwango hiki cha utajiri kimesaidia nchi za Afrika kwenye maendeleo ya kiuchumi?
Zifuatazo ni nchi 5 zinazoongoza kwa utajiiri wa madini barani Afrika kwa mujibu wa uchunguzi wa kisayansi na taarifa mbalimbali.
1. Botswana
Botswana ina inahifadhi ya asilimia 35 ya madini ya Almasi barani Afrika. Pia ndio wanaouza almasi nyingi zaidi kutoka Afrika. Lakini pia wanazalisha madini mengine kama shaba, dhahabu, nickel na soda ash.
2. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Inakadiriwa DRC ina hifadhi ya madini ambayo hajajaguswa yenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 24, pia inazalisha asilimia 34 ya almasi na shaba asilimia13 kwa Afrika. Pamoja na hayo DRC ni miongoni mwa nchi maskini.
3. South Africa
Afrika ya Kusini hii ndio nchi yenye uchumi imara na tajiri zaidi barani Afrika. Uchumi huu imara umechangiwa kwa kiwango kikubwa na sekta ya madini. Dhahabu na shaba ndio madini yanayozalishwa zaidi nchini Afrika Kusini.
South Africa ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha madini yafuatayo Chrome, Manganese, Platinum, Vanadium and Vermiculite na ikishika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa madini ya Ilmenite, Palladium, Rutile, and Zirconium.
Hawa uchumi wao unashabihiana na kiwango chao cha madini.
4. Tanzania
Tanzania licha ya kuwa mzalishaji namba nne kwa Dhahabu yote barani Afrika Tanzania asilimia 3 tu GDP kutoka katika sekta ya madini.
Tanzania ina hifadhi kubwa ya madini ya chuma, nickel, shaba, cobalt, fedha, almasi,tanzanite na mengine mengi. Hapa napo hakuna mlinganyo kati ya uchumi na utajiri wa madini.
5. Namibia
Nchi ya Namibia imejaaliwa kuwa hifadhi kubwa ya madini. Inazalisha asilimia 46 ya madini ya Uranium ikichangia asilimia 25 ya Pato la taifa. Huku kidogo madini yameleta maendeleo ya kiuchumi. Kesho tutaangalia hali za kiuchumi ya nchi hizi.
Source: World Bank
@military_Genius