Nchi nyingine zijifunze toka China

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,061
Nchi nyingine zijifunze toka china.
China hawana mashart ya ajabu ajabu, china ni rafiki wa kweli.

Bado kauli hii sijaielewa naomba wenye kujua wanijuzee,
kwanza hizo nchi zenye mashart ya ajabu ajabu ni zipi, hayo mashart ni yapi?

Je nchi hizo bado tuna balozi zao hapa?
Ikitokea nchi hizo zenye mashart ya ajabu ajabu wakajitoa katika kufadhili miradi na misaada tutaweza kujimudu?

Kulikua kuna ulazima wakuyaongea hayo mbele ya wananchi?

Wasalaam
 
Mkuu,wachina wana masharti nafuu kwani wao hawaingilii siasa za nchi yeyote!nyie mchinjane,muuane na hata mchakachue kura,mchina atanyamaza kimya as long as nyama ya punda aipate,meno ya tembo kama kawa na gesi ya nchi tajwa!ila wale wa magharibi tukichakachua kura wanalongaaa japo kutuibia wanatuibia!na misaada yao wakikasirika tunaikosa...ila mchina hana hayo!
 
Nchi nyingine zijifunze toka china.
China hawana mashart ya ajabu ajabu, china ni rafiki wa kweli.

Bado kauli hii sijaielewa naomba wenye kujua wanijuzee,
kwanza hizo nchi zenye mashart ya ajabu ajabu ni zipi, hayo mashart ni yapi?

Je nchi hizo bado tuna balozi zao hapa?
Ikitokea nchi hizo zenye mashart ya ajabu ajabu wakajitoa katika kufadhili miradi na misaada tutaweza kujimudu?

Kulikua kuna ulazima wakuyaongea hayo mbele ya wananchi?

Wasalaam

Mkuu acha kuishi kwa hofu ya wafadhiri na misaada! Hakika nakwambia nchi hii inauwezo wa kujiendesha bila wafadhiri na misaada yao, ni sisi tu kua tayari kuishi maisha hayo. Ila kwa hulka zetu hizi za kushadadia siasa sidhani. Chukulia nchi kama NORTH KOREA wanaishi kwa vikwazo chungu mzima lakini bado wanauwezo wa kuendesha project za kurusha vyombo anga za mbali. Kwani wao sio watu??? Wale waliamua kuweka siasa na polojo pembeni wakamchagua kiongozi wao mmoja tu wakaanza safari tizama leo walipo. Japo mtakuja mbio kunikejeli apa kwamba kim jong ni dictator, wale wameamua kutembea kwenye mstari mmoja tu bas yeyote atakaeonesha dariri za usaliti huyo ni mhaini na adhabu yake ni kumtanguliza mbele ya haki msamaha atatoa Mungu kama itampendeza kufanya hivo. Tatizo sisi tunachekeana mno na kuoneana haya kwa staili hii hakuna hatua tutakayopiga miaka nenda rudi.
 
China anakuja kitawala Afrika kwa nguvu zote. Polution ya viwanda vimeshachafua hali ya hewa kwenye miji mikuu yake sasa unatafuta sehemu ya kuhamishia baadhi ya viwanda vyake na kupata mali ghafi kwa bei nafuu au bure. Afrika ndio anakuja kama walivyokuja wazungu ila yeye wanaingia kisanii. Baada ya miaka kadhaa tutalazimika kujifunza kichina kama ilivyo kwa kizungu hivisasa. Lazima atubembeleze kwa kuanzia kuekeza kwake hadi pale tutakapozama ndani ya mahaba ndio hapo!
 
China as China haina ubavu huo, suala la msingi kujiuliza ni nani yupo nyuma. Sasa ukitaka kujua hilo, angalia uchumi wa China unamilikiwa na nani? Utachanganyikiwa zaidi endapo utazijua zile BRIC countries, kwanini zilianzishwa na ni kwa mrengo upi? Katika list mtoe Mrussi tuu nahisi utakaa chini na kulia kabisaaa.
 
Back
Top Bottom