Nchi kuingia gizani - TANESCO sasa hoi kifedha

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 January 2012

TANESCO sasa hoi kifedha


UWEZO wa Shirika la Taifa la Umeme (TANESCO), kukidhi mahitaji ya nishati hiyo ni mdogo na nchi inaweza kuingia gizani wakati wowote, MwanaHALISI limegundua.

Hata nyongeza ya gharama ya umeme kwa walaji, ambayo iliruhusiwa na Wakala wa Usimamizi wa Nishati na Maji (EWURA) wiki iliyopita, "yaweza kuyeyukia kwenye malipo ya makampuni ya kuzalisha umeme," imeelezwa.

Taarifa za wizara ya fedha, wizara ya nishati na madini na TANESCO zinasema, tayari zaidi ya Sh. 544 bilioni zimetokomea katika kipindi cha miezi miwili na kufanya shirika hilo kuomba EWURA kuongeza gharama za umeme kwa mlaji.


Kiasi cha Sh. 136 bilioni ziliingizwa TANESCO kati ya Agosti na Desemba mwaka jana. Fedha hizi zilitoka serikalini, kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini yenye Kumb. Na. CBA.88/560/01/64 ya 30 Desemba 2011.


Barua hiyo inayokwenda kwa Haruna Masebu, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA na iliyosainiwa na E.C. Maswi aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu (sasa ndiye katibu mkuu) inasema, "…fedha hizo siyo mkopo bali mchango wa serikali katika kuondoa mgawo wa umeme na kutekeleza mpango wa dharura wa kuondoa mgawo nchini kwa kipindi cha miezi minne…"


Awali fedha hizo zilikuwa zimetolewa kama mkopo chini ya kile walichoita "Bridging Finance" ili kufidia pengo lililotokana na kuwepo mitambo mingi ya kukodi "kwa gharama kubwa tofauti na mapato yatokanayo na bei ya umeme anayouziwa mteja wa mwisho," inaeleza barua hiyo.


Kiasi kingine cha fedha ambacho tayari kimetokomea katika makampuni ya kufua umeme ni Sh. 408 bilioni ambazo TANESCO ilikopa kutoka mabenki ya nchini, taarifa zimeonyesha.


Mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando alinukuliwa na vyombo vya habari akikiri shirika lake kukopa fedha hizo ili kulipa, pamoja na makampuni mengine, kampuni ya Independent Power Tanzania limited (IPTL) iliyoko Salasala, Tegeta.


"Hata kwa fedha hizo zote, bado TANESCO iko chumba cha mahututi. Tuliomba EWURA waruhusu matumizi ya Sh. 937.4 bilioni kwa ajili ya kugharimia mitambo ya umeme wa dharura lakini walitoa nusu ya maombi yetu," ameeleza ofisa wa shirika hilo.


TANESCO wameruhusiwa kutumia Sh. 473.78 tu kwa ajili ya umeme wa dharura.

Maelezo ambayo yamepatikana EWURA ni kwamba TANESCO wangeruhusiwa kutumia mkiasi chote walichoomba, gharama ya umeme ingekuwa kubwa zaidi ya ile iliyoongezwa.


Nyaraka ambazo MwanaHALISI limeona zinaonyesha makampuni matatu pekee ya kufua umeme nchini – Symbion Group, Aggreko na IPTL yanakomba karibu robo tatu ya mapato ya TANESCO kila mwezi.


"Kama serikali itasimamisha ruzuku kwa TANESCO, shirika hili linaweza kufa mara moja; nchi nzima ikaingia gizani. Huu ndio ukweli wenyewe," kimeeleza chanzo cha gazeti kutoka TANESCO.


Akitangaza gharama mpya ya umeme wiki iliyopita, Masebu alisema hilo lilikuwa zoezi la miezi sita; baada ya hapo wataangalia utaratibu mpya wa bei.


Hivi sasa serikali ina mikataba ya kuzalisha umeme wa dharula na makampuni ya Aggreko, IPTL, Songas, Symbion na Ubungo New Plant ambayo ni ya TANESCO.


Nyaraka zinaonyesha kampuni ya IPTL peke yake inakomba zaidi ya Sh. 18 bilioni kila mwezi kwa ununuzi wa mafuta ya kuendeshea mitambo na matengenezo; na Sh. 102 bilioni ikiwa ni malipo ya kuweka mashine – Capacity Charge – na ununzuzi wa umeme kutoka kampuni hiyo.


Mbali na gharama hizo, serikali imepunguza kodi ya mafuta yanayoingizwa na IPTL kuendeshea mitambo yake. Taarifa zinasema gharama hizo zilipunguzwa kwa Sh. 415 kwa lita ya gesi na Sh. 40 kwa mafuta mazito.


William Ngeleja, waziri wa nishati na madini, yuko kwenye rekodi akiomba Sh. 46.4 bilioni ili kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL kwa kipindi cha miezi mitatu.


Haya yanawekwa wazi katika ombi rasmi alilowasilisha kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri kupitia waraka Na. CAB. 38/88/02 wa Novemba 2010.


"Waheshimiwa mawaziri wanaombwa kutafakari mapendekezo yaliyomo katika aya ya 18 ya waraka huu na kumshauri Mhe. Rais akubali na aagize yatekelezwe ipasavyo," unasema waraka wa Ngeleja.


Aya ya 18 ya waraka inasema zinahitajika Sh. 46.4 bilioni kwa ajili ya mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL.


Kampuni ya Symbion inalipwa kiasi cha Sh. 467.8 bilioni. Mchanganuo unaonyesha TANESCO inailipa kampuni hiyo, kiasi cha dola za Marekani 100,000 (Sh. 152 kila siku) kama malipo ya kuweka mitambo – Capacity Charge.


Kampuni ya Aggreko inalipwa na TANESCO kiasi cha Sh. 175.2 bilioni kwa mwaka. Mitambo ya Ubungo New Plant inagharimu Sh. 30.861 bilioni kwa manunuzi ya umeme na Sh. 7.2 bilioni kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji (Management Contract Costs).


Kampuni ya Songas inalipwa Sh. 35.2 bilioni kwa mwaka kama malipo ya gharama ya kuweka mitambo. Mkataba wake na serikali unairuhusu kampuni hiyo kuuza umeme wake kwa TANESCO hata kama shirika litakuwa na umeme wa uhakika.


Habari zinasema, wakati wa mvua kubwa za masika, ambapo umeme wa TANESCO unatosheleza mahitaji, serikali imeagiza kuzimwa kwa mashine zake ili kuruhusu Songas kuingiza umeme kwenye gridi ya taifa tayari kwa mauzo, jambo ambalo wadau wa nishati wanajengea shaka mantiki yake.


MwanaHALISI limenasa mawasiliano kati ya Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) na uongozi wa EWURA yanayoonyesha kuwa kupanda kwa gharama za umeme kutaathiri, kwa kiwango kikubwa, uchumi wa taifa.


Waraka wa TNBC kwenda kwa EWURA unasema gharama zitaathiri sekta ya viwanda nchini kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji. Gharama za umeme zinachukua asilimia 27 hadi 35 ya gharama ya uzalishaji viwandani nchini.


TNBC inasema kupanda kwa gharama ya umeme kutasababisha wafanyabiashara wakubwa wa viwanda kushindwa kukabiliana na wenzao kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki na nchi zilizoko Kusini mwa Afrika (SADC).


Inaelezwa wateja wakubwa wa TANESCO, ambao huchangia zaidi ya asilimia 60 katika matumizi ya nishati ni sekta ya viwanda.


Kamati iliyoundwa na kamati ya utendaji ya TNBC ilifanya kikao na TANESCO 27 Decemba 2011.



 
Mi ningetaka hata waitoweshe kbs!

Ni juzi tu tulitangaziwa ya kwamba mgao utakuwa historia hapa Nchi ikimaanisha hakuna mgao leo tunaambiwa tunaingia gizani.

Sasa tuna maana gani ya kuwa huru ingali tupo gizani?
Mi naongea toka rohoni ya kwmb serikali legelege kama hii ya kwetu niwa kuwaondoa madarakani kwa nguvu ya UMMA tu.

Sioni haja hata kidogo wizara husika kuwepo hata kidogo.
Na kama huu siyo wizi wa macho kwa macho itakuwa ni nini?
Halafu bado tunasema tunasherekea miaka 50 ya uhuru.

Hii thread inazidi kunichafua nafsi yangu kbs!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom