Nchi Itatawalika kwa Diplomasia, sio mabomu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi Itatawalika kwa Diplomasia, sio mabomu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Feb 7, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Katika siku za karibuni watawala waandamizi pamoja na Mtawala mkuu wa nchi hii wamekuwa wakitoa kauli kuwa kuna kundi la watu ambalo linataka kuifanya tz isitawalike. Watawala hawa wamekuwa wakiapa kuwa kwa namna yeyote hiyo azma hiyo haitatimia na lazima nchi itatawalika.

  Tumeshuhudia siku za karibuni, katika maeneo mbalimbali polisi wakijitahidi kuzima madai ya wananchi kwa kutumia mabomu na risasi. Hivi ni kusema kuwa wanatekeleza viapo vya wakuu wao kuwa nchi itatawalika tu, kwa vyovyote vile.

  Naamini kwa siku za karibuni, serikali itakuwa imeagiza shehena ya mabomu ya machozi (nadhani hayatengenezwi Mzinga haya). Naamini hata idadi ya yale magari yanayomwaga maji ya kuwasha yameongezeka.

  Naomba niwaambie hawa 'wababe' kuwa, hakuna vita iliyowahi kushinda dhidi ya nguvu ya umma kwa kutumia mabavu. Badala ya serikali kutumia raslimali nyingi kupata mabomu, risasi na magari, ni bora watumie raslimali hizo kupata wanadiplomasia watakaowekwa katika nafasi muhimu serikalini.

  Uanadiplomasia ni kipaji, tena wamejaliwa wachache. Kikwete asidhani kuwa kila mtu anaweza kwa wakati huu kuact diplomatically katika nafasi muhimu kama za IGP, waziri wa mambo ya ndani na wengine. Anatakiwa aajiri wanadiplomasia hasa katika nafasi hizi.

  Ni falsafa rahisi tu kuwa ukinirushia bomu la machozi, nitakimbia sio kwa sababu nimekuogopa, bali kwa sababu macho yangu yanawasha. At the end nitakuwa nimeongeza chuki kwako, na muwasho ukiisha, nitarudi tena na kwa nguvu zaidi. JK asijidanganye kuwa kwa mfano kule Arusha sasa watu wanaiogopa na kuitii serikali. Kiukweli watu watakuwa wanaichukia zaidi serikali, na siku wakilipuka tena itakuwa balaa zaidi.

  Kwa sasa serikali inaona kama mzaha vile kudhibiti maandamano kwa mabomu ya machozi. Lakini, kwa uwezo wa askari wetu na nchi yetu, siku ikitokea watu laki moja wanaandamana kwa wakati mmoja, itakuwa ngumu sana kwa mabomu ya machozi kuwadhibiti.

  Na ukweli ni kuwa kwa sasa irritation iliyopo kwa wananchi, ni matter of time tu, kuna siku wataandamana watu milioni moja kwa wakati mmoja. Kwa akili na uwezo finyu wa watawala wetu, watataka kutumia mabomu kuwadhiditi, hapo ndipo watakapoonja joto ya nguvu ya umma wa kweli. Ipo siku, na haipo mbali sana. Kama JK asipojitahidi kutafuta wanadiplomasia watakaowatuliza waTz kwa kutumia akili, then madhara yake atayajutia.
   
Loading...