Nchi Ipo Kwenye "Hali ya Hatari?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi Ipo Kwenye "Hali ya Hatari?"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Nov 24, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  MSIMAMO wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kutoyatambua matokeo ya urais huku kikidai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, umemtikisa Rais Jakaya Kikwete na chama chake, kiasi cha kuanza kuzuiliwa kufanya mikutano yake ya hadhara ya kuelimisha wananchi juu ya misimamo ya chama hicho, Tanzania Daima Jumatano limeelezwa.

  Hatua ya wabunge kususia hotuba ya Rais Kikwete na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wiki iliyopita, imeelezwa kuwatia hofu vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa maslahi ya sasa ya chama chao na serikali yake yatakuwa mashakani ikiwa wananchi watazidi kuelewa manufaa ya hoja hizo za CHADEMA kwa taifa.

  Taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vyetu mbalimbali zimethibitisha kuwapo kwa njama za kuizuia CHADEMA kufanya shughuli kubwa za kisiasa hususan mikutano ya hadhara, huku Jeshi la Polisi likidaiwa kutumiwa kufanikisha mpango huo.

  Mtoa taarifa wetu ndani ya makao makuu ya CHADEMA jana alilithibitishia gazeti hili kuwa tayari chama hicho kimeshazuiwa kufanya mikutano ya hadhara katika mikoa mbalimbali nchini iliyokuwa ihutubiwe na wabunge na viongozi wake wa mikoa.

  Mikoa inayotajwa kuzuiliwa kwa mikutano ya hadhara ni pamoja na Mbeya, Arusha, Mara, Manyara, Iringa na Mwanza ambayo wabunge wa chama hicho kupitia viongozi wa mikoa, waliomba vibali toka polisi kuruhusu kufanyika kwa mikutano hiyo.

  “Kuna mkakati umeanza na kutekelezwa na Jeshi la Polisi kwa kutumiwa na CCM kuidhibiti CHADEMA isikutane na wananchi, sababu ni hofu. Wanahofia wananchi watazidi kuelewa madai ya chama, watazidi kuyaunga mkono na kuwa madai ya kitaifa.

  “Wabunge wetu kwa kushirikiana na viongozi wa mikoa walipanga kufanya mikutano hiyo ambayo pia ililenga kuwashukuru wananchi kwa kutuunga mkono…Iringa mjini wamezuiwa…Arusha mjini, Musoma, Mbeya, Mwanza na kule Manyara, kote kulikoombwa vibali Jeshi la Polisi limekataa kuruhusu mikutano hiyo.

  “Lakini sababu wanayotoa wao ni kwamba hali ya usalama nchi nzima ni tete hasa baada ya chama hicho kutoa msimamo wa kutotambua matokeo ya urais na kwamba bado serikali haijaundwa, hivyo hawawezi kuruhusu uvunjifu wa amani,” alisema mtoa taarifa huyo.

  Gazeti hili lilipojaribu kuwasiliana na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuhusiana na chama chake kuzuiliwa kufanya mikutano ya hadhara, simu yake iliita mara nyingi bila kupokelewa.

  Jitihada za kumtafuta katibu mkuu wake, Dk. Willbrod Slaa, pia zilikwama baada ya kujibiwa na mmoja wa maofisa wa makao makuu ya chama hicho kuwa alikuwa kwenye kikao kirefu.

  Hata hivyo, hatua ya Jeshi la Polisi kuizuia CHADEMA kufanya mikutano ya hadhara kwa madai ya kuwapo hali mbaya ya usalama nchini, inaonekana kutokuwa na mashiko hasa ikizingatiwa kuwa rais hajatangaza hali ya hatari.

  Mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa na utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipoombwa kutoa ufafanuzi wake juu ya hatua hiyo ya Jeshi la Polisi alisema:

  “Kama wamezuia mikutano kwa sababu hiyo basi wamewaonea, rais hajatangaza hali mbaya ya usalama kama linavyodai jeshi hilo. Ni lazima hali hiyo itangazwe na mkuu wa nchi kwa mujibu wa Katiba…vyama vya siasa vina haki ya kufanya siasa, kukutana na wananchi na kunadi sera zao. Huwezi kuibana haki hii kwa kisingizio cha uvunjifu wa amani ambao haujulikani,” alisema msomi huyo huku akihofia kutajwa jina lake.

  Kwa mujibu wa Ibara ya 32 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, rais anaelekezwa kutangaza hali ya hatari kwa kutuma nakala ya tangazo lake kwa Spika wa Bunge ambaye baada ya kushauriana na kiongozi wa shughuli za Bunge ataitisha kikao cha Bunge kujadili hali hiyo kabla ya kuiidhinisha.

  Ibara hiyo inasema, “Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania Bara nzima au Tanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara moja nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano wa Bunge, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali ya mambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais.”

  Aidha, ibara hiyo imefafanua kuwa rais anaweza kutangaza hali ya hatari ikiwa nchi iko katika vita, inakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita au kuna hali halisi ya kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani na usalama.

  Kiongozi mmoja wa makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa sharti la kutotajwa jina lake aliliambia gazeti hili kuwa sababu ya kuwapo ‘hali tete ya usalama’ nchini iliyotolewa na jeshi hilo si ya kweli kwani hali hiyo inapaswa kutangazwa na kuidhinishwa rasmi.

  Hatua ya CCM kuzuia maandamano yaliyoandaliwa na uongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, inadaiwa kuwa ni maandalizi ya kuhalalisha Jeshi la Polisi kuzuia mikutano hiyo ya CHADEMA.


  Source: Tanzania Daima.
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kila jambo lina mwanzo na mwisho wake

  e mungu bariki viongozi wa chadema ili yale mema wanaotaka yatendeke ktk hii nchi yatimie

  mapinduziiiii daimaaaaaa
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ni kuandamana kwa nguvu tu wacha tupigwe virungu lakini meseji ifike
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lakini JK alitahadhalisha majeshi yetu siku ya kuapishwa kwake, hivyo yawezekana walitegema haya kutokea..

  Mimi nadhani Chadema wanatakiwa ku slow down na kujaribu njia za mapatano ili kuondoa mgogoro huu ikiwa maswala yote yanahusiana na katiba. Kama CCM wamesema hawatakubali kubadilisha Katiba hapo ndipo Chadema wanaweza kuwapelekea kesi yao wananchi lakini kwa sasa hivi wajaribu zaidi suluhu itakayopelekea uwezekano wa kuundwa katiba mpya kwani yapo maswala mengi sana yanayotakiwa kuwekwa sawa kitaifa ikiwa ni pamoja na nafasi ya Zanzibar ktk serikali ya Muungano kwani hivi sasa mkorogano umetupoteza kabisa. katiba ni lazima iandikwe upya na sidhani kama CCM wataendelea kupinga kwani maji haya ni marefu kiasi kwamba JK atataka kuchukua sifa ya kuliwezesha...
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  CHADEMA itangazie wananchi kwamba polisi inawazuia kuongea na wananchi then wananchi wenyewe ndio wataamua.
   
 6. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Lazima tudai haki yetu ya kupandikiza vibaraka na kuweka pembeni matokeo halisi ya kura.

  CHADEMA TUTAKOSANA IKIWA HAMTATEKELEZA AZMA YA KUDAI MAANDAMANO KUUAMBIA UMMA KUWA WALITANGAZWA WASIO WASHINDI NA KUACHA WASHINDI PEMBENI.

  TUNAUMIA KURA ZETU ZIMEHUJUMIWA, TUNATAKA WALIO HUSIKA WACHUKULIWE HATUA MARA MOJA.
   
Loading...