Nchi inapotawaliwa kisanii nini matokeo yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi inapotawaliwa kisanii nini matokeo yake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by King Suleiman, Feb 23, 2011.

 1. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Hallow JF,
  mwanasayansi Isack Newton aliwahi kutamka "politicians they just talk they dont write or practice" Je, viongozi wetu wa serikali ya Tz nao wapo katika mkumbo huu au wao wana practice?

  kwa hakika ni usanii mtupu unaotokea kwa uongozi wa nchi, waziri anaweza kutamka tofauti na raisi wake na hakuna uwajibikaji , katibu mkuu nae anaweza kutoa muongozo vilevile just kuridhisha watu fulani. Mifano ni mingi na karibu wote tunajua.

  sasa najiuliza hivi nchi inapotawaliwa kisanii na wakuu wetu hawajui hata vyanzo vya matatizo yanayowakabili wananchi, nini matokeo yake??

  je tutaendelea kukandamizwa na kuwa wajinga?
  Siku moja tutazinduka??
  Je usanii utaendelea daima na kurubuni wananchi kwa vizawadi vya msimu? Au
  ni mapinduzi ya fikra yanaweza kuibuka na kuibua mapinduzi halisi?? Sijui yetu sie macho...
   
 2. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Angalia isu za Dowans, matukio ya Arusha na skendo nyingine nyingi utaona jinsi wakuu wanavyojikanyaga na kila kiongozi atatoa yake. Wakijichanganya utasikia ooh "hayo ni maoni binafsi..." kweli nchi hii ina usanii mwingi serikalini hata ktk mambo ya msingi.
   
 3. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Si rahisi kukombolewa katika mazingira haya. Walipoona sisi walalahoi tunaanza kusomesha watoto wetu ili waje wakatae kutawaliwa na wao wakaamua kuleta shule za kata ili watoto wetu wawe wanapata maziro na kuishia kidato cha nne. Na sasa wamemuweka waziri asiye nauwezo kusimamia elimu... Jamani tuoneeni huruma watanzania
   
 4. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Matokeo yake ni ya usahiii mtupu,hakuna tija.Swali siku 110 tangu jamaa yupo madarakani nini kimefanyika ?.matokeo watu kufa,kujiua,mabomu
  risasi ndo vinasikikia kila kukicha.
   
 5. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ndio hapo K' tunapoulizana huu usanii utaendelea mpaka lini? Au ndio utaratibu tuliojiwekea wa kukaa utumwani siku zote?? Ni hatari kwa kweli usanii huu unaliponza taifa letu.
   
 6. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ni kweli mzee wa Rubisi haya ndio matokeo ya usanii. Wkt wa kampeni aliahidi ahadi za mamilioni lakini leo tunashuhudia hakuna hata ahadi moja iliyotekelezwa au hata inayoanza kutekelezwa. Sasa je watanzania tunapenda kudanganywa ili watawala wajinufaishe??
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Halafu kuna wizara inaitwa ya UTAWALA BORA...LOLZ!
  Nadhani watakuwa wanashinda wanasoma magazeti ofisini hawa!
   
 8. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  hahaha! PJ ndio serikali yetu hiyo, utawala bora au bora utawala? Kwa hakika kila maeneo wanaleta usanii. Kama wewe sio msanii basi haufit kwenye serikali ya bosi JK
   
Loading...