Nchi inaliwa na Viongozi Ranchi ya Usangu, masikini Tanganyika

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Rais Wasaidizi wako wanakuangusha Tanganyika imegeuzwa shamba la bibi au kichwa cha mwendawazimu kila anayejifunza kunyoa anaenda kwenye Ranchi ya Usangu.

Kazi yetu kukuhabarisha, hatua stahiki utazichukua wewe.

millardayo_1673843955779470.jpg



===
Ranchi ya Usangu yageuzwa Shamba la Bibi

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa na kikao kazi na wadau wote muhimu wa uhifadhi na utunzaji vyanzo vya maji, leo Januari 16, 2022 huku agenda kubwa ikitajwa ni kunusuru uhitadhi wa Bonde la Usangu na Hifadhi ya Taifa Ruaha maeneo ambayo yapo katika hali mbaya kutokana na kuharibiwa na shughuli za binadamu ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi.

Taarifa zinaeleza Waziri Mkuu atakuwa Mbeya kwa siku mbili (Januari 16 na 17, 2023) ambapo pia atatembelea eneo la Mbarali kuona hali ya uharibifu.

Wakati Waziri Mkuu Majaliwa anakwenda Mbeya, taarifa zaidi zinasema eneo la Ranchi ya Usangu ambayo ni sehemu muhimu ya ardhi oevu ya Bonde ya Usangu limegawanywa kama njugu na Vigogo kadhaa na kubadilishwa matumizi yake.

Eneo hilo lenye mito muhimu kwa ajili ya maji yanayotiririka kwenda Mto Ruaha Mkuu, mito hiyo ni pamoja na Mto Mkojo, Mlowo na Mapala limeharibiwa na wengi wa wawekezaji waliomilikishwa na vitalu katika eneo hilo.

Wawekezaji hao wamekuwa wakitumia eneo kwa kilimo cha umwagiliaji huku wakichepusha maji kutoka katika mito hiyo bila ya kupata vibali na kufanya malipo ya maji kwa mamlaka ya Bonde la Rufiji.

Aidha, tofauti na sheria inavyotaka wawekezaji hao wanafanya shughuli za kilimo na wakulima wadogowadogo ambao wanakodishiwa maeneo ya wakulima na wawekezaji waliopewa vitalu.

Pia, wawekezaji wa eneo hilo wamekuwa wakiwakaribisha na kuwakodishia maeneo ya kuchungia mifugo katika eneo hilo huku wakikusanya fedha ambazo hata hakuna makusanyo ya kodi za Serikali.

Kutokana na mifugo mingi eneo hilo wakati wa kiangazi, uharibifu wa uoto wa asili na vyanzo vya maji umekuwa mkubwa.

Katika hali isiyoeleweka eneo hilo muhimu kwa uhifadhi wa vyanzo vya maji ambalo mwaka 2008 lilijumuishwa kwenye mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kupitia GN28 limeondolewa nje ya mipaka ya hifadhi na kusababisha mshangao mkubwa kwa wengi.

Hiyo ni kwa kuwa eneo la ranchi ambalo linamilikiwa na watu wachache liliondolewa ndani ya hifadhi huku maeneo makubwa yenye Wananchi wengi yakiondolewa kutoka katika mipaka ya Hifadhi ya Ruaha.

Chanzo: Jamvi la Habari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom