Nchi inakwenda wapi, muda si mrefu bomu litaripuka

Nchi inakwenda wapi, muda si mrefu bomu litaripuka

UFASHE MLIBHONA

Senior Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
177
Reaction score
51
Nimetafakari sana naona giza mbele. Haya maendeleo hayatupeleki tunakotaka kwenda. Sina uhakika kama viongozi wetu wanawaza na kutafakari sababu za yanayotokea sasa. Hebu tupitie kidogo:

1.Zamani watumishi wa Umma kama walimu, askari, waganga na wengine wengi walikuwa wanaheshimika sana katika jamii. Leo hii hawathaminiwi tena , wanaonekana ni vibaka, wezi, wala rushwa maskini malofa.

Sasa hivi sio ajabu kukuta askari amevamiwa anapigwa na raia, Wananchi kuvamia vituo vya polisi kuvichoma moto, kuua askari sio ajabu tena. Nchi yetu inakwenda wapi?

2.Kuzuka kwa vikundi mbalimbali na majina tofautitofauti mfano Panya road, mbwa mwitu,tukale wapi-polisi,mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, al-shabab-Tanzania vinavyofanya matukio ya kihalifu.

3.Vijana waliomaliza JKT kutaka kuandamana kwenda ikulu. Mambo ya ajabu kabisa!!!.Askari akiandamana maana yake ni mapinduzi(coup) Nilitegemea vijana kama hawa wawe wamefundishwa stadi za kazi,kujitegemea, ujasiriamali na uzalendo kwa nchi yao na si kutegemea ajira serikalini baada ya kuhitimu mafunzo yao.

Pengine iko haja ya serikali kupitia mtaala wa mafunzo ya JKT upya. Inaonekana mafunzo ya sasa ni ya kizazi kipya(dot.com).Tuangalie tusijiandalie wenyewe waasi wa siku za mbeleni.

4.Nafasi mbalimbali za kazi kutolewa kwa msingi wa kabila au dini ya mtu: Sasa ndio imekuwa utaratibu mfano Mkuu wa Mkoa akiwa wa kabila fulani ,basi anataka na wakuu wa wilaya wawe kabila lake, wakuu wa idara wote wawe kabila lake. Sasa si ajabu tena kukuta ofisi fulani watendajizaidi ya robotatu wakatokea dini moja aau kabila moja.

Tumemsahau Nyerere aliyehakikishaa tunachanganyika na kusahau dini na kabila zetu. Leo hii ukifika ofisi yoyote swali la kwanza utaulizwa unatokea mkoa gani-MAAJABU.

5.Ufisadi ndio umekuwa utaratibu wa kuendesha nchi. Kila kiongozi serikalini ni fisadi wa namna moja au nyingine Usipokuwa fisadi hufai kuwa kiongozi. ufisadi sasa ni sifa ya kuwa kiongozi.

6.Rushwa kuwa sehemu ya maisha ya Mtanzania. Ofisi zote iwe ya serikali,NGO,binafsi rushwa ndio msingi wa mafanikio yako. Bila rushwa hakuna huduma labda na wewe uwe ni sehemu ya mtandao huo.

7 Wabunge(Zamani walikuwa wawakilishi wa wananchi) kudai na kulipwa malipo/fedha pasipo kuangaalia hali na vipaumbele vya nchi. Kipato cha mwananchi wa kawaida Shs 600,000/= kwa mwaka. mwalimu/daktari Shs 186.271/= kwa mwezi baada ya makato mbalimbali, mbunge zaidi ya shs 300,000/=kwa siku. Sidhani kama bado mbunge anamwakilisha mwananchi.

washauri wa viongozi wetu waelezeni hali halisi msiwape sifa na kuwadanganya, hali huku kwetu si shwari. someni alama za nyakati
 
Tz;imekuwa ukoo Wa panya baba mwiz mama mwiz watoto wez!!!;afu wakatafta kajina kazuri sana wakajiita FISADI;!!! Baada ya neno mwiz.kazi ipo
 
Back
Top Bottom