Nchi inajengwa na maisha yanaguswa

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Tangu serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan iingie madarakani wengi walikuwa na hofu kuhusu miradi ya kimkakati. Sasa nakufahamisha Mama kaupiga mwingi sana.

Serikali anayoiongoza Rais Samia imeendelea kumwaga fedha kwa ajili ya miradi mikubwa. Ukichukua gharama za miradi mikubwa ya SGR na mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP inayoendelea kwa sasa yaani SGR Isaka -Mwanza kilometa 341 kwa shilingi trilioni 3.02, Makutupora-Morogoro kilometa 422 kwa shilingi trilioni 4.4, Dar -Morogoro kilometa 300 kwa shilingi trilioni 2.7, Makutopora-Tabora kilomita 371 kwa shilingi trilioni 4.606 na mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP shilingi trilioni 6.55 inakua Jumla yake ni shilingi trilioni 21.206

Anastahili pongezi Rais Samia Suluhu Hassan kwani pamoja na nchi kupitia changamoto za uviko-19, ukame na mitikisiko wa uchumi wa dunia lakini bado hakuna mradi uliosimama. Hakika Mama anaupiga mwingi.

Serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuleta vicheko, tabasamu na furaha kwa makundi mbalimbali kuanzia waandishi wa habari, vyama vya siasa, wafanyabishara, wawekezaji, NGOs, watumishi wa umma, wanafunzi elimu ya juu, bodaboda na machinga.

Katika kuendelea kujenga taifa lenye umoja, mshikamano, amani na utulivu serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea na vikao na mikutano mbalimbali kupitia baraza la vyama vya siasa na kituo cha demokrasia nchini ili kujenga maridhiano na kuimarisha mazingira ya ufanyaji siasa nchini. Kwa hili Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha ukomavu, uvumilivu na ustahimilivu akionesha Tanzania ni yetu sote tushirikiane kuijenga. Anastahili kuungwa mkono kwa uamuzi wa busara wenye maslahi mapana na Nchi yetu.

Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mpaka serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inaingia madarakani zaidi ya wanafunzi elfu 11 walikosa mikopo katika mwaka wa fedha 2020/21. Baada ya kuingia imeongeza shilingi bilioni 106 sawa na asilimia 23 yaani kutoka shilingi bilioni 464 mwaka wa fedha 2020/21 hadi shilingi bilioni 570 mwaka wa fedha 2021/22 na kuongeza idadi ya wanafunzi wenye sifa kunufaika zaidi na mikopo hivyo kuweza kujiunga na kuendelea na masomo ya chuo kikuu.

Serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imefuta kabisa ada ya asilimia 6 ya kulinda thamani ya mkopo (Value Retention Fee) kwa wanufaika wa mkopo elimu ya juu nchini kuanzia mwaka wa fedha 2021/22. Kwa lugha rahisi tunasema ameongeza kiasi hicho kwenye kiwango cha mshahara anachobaki nacho mtumishi aliyekuwa mnufaika na kutakiwa kukatwa ili kufanya marejesho.

Kwa upande wa watumishi wa umma sote tunafahamu kwa miaka mitano mfululizo tumeshuhudia watumishi wa umma hawajapandishwa vyeo/madaraja. Baada ya kuingia madarakani ndani ya muda mfupi tu ameshatoa shilingi bilioni 509, kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 yaani shilingi bilioni 449 za madaraja/vyeo na shilingi bilioni 60 za malimbikizo ya mishahara na tayari Pesa hizi zimeshalipwa kwa wahusika na kurejesha furaha miongoni mwao.

Rais Samia amepunguza kodi ya PAYE toka asilimia 9 kwa mwaka wa fedha 2020/21 mpaka asilimia 8 kwa mwaka wa fedha 2021/22. Hii inamaanisha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza hii asilimia moja kwenye makato ya mishahara yao, basi amefanya nyongeza kwenye mishahara ya watumishi wa umma.

Kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu wenye sifa za kuajirika wamesubiri mtaani kwa kipindi cha takribani miaka mitano. Ajira serikalini kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka wa fedha 2015/16 wakati huo Rais alikuwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipoachilia ajira mpya elfu 52 trh 01/05/2015. Leo tunashuhudia tena Rais Samia Suluhu Hassan akiachilia ajira mpya za Serikali elfu 40 kwa mwaka wa fedha 2021/22 kwa gharama ya shilingi bilioni 239 na shilingi bilioni 120 kwa ajili ya kubadili muundo wa Utumishi.

Maajabu zaidi ya serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uwekezaji imeendelea kufanya vizuri ambapo tayari miradi mipya mikubwa 93 imeshasajiliwa yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.6 takribani shilingi trilioni 3.23 ambayo inakadiriwa itaajiri watu 23,600.

Katika mwaka wa fedha 2021/22 serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeshatoa shilingi bilioni 132 sawa na shilingi milioni 500 katika kila Jimbo kwa majimbo yote 264 kama fedha za maendeleo ya miundombinu ya barabara.

Aidha serikali inayoongozwa na Rais Samia imetoa shilingi bilioni 322.158 kama bajeti ya nyongeza kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa Vyumba 10,000 vya madarasa, Zahanati 555 na Vituo vya afya 211.

Serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeongeza bajeti ya TARURA kwa asilimia 254 yaani kutoka shilingi bilioni 273 kwa mwaka wa fedha 2020/21 hadi shilingi bilioni 966.43 kwa mwaka wa fedha 2021/22 ili kuhakikisha barabara za vijijini na mijini zinajengwa na kukarabatiwa ili zipitike wakati wote.

Serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ilitangaza hadharani kuwa haihitaji kodi za dhulma bali za haki zinazokusanywa kwa weledi bila ubabe na mabavu. Rais Samia amesisitiza kutaka TRA kujenga mazingira mazuri na rafiki kwa wafanyabishara nchini kwa kuonana marafiki ili kuwa chachu kwa ukuaji wa biashara, kujenga hamasa ya ulipaji kodi kwa hiari na mapato zaidi kwa serikali.

Upande wa vyombo vya habari tangu serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan iingie madarakani tumeshuhudia uhuru wa habari ukilindwa, magazeti na televisheni za mtandaoni zikifunguliwa na kutakiwa kuendelea na kazi kwa kufuata na kuheshimu sheria na miiko ya taaluma ya uandishi wa habari. Aidha, amepunguza viwango vya usajili wa televisheni za mtandaoni kutoka shilingi 500,000-1,000,000 hadi shilingi 50,000-200,000 kwa miaka mitatu.

Tumeendelea kusikia katika dhamira ile ile ya kuliimarisha shirika letu la ndege (ATCL) kwa lengo la kuimarisha na kukuza biashara, utalii na uwekezaji nchini serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeagiza ndege tano ambapo ndege nne ni za abiria na moja ya mizigo huku tayari shilingi bilioni 560 zimeshalipwa.

Maajabu mengine ya serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni uwazi katika mikopo ambayo serikali au Nchi inachukua toka taasisi za fedha duniani. Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia Rais wa nchi yetu akitoka hadharani kueleza tumekopa na kutoa mchanganuo wa namna mkopo huo utakavyotumika pamoja na kutoa mrejesho wa utekelezaji.

Kwa hakika kazi kubwa imefanyika tutaendelea kukuletea mafanikio ya serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kila Jpili....

KAZI IENDELEE

%2B255%20738%20969%20820%2020220226_093149.jpg
 
ID yako inakataa bandiko lako...huyo unayemuimbia hilo pambio, wenzako wanasema sio WA WANYONGE. Au ndo katika kudumisha mila za misioga?
 
Sema nchi inatafunwa kwa kasi ya ajabu na genge la msoga baada ya genge la kisukuma kuwekwa pembeni.
Mchwa wa kijani hawanaga huruma wala kutosheka, wanatafuna kwa kwenda mbele tu.
 
Anastahili pongezi
 
Back
Top Bottom