Nchi hii wanasiasa wote ni WATAKATIFU

pocha2

JF-Expert Member
Sep 23, 2014
890
396
Wakuu mimi kwa maoni yangu naona nchi hii watu wenye dhambi au makosa ya kiutendaji, wizi na ufisadi ni watumishi wa Umma tuu. Ukiangalia kwa makini jinsi hatua mbali mbali za kudhibiti UFISADI au UZEMBE zinazochukukiwa na serikali yetu,, utabaini kuwa hakuna mwanasiasa yeyote ambaye kachukuliwa hatua, hata kama wana kashfa za wizi, wa mabillion au walifanya maamuzi kwa UZEMBE. Bungeni karibu wote wamepata vyeo,, waliofungwa wameachiwa na wengine sasa ni mawaziri. Mahakamani pia naona kuko mswanu kabisa. Hii si vita halisi,, watumishi mjipange.
 
Kuwa mtumishi wa umma nchi hii ni zaidi ya utumwa
kusafiri nje ya nchi hata kwa pesa yako uombe kibali Ikulu
hata kina Kingwendu na masanja wana uhuru wa kusafiri kuliko mtumishi wa umma
bado kufungiwa geti na waziri
bado kumsikia Rais akikutangazia vita kama vile wafanyakazi wa ATCL
bado unyonywe pesa za kila mwezi na vyama vinavyotakiwa kukutetea huku viko kimyaa unanyanyasika
 
Wanasiasa wanawaonea watendaji, wao hakuna aliyewajibishwa hata mmoja tatizo liko kwa watendaji, lkin ngoja wakome sababu wao ndo wameplay role kubwa sana kuwaweka wanasiasa madarakani kupitia polisi, usalama wa taifa, wakurugenzi wa mawilaya, kwa vile cha moto wanakiona, inawezekana kabisa chaguzi zijazo wakatenda haki, hivyo kutufanya sis wananchi wa kawaida kupata kinachostahili. Sababu ukiona maslah ya watendaji yamezuiliwa huku wakitakiwa kufanya kazi sana ni dhahir hiyo serikali haina mda mrefu itang'oka tu sababu hakuna wazee wa figisu figisu kama watendaji, time will tell. Kuna watu saiv makazin ni bora liende na hujuma tu, nayajua haya kwa kuwa kabla cjaachana na utumwa wa TGS niliyashuhudia.
 
Kuwa mtumishi wa umma nchi hii ni zaidi ya utumwa
kusafiri nje ya nchi hata kwa pesa yako uombe kibali Ikulu
hata kina Kingwendu na masanja wana uhuru wa kusafiri kuliko mtumishi wa umma
bado kufungiwa geti na waziri
bado kumsikia Rais akikutangazia vita kama vile wafanyakazi wa ATCL
bado unyonywe pesa za kila mwezi na vyama vinavyotakiwa kukutetea huku viko kimyaa unanyanyasika

Poetry should be written to poets!! Do we really have any here?
 
Back
Top Bottom