Nchi hii tulipata bahati mbaya

CCM hawakuwahi kujua kama Rais huwa anaweza kufa madarakani.
 
Na nyie wafuasi wa Magufuli, kila kitu mnataka kutuaminisha Magufuli alikuwa na akili sana na mzalendo sana. Kiongozi mzuri haharibu mifumo ya utawala bora na yeye kujigeuza Mungu mtu.
Aliharibu mfumo gani?
 
Ile International airport ya Chato imeanza kupokea ndege ipi ?? au thomassankara airlines ??
 
Nasisitiza Magufuli alikua anazingatia sana katiba na sheria. Wasiopenda haki hawakumpenda kwa wao kutaka kutumia sheria kuepa haki au kufanya biashara ya kuuza haki kupitia sheria.
Magufuli akizingatia sana katiba na sheria na ndio akaiba uchaguzi na akamweka kibaraka wake Mwinyi kuwa Raisi huku Zanzibar baada ya kuuwa watu na kuwajeruhi wengine kupata ulemavu wa maisha
 
Nasisitiza Magufuli alikua anazingatia sana katiba na sheria. Wasiopenda haki hawakumpenda kwa wao kutaka kutumia sheria kuepa haki au kufanya biashara ya kuuza haki kupitia sheria.
Kama anazingatia sheria, pesa alizopora kwenye bureau de change alizipeleka wapi? Vitambulisho vya wamachinga vilikuwa vinatolewa kwa shilingi 20,000, zile pesa zilikusanywa kwa sheria gani na ziliingizwa kwenye mfuko gani. Ni wajibu rais kuisimamia pesa za umma na kupeleka maendelea nchi nzima bila upendeleo maana pesa sio zake. Je alipokuwa anapita na kusema walipochagua wapinzani hapeleki maendeleo alikuwa anatumia sheria na katiba gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…