fj_dom
Member
- Jan 29, 2017
- 22
- 13
Kwa kweli kuna mambo yanayonishangaza sana! Nikikumbuka kipindi cha kampeni 2015 hali ilivyokuwa kwa wagombea, walivyohangaika kuomba kura na kuzunguka kwa wananchi kadiri walivyoweza na hatimaye kufanikiwa kupata ubunge, leo hii mtu huyo anasombwa ghafla tu as if ni jambazi au mtuhumiwa wa mauaji.
Mbunge ni mtu mwenye heshima na hadhi mbele ya jamii, lakini anavyodhalilishwa na polisi kwa kubebwa tu. Mimi nadhani hivi vyeo vya ubunge vya kuteuliwa ifike mahali waviondoe kwenye katiba, maana mtu hajui hustle ya kugombea ubunge, yeye anapewa tu alafu tena anapewa na wadhifa wa juu wa kulisimamia bunge then ananyima uhuru wa wabunge kuzungumza mawazo yao na wakijaribu kumwelesha wanaamriwa watoke nje.
Au kinga ya wabunge wa upinzani imefutwa? Yaani bunge ndio ilikuwa sehemu ya debate hasa ya maswala nyeti yanayohusu nchi hii maana mishahara yao ni kodi zetu lakini cha ajabu mambo yanaminya, uhuru hamna, ilikuwa live sasa hatujui nini kinaendelea zaidi ya kupewa habari juu juu.
Bila katiba mpya, nchi hii kupata maendeleo stahiki ni vigumu mno maana unapomyima mtu uhuru hata wa kujieleza tu, sijui atapata wapi hamasa ya kufanya shughuli za maendeleo maana duniani kila mtu aliumbwa tofauti na mawazo ya mtu mmoja hayawezi kuwa sahihi kwa watu milioni 50.
Kwakweli tunapoelekea uchaguzi wa 2020, katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ndio viwe mambo ya msingi ya kudai ili twende kupiga kura tukiwa tunajua haki itatendeka katika huo uchaguzi.