akili ndogo we mda wote unawaza uchonganishi wa dini tu ??
Hivhi uchanganishi uko wapi, jisomee;
Chama tawala nchini Ujerumani,
Christian Democratic Union (CDU), ambacho ni chama rafiki na Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kimesema kitawapa nafasi za mafunzo nchini humo vijana viongozi wa
Chadema, kusomea maadili na uongozi.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema hayo mwishoni mwa wiki baada ya mazungumzo ya faragha yaliyomshirikisha pia Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa na viongozi wengine wa juu, na ujumbe wa CDU, uliokuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa Ujerumani, Profesa Dk. Horst Kohler.
Alisema katika mazungumzo yao, Kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa Chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao.
"Tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa Chadema kwenda kusomea uongozi na maadili nchini Ujerumani," alisema.
Chanzo:
Vijana wa Chadema kupewa mafunzo Ujerumani - Jukwaa la Wananchi
Cha kushangaza, hawa CDU waliiona kuwa chadema haina maadili ndiyo wakawapa ofa ya kuwafunda maadili, badala ya chadema kupeleka Mwenyekiti na Katibu Mkuu wao kundwa maadili wao wanapeleka vijana, makubwa haya.