NCCR Mageuzi yamfukuza uanachama Kafulila na wenzake!

Je NCCR wanaweza kushinda tena jimbo la David Kafulila? Naamini aliyeshinda huo uchaguzi alikuwa ni yeye David, sasa je kwa hayo maamuzi watakuwa NCCR wamepoteza?
Nawasilisha.
 
Zitto nae alipeleka maaskari kwenye kikao cha NCCR yeye kama nani? Jamani hizi siasa zimekaa vipi Tanzania hii. Upinzani bado upo poor kabisa wanajilazimisha tuu. Na tukiwapa upenyo kuongoza nchi mambo yatakuwa shaghalabagala kwa muda mfupi sana.
 
Ndugu kafulila, mimi nitakuombea msamaha kwa Chadema. Ila ukirudi tena Chadema koma kabisa na hizo bla bla zako.Vinginevyo nenda chama cha magamba ili uzomewe na wapiga kura wako.
 
Hatujawa na wagombea binafsi hapa iliyoshinda ni NCCR. Agombee yeye kama Kafulila sasa kama Tendwa anamfahamu kwenye daftari la vyama
 
Hiyo ni ajali ya kisiasa bwana Kafulila isikunyime usingizi. Sasa jipange kurudi nyumbani kwenu CHADEMA Maana NCCR ulikuwa kama uko uhamishoni.

Na upande wa CHADEMA nawaombeni mmpokee kafulila atakuwa ameshajirekebisha.

KAFULILA NI JEMBE.

The past is over.
 
Ndugu kafulila, mimi nitakuombea msamaha kwa Chadema. Ila ukirudi tena Chadema koma kabisa na hizo bla bla zako.Vinginevyo nenda chama cha magamba ili uzomewe na wapiga kura wako.

Hiyo ni ajari ya kisiasa bwana kafurila isikunyime usingizi.Sasa jipange kurudi nyumbani kwenu CHADEMA Maana NCCR ulikuwa kama uko uhamishoni.Na upande wa chadema nawaombeni mmpokee kafulila atakuwa ameshajirekebisha.KAFULILA NI JEMBE.The past is over.
Kuna thread ya kumwombea msamaha twendeni tuchangie huko labda viongozi wa CDM watasikia kilio chetu.
 
Ndugu kafulila, mimi nitakuombea msamaha kwa Chadema. Ila ukirudi tena Chadema koma kabisa na hizo bla bla zako.Vinginevyo nenda chama cha magamba ili uzomewe na wapiga kura wako.

Kama Chadema ni chama makini, tuone kama watampokea tena Kafulila.
 
Nchi yetu hatuna utaratibu wa mgombea binafsi lakini kiukweli aliyeshinda uchaguzi 2010 alikuwa KAFULILA na si NCCR kama wengi wanavyodhania.Kwa hiyo NCCR hilo jimbo wamepoteza Completly.
 
Kafulila hakufukuzwa CDM, alihama mwenyewe. Kwani Tambwe Hizza akitaka kurudi CUF ni lazima aombe au aombewe msamaha?
 
Hapa tunajaribu kuchambua ukweli wa siasa zetu kwa kipndi hiki, haswa ambayo yamechukuliwa na upinzani.

Pamoja na kuwa inawezekana chama kikawa tiketi, lakini nadhani wananchi a.k.a wapiga kura wanakuwa na imani zaidi na mbunge wao kuliko chama.

Mfano ni John Shibuda, pamoja na ukorofi wake, ila CDM wanabusara hawana papara kwa sababu wanafahamu umuhimu wa kuwa na watu wenye challange ndani ya chama.
 
Kafulila amewahi kunieleza mambo mengi sana yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chadema baada ya yeye kujitoa mhanga kumuunga mkono zitto alipotangaza kumpima ubavu Mbowe kwenye uchaguzi wa ndani wa cdm, aliniambia mengi sana mpaka jinsi alivyoongea kwa masaa mengi sana na zitto akiwa "nyumbani kwake" ujerumani kumsihi asijitoe kugombea kwa kuwa akijitoa watakaoumia ni wao kwa kuwa yeye zitto tayari alikua na muscles za kisiasa za kutosha kuliko wao,

Lakini zitto akasisitiza asiwe na wasiwasi yeye atamlinda! lakini yeye kafulila akamwambia zitto kwamba yeye amefanya kazi na Mbowe muda mrefu hivyo anajua style yake ya kushughulikia watu wanaompinga na kwamba anajua baada ya uchaguzi yeye ndio atakuwa wa kwanza kushughulikiwa na Mbowe kwa kuwa ndio alikua mstari wa mbele kumsupport zitto, lakini zitto hakumsikiliza akajiondoa! baada ya hapo kafulila anasema kazi ikaanza na aliyotabiri kwa zitto yakatimia kwa yeye kukimbia chama kabla ya kufukuzwa kwa kuwa kwa jinsi alivyomfahamu Mbowe anasema alijua anaanda umafia wa mkumfukuza ili kummaliza kisiasa, yeye ndio akaona bora kutangaza kukihama chama unakua na heshima kuliko kuondoka kwa kukufukuzwa.

Sasa natamani kumuuliza kafulila safari hakuogopa kufukuzwa wakati alishaona dalili maepema kupitia kauli za sam ruhuza dhidi yake? na je kwa kufukuzwa namna hii haoni kwamba imemuharibia sana malengo yake ya kisiasa huko mbele?
 
Huku Kafulila Kule Hamad Rashid...........viongozi wa timu ya kambi ya upizani Bungeni.............inauma, inaonya, inasikitisha, inasisimua, inasimanzisha, inahurumisha, inatatanisha, inagonganisha, inakatisha tamaa, inagharamisha (uchaguzi tena) inatafakarisha, inadidimiza, inaangalizo, inanogesha, inalipiza, inadidket, inaunganisha, inakasirisha, haichekeshi, itauza, .........
 
Kama Kafulila ametolewa uanachama je NCCR-Mageuzi wana mtu wa kulitetea jimbo? Sina hakika hii ni sawa na kesi ya kuibiwa kuku unauza ng'ombe ili ushinde kesi
 
AMPIGIA MAGOTI MBATIA KWA MACHOZI, WAJUMBE WAKATAA KUMSAMEHE
Na Fidelis Butahe

CHAMA cha NCCR- Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urasi wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu Nec ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi.Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: "Naomba radhi, nimekosa mnisamehe..."

Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama."Hatutaki , Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...," walisikia wajumbe hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.

Dalili za Kafulila kufukuzwa zilijionyesha wazi juzi baada ya wazee wa chama hichi kupitia kwa Katibu wao wa Taifa, Ernest Mwasada kuitaka Nec kumfukuza (Kafulila kwa kuwa ndiye cha migogoro yote inayoendelea ndani chama.
"Hizi vurugu zinachochewa na Kafulila ambaye ndiyo mfadhili na kiongozi wa waasi wa uchochezi huu.
Menejimenti inapaswa kumwangalia sana, huyu ni hatari ndani ya chama hastahili kabisa kukaa na jamii yeyote inayopenda amani," alisema Mwasada. chama hicho hivi sasa.Hata hivyo, Kafulila juzi alikanusha akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba, Katibu wa Taifa wa chama hicho anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye amekosana naye.

"Ni hivi, Katibu wa Wazee wa Chama anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye hatuelewani na juzi alifanya kikao kilichoeleza mambo mengi mabaya dhidi yangu, " alisema Kafulila na kuongeza:

"Huyo Katibu wa Wazee amelishwa maneno na Ruhuza kwani ndiye mwajiri wake ambaye anafanya kazi maalumu ya kumchafua Kafulila na alifanya hivyo kwenye semina ya wenyeviti na makatibu wa chama 19 iliyomalizika jana (juzi) jijini Dar es Salaam."
Kafulila alisema kazi ya Ruhuza ni kuwanywesha sumu viongozi wa chama kuwa yeye (Kafulila) ni mkorofi badala ya kuendesha semina kuhusu mambo ya msingi ya kukijenga chama.

Aliongeza kuwa, Katibu Mkuu huyo amefikia hatua ya kutaka ionekane kuwa wenyeviti wa chama wa majimbo ya mkoa wa Kigoma wanampinga (Kafulila), lakini kati ya wenyeviti wanane ameambulia wawili tu ambao ndiyo anawanywesha sumu ya chuki dhidi yake.
 
kafulila umefulia full!
Tatizo lako umemweka mno zitto mbele, yaani unakubali kuongozwa na mawazo ya zitto kabwela, ungejifikiria tu kidogo kuwa umepata ubunge juzi tu hatabado hujaanza kutumikia wapigakura wako,tayari unajiingiza kwenye migogoro ya madaraka! Hata ungekuwa na sababu ya msingi ila ungewatumikia wananchi kwanza, na wapiga kura wako nimeambiwa hawakutaki tena kwani toka uwe mbunge umewasahau kabisa . . . .
 
Back
Top Bottom