George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 148
NATIONAL CONVENTION FOR CONSTRUCTION AND REFORM –MAGEUZI
(NCCR-MAGEUZI)
TAMKO LA CHAMA KUHUSU MASLAHI YA TAIFA LETU LA TANZANIA
Ndugu wananchi,
Baada ya kutafakari kwa kina mambo kadhaa yaliyojiri katika taifa letu hivi karibuni na yanayoendelea kutokea hapa nchini na kwingineko tumeona ipo haja ya watanzania kuwa makini sana ili taifa letu lisije likakosa mwelekeo kabisa, tusije kufika mahali tukapoteza yale yaliyo ya thamani kwetu tukaingia katika mvurugano, machafuko na hatimaye kuangamiza taifa letu sisi wenyewe. Hivi sasa kwa mfano kuna ongezeko wa utoaji wa kauli zenye shari katika majukwaa ya kisiasa, ongezeko la migogoro/migomo ya wafanayakazi, kadhalika mzozo unaoibuka kuhusu mpango wa serikali kuitafutia nchi yetu uanachama wa jumuiya ya Organization of Islamic Conference (OIC)
Ni kutokana na tafakuri yetu juu ya yote hayo, tumeonelea ni vyema tukatoa wito kwa kila mwananchi wa Tanzania kuitambua hatari hii na kuchukua hatua za maksudi la kulinusuru taifa. Hatua za kuchukuliwa na kila mmoja wetu ni pamoja na kuhakikisha kwamba kwa mawazo yetu, matendo yetu, kauli zetu zote tangia sasa zizingatie kwa dhati kabisa MASLAHI YA TAIFA.
Ndugu wananchi, kinachoendelea katika taifa letu kisiasa, kiuchumi na kijamii kinaashiria ongezeko la watu kutojali maslahi ya taifa badala yake kuzidisha umimi na uendekezaji wa maslahi binafsi na au maslahi ya wachache.
Uendekezaji huu wa maslahi binafsi una na utaendelea kutengeneza nyufa zitakazolibomoa na kulisambaratisha taifa letu. Hatuna budi basi kujisahihisha na kuamua kurejea sote kwa pamoja katika uzingativu wa MASLAHI YA TAIFA.
Ndugu wananchi, ili tuweze kuyazingatia vema maslahi hayo ya taifa hatuna budi kwanza kuyatambua ni yapi. Yamkini orodha yaweza kuwa ndefu, lakini sisi katika chama chetu cha NCCR-Mageuzi tunayatambua maslahi ya taifa kuwa ni pamoja na yafuatayo.
• Amani
• Umoja wa kitaifa
• Haki za kisheria, kijamii na uchumi
• Ustawi wa jamii
• Ulinzi na uvunaji wa rasilmali za nchi kwa manufaa ya wananchi wote
• Maendeleo ya kijamii na kiuchumi
• Usalama wa nchi
Ndugu wananchi, suala la uwepo wa amani na utunzaji wake ni la maslahi ya taifa yaliyo bayana. Hivyo mtu yeyote anayewaza na kutoa kauli zozote zinozoashiria uvunjifu wa amani, yatupasa tumtambue kuwa kwanza ni mbinafsi na tena ni mtu hatari asiyelitakia taifa letu mema. Mtu au kundi la watu wa namna hii tusiwaache wakaendelea kulihatarisha taifa letu. Hatuna budi kuwakemea watu wa namna hii na kujiepusha kuwaunga mkono kwa namna yoyote ile. Hatutakiwi tena kuendelea kuwapa fursa baadhi ya watu wanaoufanya vitendo ambavyo vina mwelekeo wa kutuondolea amani yetu.
Katika hili tunatoa wito kwa kila mtanzania kuitetea na kuilinda amani ya nchi yetu. Tunawaomba sana walioko katika vyama vya siasa na vikundi vingine vyenye fursa za kuielimisha jamii hususan katika mikusanyiko ya hadhara, wajiepushe (kwa asilimia 100) kujihusisha na jambo lolote lililo kinyume na utunzaji wa amani.
Tunatoa pia wito kwa vyombo vya habari vyote nchini, vinapoendelea kufanya kazi yenye heshima ya kuihabarisha jamii vizingatie kujiepusha na utoaji, utangazaji au uandishi wa habari zozote zinazochochea uvunjifu wa amani. Kwa mantiki hiyo habari zote wanazopatiwa watanzania hazina budi kuzingatia MASLAHI YA TAIFA.
Umoja wa kitaifa ni jambo ambalo taifa letu linauhitaji sana husuan katika kipindi hiki tulichonacho kilichogubikwa na mabadiliko mengi sana yanayoikumba dunia. Tunapaswa kwa maslahi ya taifa kudumisha umoja wa Taifa , bila kujali tofauti zozote zile tulizo nazo. MASLAHI YA TAIFA yako juu ya tofauti zetu za kiitikadi, uanachama wa vyama, imani zetu za kidini, makabila na koo zetu, madaraja ya kipato, rangi , jinsia na au umri. Tunapaswa kudumisha mifumo na taratibu zitakazohakikisha kwamba, kwa MASLAHI YA TAIFA tunajitambua kwamba sisi ni watanzania wamoja na kamwe tofauti zetu hazitugawi kwa namna yoyote ile. Kwa kuheshimu umoja wetu, ndio maana sisi katika NCCR-Mageuzi tungependa kuona kwamba hakuna masuala ya kitaifa yanayoonekena kuwa na mwelekeo wa kuvinufaisha au kuvishirikisha vikundi fulani tu katika jamii na vingine vinabaguliwa.
Mfano dhahiri ni jinsi chama cha CCM kilivyobinafsicha Mwenge wa Taifa. Ndugu wananchi, ,kadri mwenge utakavyoendelea kuonekana au kutumika kwa maslahi ya CCM, tutakuwa tumehalalisha hata upotoshaji wa lengo la msingi la kuanzishwa kwa mbio zenyewe. Tunaitaka serikali katika hili itangaze wazi kuwa mbio za mwenge zitashirikisha vijana wote wa taifa hili bila ubaguzi wowote wa kisiasa tangu sasa na siku zote.
Haki, kama inavyotajwa hata katika misahafu, inaposhamiri katika taifa lolote hakika italiinua taifa hilo. Nchi yetu inazo sheria kadhaa ambazo ndio chanzo cha ukiukwaji wa haki za wananchi. Tukichukulia mfano wa matatizo yanayowakumba walimu hivi sasa na jinsi walivyozuiliwa na mahakama kugoma. Kama tunashuhudia waalimu wa watoto wetu wakizibwa midomo kwa nguvu za dola, je tunatazamia walee vijana wetu kuwa binadamu huru au makondoo tu.
Kila mtanzania ana haki sawa na anastahili kulindwa maslahi yake na vyombo vya dola. Mbona tunashuhudia haki za raia binafsi na makundi zikivunjwa kila siku na vyombo vya dola? Mbona wastaafu wa Jumuia ya Afrika Mashariki hawalipwi malipo halali wanayodai? Mbona wafanyakazi katika sekta mbalimbali wanagoma kutokana na mishahara kiduchu na mazingira duni ya kazi na serikali haichukui hatua muafaka kuwaondolea kero zao? Mbona wanafunzi wanagoma kila kukicha, wakilalamikia mfumo mbaya wa mikopo, na serikali haiwajali?
Katika hili tunawaomba tena watanzania wote popote walipo,watu wote ambao wana mamlaka ya aina yoyote juu ya watu, watende haki yote. Hatuna budi kuondokana na ukiukaji wa haki za binadamu. Tuondokane na vitendo vya kunyanyasa watu na kuwanyima mafao yao.Amani ni tunda la haki. Hivyo tunatoa wito kwa serikali yetu, kwamba wakati umefika ichukue hatua za dhati za kuliondolea taifa sheria zote zisizotenda haki hapa nchini.
Ndugu wananchi, sote tunafahamu jinsi Mungu alivyolijalia taifa letu utajiri wa rasilimali. Wajibu wetu sote ulio MASLAHI KWA TAIFA, ni kuzitunza rasilimali hizi na kuzitumia kwa busara kubwa. Tusimame kwa pamoja sasa na kuamua kuwa kwa maslahi ya taifa tutatunza kwa uangalifu sana rasilmali na mazingira yetu. Aidha tudhamirie kuvuna na kutumia raslimali zetu kwa namna ambayo ni endelevu na inaliletea taifa letu faida. Ili zitunufaishe sisi na vizazi vyetu vijavyo.
Ustawi wa jamii, ni miongoni mwa mambo yenye maslahi makubwa kwa taifa katika mantiki ya kwamba kusitawi kwa jamii ndiko kustawi kwa kwa taifa lenyewe na watu wake. Hatuna budi sote kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunajiepusha na mambo yote yanayodumaza jamii yetu. Sote kwa pamoja tunalo jukumu kubwa la kufanya katika hili, lakini serikali yetu inao wajibu ambao imekabidhiwa rasmi na wananchi iufanye.
Tunapenda kuikumbusha serikali kwamba izingatie maslahi haya ya taifa kwa kuhakikisha inaondoa na kudhibiti vikwazo vyote vinavyozuia ustawi wa mtanzania mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Tunaitaka serikali iondokane na matumizi ya sera au programu zinazonyima watu fursa ya kupata elimu bora hadi upeo wao. Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba jamii nzima inapata huduma za afya na maji bila ubabaishaji wowote na visingizio visivyoisha.
Kwa bahati mbaya baadhi ya watumishi wa umma na viongozi wetu wamekengeuka kimaadili katika nafasi zao za kazi na wametindikiwa uaminifu. Ndugu wananchi, katika baadhi ya nchi hapa ulimwenguni ambako watu wake wanajali maslahi ya taifa lao, wanajivunia uwepo wa ‘zero corruption' tuamue sasa kwa maslahi ya taifa kuchapa kazi na kurejesha kiwango cha juu cha uaminifu katika nafasi zetu za utumishi.Tupige vita ufisadi Kwani huyu ni adui wa kwanza wa taifa.
Sisi katika NCCR-Mageuzi kuanzia sasa program zetu za elimu ya uraia na ziara tutakazozifanya katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu zitatanguliwa na dhima hii ya MASLAHI YA TAIFA.
Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania, utuwezeshe tuyalinde maslahi ya taifa letu.
Ahsanteni kwa kutusililiza,
Imetolewa na Secretariat ya Halmashauri kuu ya Taifa,
NCCR-Mageuzi