NCCR Mageuzi yakataa kushiriki mazungumzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR Mageuzi yakataa kushiriki mazungumzo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by February, Nov 25, 2011.

 1. February

  February Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mbunge wa kigoma kusini na katibu mwenezi wa nccr mageuzi david kafulila amesema chama chao hakihitaji kukutana na Rais JK kwakuwa CCM, Serikali na hata Rais mwenyewe haina dhamira ya kweli ya kuleta katiba mpya.

  Kafulila aliliambia tzdaima kuwa wameshangazwa na kauli ya ccm ya kutaka mazungumzo hayo yahusishe vyama vingine. Uamuzi wa kamati kuu ya ccm kuwa vyama vyote vikutane na JK. Sioni mantiki yake badala yake naona akutane na wanaotaka kukutana nae alisema Kafulila na kuongeza

  "Binafsi sitegemei lolote kutoka katika kikao kwa namna hiyo. Wabunge wa nccr hawakutoka bungeni ili badae wakutane na rais. Tunaamini yeye rais, chama chake ccm na hata serikali yake hawana dhamira yakweli katika agenda ya katiba mpya tangu awali na hawatakuwa nayo" akitetea kauli yake, kafulila alisema CCM haiko tayari kukubali mabadiliko kwani ni msumari kwake yeye, ccm na serikali yake.

  Akifafanua hoja hiyo kafulila alitoa mifano mitano kuthibitisha hilo. Kwanza ccm walikataa kuingiza agenda ya katiba kwenye ilani yao ingawa ilikuwa mahitaji ya umma, pili hata bada ya uchaguzi mwanasheria mkuu na waziri wa sheria na katiba waliweka wazi kuwa katiba mpya sio muhimu kwasasa kauli ambayo haijafutwa. Tatu ni kwa msingi huo mwezi april serikali kupitia baraza la mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni rais walileta muswada mbovu kabisa ulioibua hasira hata kutakiwa urejeshwe serikalini. Nne bada ya kurudisha kikao kilichopita wamerudisha muswada mpya ambao ilitakiwa usomwe kwa mara ya kwanza ili umma upate nafasi kujadili lakini serikali na ccm wamekataa.

  Na kuhitimishwa na kikao cha rais na wazee wa ccm mkoa wa dar kupuuza sauti ya umma ndani na nje ya bunge. Huu ni ushadi tosha kuwa hakuna dhamira ya kweli kutoka kwa rais na chama chake na hivyo nccr hatuoni sababu ya kushiriki alihitimisha Kafulila.
   
 2. February

  February Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimesoma story hii tanzaniadaima na nipashe nikaipenda lakin najiuliza kweli huu ni msimamo wa nccr au kafulila binafsi?
   
 3. S

  Sina pa kwenda Senior Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Safi sana maana haiwezekani barua wepeleke wengine nyie halafu wajibu eti wakutane na vyama vyote vya upinzani
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuuliza namna hii wewe unataka choko choko kesha sema masimamo wa NCCR nawe si NCCR unahoji zaidi ili iweje wewe jikite kwenye mada kwamba wamekataa wao NCCR.

  Kitendo cha vyamma vingine kukubali ku join maongezi haya kutathibitisha kutumiwa na CCM maana watakuwa hawana maana maamuzi hado NEC ya CCM iseme ndiyo wao wasimame kufuata .Kama watasikiliza haya wacha tuone ni wapi wanapokea order za CCM na kwa nini .
   
 5. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Aibu kwa serikali ya CCM kujitia wasemaji wa vyama vya upinzani.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo James Mbatia hatohudhuria hicho kikao?
   
 7. R

  Rockabie Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I find it logical...!
   
 8. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Mwamakula, mimi naungana mkono na kafulila. Sijui ni kwa nini Watanzania tunaishi kwa mazoea ya kuwaamini hata watu ambao tayari jana yake tu wametuumiza. Kwa kifupi Watanzania tu wavivu wa kufikiria hata nini tunahitaji. Pa1 na kelele zoote na mahubiri ya CHADEMA na wanaharakati, bado kuna watu hawaoni na hawana haja ya kutafakari tulipo, badala yake wanakuwa wa kwanza kusema CHADEMA na WANAHARAKATI wanataka kutuletea vurugu.

  Uzembe wa kufikiri wa Watanzania, hautupi nafasi ya kukumbuka kuwa waha vigeugeu wanaojipa sasa kazi ya kuratibu mchakato, mwanzoni walipinga KABISAAAA wazo zima la kuwa na katiba mpya.

  Lkn haya yote mimi nayaona 9, kumi ni hoja za upande wa pili uliodai hata kufurahishwa na hotuba ya Rais aliyowahutubia wacheza bao wa mwembe Yanga. Wao wanasema wamefurahishwa sana na hotuba nzuri (kwa namna hii hata KHANGA watainunua kwa maneno yake na sio ubora) na ahadi iliyotolewa na Rais (ambaye aliwahi kuwaahidi Waislamu mahakama ya Kadhi=nao wamesahau tayari) ya kwamba watu wote watafikiwa na kupata fursa ya kutoa maoni yao. Sasa hapa ndio utaona tu kuwa sio tuna uzembe tu, bali na utaahira juu yake: Hivi nia ni kila mmoja atoe maoni, au maoni ya kila mmoja yafanyiwe kazi?

  Tatizo hapa ni ubongo wa Mtanzania unaopenda likizo kuliko kazi. CCM ina kawaida ya kukubali jambo kwa mdomo na kuhakikisha linaundiwa tume ya KULIKWAMISHA. Mambumbumbu wenzangu tunaotaka CHADEMA na WANAHARAKATI wakae kimya 'ili tutunze amani', tumeshajiuliza serikali ingepungua wapi kama muswada huu ungejadiliwa na wananchi kwanza?

  Mwenye akili angalau kidogo angeona tu kuwa serikali yetu ni serikali ya ajabu kutokana na nafasi tunayoipa ya kujifanyia mambo kwa kadiri wanavyotaka.

  Juzi hapa Kamanda wa CCM wa Kanda Maalum ya DSM CCP Sule Kova, ametoa karipio la kukataza Maandamano ya Amani ya KUPINGA MAMBO YA AJABU YALIYOFANYWA NA BUNGE LA NDOA kwa kisingizio cha Al Shabaab.
  Hebu tujiulize,
  1. Tutaahirisha sherehe za UHURU kwa sababu ya Al Shaabab?
  2. Maandamano ya Mch. (sijui nani wa kilokole) kwa sababu ya Al Shaabab?
  3.Tamasha la MP Sugu na masharobaro nalo litaahirishwa kwa sababu ya tishio la Al Shaabab?
  Hapa utapata jibu tu kuwa CCM wanapinga katiba kabla hata haijatungwa. Kukataza maandamano ni kumnyima Mtanzania haki ya KIKATIBA. Sasa mnatoa wapi hii IMANI mbovu kuwa Rais na CCM na Jeshi lao wana nia ya kusimamia huu mchakato na kuufanikisha ikiwa mambo yao ndio haya?

  Watanzania tuache kuwapigia makofi watu wanaotuvuruga huku tunawalaani wanaotutetea kwa kuwa tu tumeelekezwa hivyo na wanaojua namna watakavyonufaika na katiba MBOVU.

  NOTE: Kwa maoni yangu, mtu yeyote ambaye mpk sasa haoni kuwa jeshi la polisi ni sehemu ya CCM basi hata kubakwa kwake ni rahisi. Mtu atakuvua nguo, atakupaka mafuta sehemu za siri na bado utaniambia hujui nia yake kwa hiyo unasubiri afanye hicho anachotaka kufanya ndio ugome. Kama kweli tuna tishio la Al Shaabab kama alivyotanabahisha kamanda wa CCM kanda maalum ya Dar es salaam, basi jambo la kulizuia sio maandamano ya Watanzania bali ushiriki wa timu za Kenya na Uganda ktk mashindano ya CHALLENGE kwani hao wawili ndio wanaweza kutuletea Al Shaabab hapa kwetu kwani tayari wana ugomvi nao huko kwao. Vinginevyo nitaendelea kuamini ninachoamini kuhusu jeshi letu la polisi.
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  thats good. Big up Kafulila
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Kwanini siku zote ccm na serikali yake wamekuwa ni waoga kukutana na CDM make nakumbuka hata Arusha waligwaya pia..ccm mmeombwa kukutana na CDM ndo wanaoona wana ajenda ya kuongea,nyie mnakwenda kuwaita wengne,kwani nao waliwaomba?na ni kwanini kama mnaogopa kukutana na CDM msiwe wazi tukajua mnaigwaya CDM?
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  CUF itashiriki tatizo liko wapi ?.
   
 12. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  CUF nisehemu ya CCM sasa watashiriki vipi? kwa kuvua kwanza shati la CCM au ?
   
 13. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Tatizo lipo. Pale CHADEMA hawaendi kuongea na Mwenyekiti wa CCM bali Rais.

  Ingekuwa wanakwenda kuongea na CCM ingekuwa ruksa kwa CUF nao kushiriki kwani ukienda kwa mtu huwezi kumbagua 'mamsap wake'.
   
 14. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni janja tu ya kutaka kuwaingiza wake zao kwenye mazungumzo ili na ushabiki na kijikomba viwe sehemu ya ajenda. We mtu mwanaume mwenzio kakuomba mzungumze unaanza kujumuisha na mahausgel kwenye orodha wa nini sasa!
   
 15. Kiwewe

  Kiwewe Senior Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbona Kamati kuu haikumshauri JK asiongee na wazee wa CCM pekeyake, kwani ninaamini siyo wazee wote waliopo Dar ni CCM. Unajua usanii umeshapitiliza sasa hadi watoto wadogo wanayajua mazingaombwe ya CCM. Nafikiri wamefika mwisho wa kufikiri, na wachache wenye busara hawana nafasi tena ndani ya chama chetu cha "mapinduzi". Tanzania yetu.....
   
 16. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kumekuwepo na malalamiko kuwa JK anapelekewa na wasaidizi wake taarifa zilizopindishwa na au za kuficha ukweli. Ninawashauri NCCR waungane na CDM kukabiliana na Rais ana kwa ana ili tuone uamuzi atakao kuwa nao baada ya wapinzani kutoa hoja zao live.

  Hii ni chance ya pekee sana kwa wapinzani. Ninawashauri waitumie. Raisi akikataa hoja za wapinzani na akaamua kusaini mswaada, basi waende kwa wananchi.

  Vinginevyo kama Raisi ataafiki hoja za wapinzani na akamua kutosaini mswaada basi suala la maandamano litakuwa limeisha. Pimeni busara hii kwa mawazo chanya.
   
 17. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  The scheduled talks between JK and Chadema will not bring any difference with regard to making of a new constitution. The fact that Chadema's MPs failed to use their parliamentarian platform to block the bill from being sanctioned is enough to explain on how less strategic they are.

  Chadema should regret their own puerility that drove them to boycott the debate while they could have used same existing constitution provisions to impede the smooth sanction of the bill by Magamba.

  As things turned out, CCM took an advantage of Chadema's absence plus their overwhelming majority to pass the bill unchallenged.
   
 18. S

  STIDE JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mambumbumbu wenzangu tunaotaka CHADEMA na WANAHARAKATI wakae kimya 'ili tutunze amani', tumeshajiuliza serikali ingepungua wapi kama muswada huu ungejadiliwa na wananchi kwanza?

  Mwenye akili angalau kidogo angeona tu kuwa serikali yetu ni serikali ya ajabu kutokana na nafasi tunayoipa ya kujifanyia mambo kwa kadiri wanavyotaka. Juzi hapa Kamanda wa CCM w
  Hii imenikomaza imani yangu kwa CDM
   
 19. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #19
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Uwe msimamo wa Kafulila au wa NCCR lakini alichosema Kafulila ni sahihi kuwa CCM hawana dhamira ya kweli na katoa mifano hai.

  Wewe mpaka uelewe ni msimamo wa nani ndio ukubali kuwa unaibiwa?
   
 20. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #20
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...mkuu kwanza naungo mkono hoja 100%,pili nimelikubali sana hili badiko lako,kwa ufupi ni kwamba umesomeka vizuri sana hasa hapo kwenye...

  Sijui eti mtu anakupaka mafuta we' ulivyo na akili mgando unamwangalia tu,unasubiri akufanyie kitu mbaya ndo ukurupuke!...haa haa haa kwiii kwiii kwiii...sio siri mkuu umefikiria zaidi ya akili...

  ndo maana mi naipenda sana JF coz kuna watu humu waifanya akiliyangu ifikiri zaidi ya kawaida...pamoja sana mkuu!...
   
Loading...