NCCR-Mageuzi wazidi kuishambulia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR-Mageuzi wazidi kuishambulia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, May 27, 2012.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  na Mwandishi wa Tanzania Daima, Mtwara

  VIONGOZI wa kitaifa wa Chama cha NCCR –Mageuzi, walioko mjini hapa, wameendelea kukishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwataka wananchi wasikichague katika uchaguzi wowote.

  Wamesema kama wananchi wanataka maendeleo ya kweli, na njia pekee ya kuwafikisha mahali hapo ni kukihama chama hicho tawala kwa kuwa ndicho kimesababisha maisha magumu yanayowakabili.

  Mashambulizi hayo yalitolewa jana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Danda Juju na Salum Msabaha walipokuwa wakihutubia mikutano ya hadhara katika Majimbo ya Mtwara Mjini na Nanyumbu.

  Akihutubia katika Jimbo la Nanyumbu, Juju alisema umefika wakati sasa wananchi wa Mtwara kuonyesha kwa vitendo jinsi wanavyochukia maisha magumu yanayosababishwa na CCM kwa vile bila kufanya hivyo maisha bora kwa kila Mtanzania hayatapatikana.

  "Ndugu zangu, wakoloni tuliwakataa na kuwataka watuachie nchi yetu kwa sababu walishindwa kutufikisha mahali tulipokuwa tukitakiwa kufika ikiwamo kutotoa demokrasia ya kweli.

  "Wakoloni tuliwakataa kwa sababu hatukuona sababu ya kuendelea nao, lakini kwa bahati mbaya baada ya watu hao kutuachia nchi yetu, wamekuja wakoloni wengine ambao ni CCM, hawa nao sasa wanatakiwa kutupisha.

  "CCM hawana tena chao, waambieni tumechoka, waambieni hatuwataki tena kwa sababu hao CCM ndio wanaosababisha zao la korosho linakosa bei na hao hao ndio wanaosababisha maisha magumu kwa kila Mtanzania.

  "Maisha kila siku yanakuwa magumu, yaani nawahakikishia kama mtaendelea kuichagua CCM ipo siku mtaanza kula mlo mmoja kwa siku ingawa sasa wengi wetu tunaishi maisha ya kubahatisha," alisema Juju.

  Naye Msabaha alisema kama viongozi wa serikali wataendelea kutumia vibaya rasilimali za taifa, chama hicho kitaitisha maandamano ya aina yake kwa wananchi kuzingira nyumba za viongozi hao, ili kuwashinikiza wajiuzulu.

  "Korosho mnakopwa kila siku halafu mnapolipwa mnakatwa makato yasiyokuwa na maana, nawaambia kama viongzi wataendelea kuwanyanyasa wananchi, sisi NCCR tutakuja na maandamano mapya na ya aina yake.
   
 2. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  wameamka!!!
   
 3. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama Danda Juju na Salum Msabaha ndio washambuliaji wa NCCR Mageuzi basi niseme tu hicho chama kimekwisha! Walipokuwa kwetu Chadema tulikuwa tunawatumia kama watundika bendera.

  TUMBIRI,

  tumbiri@jamiiforums.com
   
 4. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Rooney wa Manchester United pindi akiwa Everton alikua ball boy na hata Steven Gerald mwenyewe alikua msafisha viatu vya kina Paul Ince na Robbie fowler pale Liverpool. Au umesahau mchonga alikua mwalimu Pugu? Jipange weweee!
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Lakini Mwenyekiti wao yuko Kimya eti? Naona anasaini stipend zake za kuhudhuria Midahalo ya Bunge bila tatizo...

  Wanaita nini tena ilitumika sana Nigeria wakati wa Utawala wa Mkoloni wa kiingereza DIVIDE AND RULE... Uliona

  Mwenyekiti wa CUF alijua hiyo akakataa; anajua Historia, kijana wetu wa NCCR yeye na tumbo ni kavu akakubali, kauza

  NCCR kiundani ndani bila kujua
   
 6. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  CHADEMA inavyojitambulisha mbele ya watanzania si chama cha mabwana na watwana, sijui wewe unazungumzia 'chadema' ipi. Kama ndivyo mlivyo, basi pole. Ila NCCR imewapa heshima hawa maana inatambua na kuheshimu UTU wa kila mtu na haki yake ya kushiriki siasa
   
 7. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hili unalolisema amekwisha kulijibu, na yeye mwenyewe yuko ziarani Mtwara na Lindi. Acheni mitazamo isiyozingatia ukweli.
  View attachment mbatia sifungwi.bmp
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi huwa siongei na mbwa nasubiri mwenye mbwa.
  kumbe mwenye mbwa naye kafugwa?
  hapo nasubiri kichaa,ni risasi tuu.
   
 9. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo mwaka huu...
   
 10. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanao ambae yupo shule ya msingi akikusema je utaogopa? jibu ni laa but yule ambae anajitegemea utaogopa sivyo? HIVYO CCM HAWNA SHAKA NA NCCR KABISA NI KAMA MWANA WA SHULE YA MSINGI
   
 11. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Shughuli ipo Tanzania hii!jamani huko ZNB wana wa UAMSHO wamewaka huku siyo Magwanda wala NCCR-Mageuzi wamechoka Juu ya Magamba.
  Kazi kweli kweli.
   
 12. M

  Mawazo metusela Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hahahahahahahhaaaa jamani Khaaaa, anayeshambulia jukwaa ni nani?................. duhhhh jamani Naomba nisi seme chochote wadau wamemaliza kazi
   
 13. R

  ROMEOWALLACE New Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaliyotabiliwa wa waasisi yanatimia
   
Loading...