NCCR-Mageuzi kumpigia kampeni Zitto

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema chama chake kitamuunga mkono Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) endapo atagombea ubunge katika jimbo lolote mkoani humo.

Sambamba na kauli hiyo ya Mbatia, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, David Kafulila ametangaza nia rasmi ya kugombea ubunge Kigoma Kusini na kusisitiza kuwa kama vile Zitto alivyoweka msimamo wa kumuunga mkono, naye atamuunga mkono katika jimbo atakalogombea.

Kafulila akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, katika kikao maalumu, alisema msimamo wa Mbatia kumuunga mkono Zitto aliutoa Februari mwaka huu katika Kijiji cha Mwandiga mkoani Kigoma alipohutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho.

Jimbo la Kigoma Kusini anakotaka kugombea Kafulila, hivi sasa linashikiliwa na Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mwanasiasa wa siku nyingi, Manju Msambia.

Kafulila akifafanua kauli hiyo ya Mbatia na msimamo wake, alisema ni wazi kuwa umoja wa upinzani bado upo na mwaka huu umelengwa kuimarishwa zaidi ingawa alikiri kuwa ngazi ya urais, nafasi kubwa ya kushinda ipo kwa CCM.
 
Back
Top Bottom