NBS yawanyima mshahara wa mwisho wadadisi 550s mradi wa HBS baada ya kumaliza mkataba.

Amoxlin

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,784
4,097
Katika hali isiyo ya kawaida wadadisi zaidi ya 550 waliokuwa wakifanya utafiti wa "mapato na matumizi ya kaya binafsi" (HBS) tangu Dec 2017 na kumaliza Nov 2018 hawajalipwa mshahara wa mwisho wa mwezi uliopita mpaka hivi sasa bila ya maelezo yeyote.

Baada ya kumaliza mkataba wadadisi hao walielekezwa kukusanya vitendea kazi vyote walivyokua wakivitumia katika utafiti huo jambo ambalo walilitekeleza bila kupinga.

Pamoja na kunyimwa mishahara pia hakuna taarifa zozote za upatikanaji wa viinua mgongo vyao wanavyotakiwa kulipwa kwani ajira yao ni ya miezi 12 tu.

Hakuna kiongozi yeyote mwenye kujali kilio cha wadadisi hawa pamoja na hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi wote kwa sasa.

Ifike mahali serikali iwajali watumishi wake na si kuwakandamiza na kuwanyonya kama wanavyowafanyia watumishi hawa.
 
Back
Top Bottom