Tutafika
JF-Expert Member
- Nov 4, 2009
- 1,443
- 631
NATIONAL BUREAU OF STATISTICS (NBS)
National Bureau of Statistics Tanzania - NBS
Hii taasisi, kusema kweli watanzania wengi hawaijui. Si kwa sababu hakuna ufisadi unaoendelea huko, hasha!, ni kwa sababu ya kushidwa kwake kutekeleza majukumu. Taasisi hii inategemewa kutoa takwimu za kitaifa za mambo yote yanayolihusu taifa la Tanzania. Mambo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, n.k. Hii taasisi inategemewa itoe hali halisi ya nchi yetu na itoe habari zinazoendana na wakati.
Kwanini nasema inatudharirisha?
Kila mtu anajua umuhimu wa takwimu na jinsi takwimu zinavyoweza kutumika vibaya zikaleta adhari kubwa katika maisha ya mtu mmoja mmoja. Takwimu zinazotumika kuielezea Tanzania kimataifa hazitokani na taasisi hii na wala haijawahi kusema lolote kuhusu takwimu hizo. Kimsingi Takwimu hizo zimekosewa ama kwa makusudi au kwa kukosa takwimu mbadala (za ukweli). Takwimu zinazopatikana https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html nyingi hasa za kiuchumi sio za kweli na zinatudharirisha. Nani anawajibika katika hili?, bila shaka ni hii taasisi.
Wanauchumi wanajua jinsi kipimo cha uchumi - GDP, ambavyo kinatumika kufanya watu wajione wanyonge na wajidharau. GDP kwa nchi kama yetu ambayo watu wake wanaishi kwa kutegemea kilimo na ambayo zaidi ya asilimia 75 wanalima na kula wenyewe bila kuuza, haiwezi kuonesha hali halisi ya maisha ya mtanzania. haiwezi kuwa kipimo cha umasikini wetu. Katika hili, NBS ilitakiwa iwe ya kwanza kupima uchumi wetu na kuweka takwimu sahihi zinazojumuisha uzalishaji wa watu wote, lakini cha kushangaza, hata takwimu za uchumi wetu hazipo NBS!!
Je, kuna haja ya kuwa na taasisi hii isiyo na faida?, Viongozi wa Taasisi hii wanafanya nini?,