NBS ilikadiria Tanzania tutakuwa Mil.61.3, Actual figures ni Mil.61.7. Kuna Haja gani Kutumia Mabilioni kufanya Sensa?

Mkuu. Census sio tu kuhesabu watu tujue wapo wangapi. Pia ku rekodi takwimu zao ndo maanua uliulizwa hadi una kuku wangapi pia sababu za usalama.

Kwa taarifa yako sasa pale makao makuu wanaweza wakaamua wazima umeme nyumba yako peke yake. Yani kama ulifanya Census na taarifa ukatoa jua umeingia cha kike. Sasaivi watu wanaweza kukujua nje ndani kama FBI
Acha upotoshaji. Hakuna mtu anaweza kuzimiwa umeme peke yake. Taarifa za sensa ni lengo la kupanga mipango ya serikali na siyo kuhujuku wananchi
 
Siyo lazima wote waishi. Lazima wengine mfe kwa kukosa maji ili kuwe na balance. Nani kakwambia masikini ana haki ya kuishi. Kwanza umaskini ni laana hata mungu hapendi na hataki kabisa kumuona maskini
Mungu mwenyewe ni tajiri. Shetani ni masikini na ndiye alienda kwa Mungu kumchomea Ayubu aliyekuwa na mali nyingi. Kama shetani angekuwa tajiri, asingekuwa na muda na mambo ya watu
 
Ndugu yangu tuna serikali za mitaa zina takwimu za makazi na kila kitu ,mambo gani tusiyajue?

Mbona zoezi la anuani za makulazi likikuwa na bajeti isiyozidi bil.30 na tumeweza kila kitu?

Justification ya Bili.400 ni ipi hasa?
Sensa inafanyika kwa mujibu wa Sheria namba 351. Sheria hii inampa NBS na Mtakwimu Mkuu wa Serikali mamlaka ya kuendesha zoezi la sensa kwa kushirikiana na wadau wakiwamo serikali za mitaa.

Kitaalamu, sensa haiwezi kufanywa na serikali za mitaa kwa sababu, kwanza, serikali za mitaa ndiyo wenye jukumu la kuhudumia wananchi, na kujua ubora wa huduma hizo ni moja ya kazi ya sensa.

Sasa, ili kupata taarifa sahihi na zisizo na upendeleo, serikali za mitaa haziwezi kupewa kazi ya kukusanya taarifa kwa sababu ni kama zitakuwa zinajihoji zenyewe. Unatarajia watoe majibu sahihi bila kupindisha?
 
Wakuu habari za kazi.

Mwezi July Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS Ilikadiria idadi ya watu Tanzania itakuwa Milioni 61.3 na Matokeo rasmi ya Sensa yaliyotangazwa na Rais baada ya sensa ni watu Milioni 61.7, tofauti ni watu laki 4 tu.

Swali kulikuwa na haja gani ya kutumia zaidi ya Bil.400 za walipa Kodi wakati Taasisi yetu yetu ya Takwimu ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 98 kwenye kufanya projections?

Mabilioni Yale kwa sasa yangekuwa yanatatua shida ya Maji.

Ushauri Kwa serikali, next time kusiwe na haja ya kutumia mabilioni ya pesa kufanya sensa bali tuwekeze kwenye mifumo Ili ifanye Kazi maana tumeshaona sasa kwamba NBS imeleta ufanisi wa projections zake.👇

View attachment 2402986
Mimi sikuwahi kuhesabiwa!
 
Mifumo inaweza pata hata hizo Takwimu zingine unazosema..

Takwimu gani haiwezi kupatikana hadi ihitaji mabilioni?
Nikeshakujibu kwenye post nyingine.

Cha kuongezea tu, sisi makarani wa sensa hatukuruhusiwa kuhoji na kuchukua taarifa zetu wenyewe kwenye kaya zetu, kaya za wazazi wetu, ndugu na majirani pia hatukuruhusiwa. Kila karani alipangwa sehemu isiyo na watu wa aina hiyo. Kaya ya karani ilihojiwa na karani mwingine, ili kuondoa kujipendelea.

Hivyo hivyo, serikali za mitaa haziwezi kuruhusiwa kujihoji maana wao nao ni sehemu ya wahojiwa.

Yaani maswala ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi zinawahusu Halmashauri, halafu hao hao halmashauri tena wakapewe kazi ya kuuliza hayo maswali ya sensa kwa wananchi, si utatengeneza majibu?
 
Na mbaya zaidi... sipendi kuamini kwamba hiyo idadi ni accurate...just imagine Tume ya Uchaguzi (NEC) yenye uzoefu mkubwa wa kufanya, kukokotoa hesabu na idadi kila baada ya miaka 5 haijawahi ku-execute zoezi la kuhesabu accurately regardless ya ku-cover number chache (10-15m maximum) na inayojileta yenyewe kwenye polling stations, sembuse kumsaka na kumhesabu mtanzania asiyekuwa na ajira wala makazi rasmi!?...nachelea kusema kunaweza kuwa na tofauti ya asilimia sio chini ya 4 hadi 8. COMPETENCY yetu bado iko chini kupata alama japo 90 kati ya 100 katika kutimiza majukumu yetu binafsi au ya kitaifa..na hii ni kila nyanja yoyote katika Taifa letu.
Nchi ya kula tu hii hakuna namna
 
Yes mkuu umegusia kitu muhimu ambacho kama nchi tulitakiwa tuwe tunafanya,mtoto anapozaliwa wazazi wanampa Jina ili atambulike,hivyo hivyo kwa nchi ilitakiwa apewe Jina(ID number)na hii number unaishi nayo na kufa nayo!,tuendelee kunywa support mifupa tutaikuta chini
Shida ya nchi hii watawala wanawaza namna ya kupiga pesa za umma
 
Wapo pia watendaji wa vijiji/mitaa na kata, hawa wanaweza kutoa hesabu inayofanana na ukweli zaidi kuliko ile siku/wiki moja ya sensa.
Taasisi nyingi za serikali hifanya kazi kwa kukariri yaliyopita badala ya kubuni mbinu mpya kuendana na wakati.
Kikubwa wao wanawaza namna bora ya kupata posho
 
Tujiulize kwa wenzetu huko mbele je huwa sensa wanafanya fanyaje, maana haya maswala si yapo duniani kote?
Mi nadhani tutakuta wanatumia hiyo mifumo vizuri lakini huku tunakopenda miradi ya kujichotea utakuta watu wanajifanya wazito kuadapt new mechanism ili waendelee na mianya yao,
Ni ulafi na ufisadi wa fedha za umma pekee
 
Mabilioni Yale kwa sasa yangekuwa yanatatua shida ya Maji.

Ushauri Kwa serikali, next time kusiwe na haja ya kutumia mabilioni ya pesa kufanya sensa bali tuwekeze kwenye mifumo Ili ifanye Kazi maana tumeshaona sasa kwamba NBS imeleta ufanisi wa projections zake
Kwanza huo "ufanisi wa zaidi ya asilimia 98", wewe umeutoa wapi?

Kwa hiyo kwa mawazo yako haya unataka hata Mamlaka ya hali ya Hewa nao taarifa zao ziwe ndiyo mategemeo ya nchi, maana hata wao hufanya 'projections' zao kadri sayansi yao inavyowaruhusu?

Naona katika maoni yako haya umeshindwa tu kumalizia maelezo yako kuhusu umuhimu wa taarifa sahihi za NBS kutangazwa kwa kurusha helikopta ili ionekane wanavyofanya kazi kwa ufanisi mkubwa!
 
Sensa ni mchakato wa kukusanya takwimu za watu na hali zao kiuchumi na kijamii.
Takwimu hizo zinahusisha siyo tu kujua idadi ya watu bali pia hali za kiuchumi, ajira, kazi, afya, kujua vituo vya kutolea afya vipo vingapi na vina hali gani.

Ndiyo maana ikaitwa sensa ya watu na makazi.

Sisi tuliokuwa makarani, tulikuwa madodoso kadhaa. Dodoso kuu lilikuwa na maswali zaidi ya 100.

Kikubwa kwenye hilo dodoso ni kudadisi hali za watu katika jamii. Na hapa ndipo ujue kwamba karani husimama kama mdadisi.

Mimi pia nilifanya udadisi kama nilivyoelekezwa na taarifa ndizo hizo unasikia NBS wanasema wanazichakata.

Dodoso la jamii nalo lilikuwa na maswali yahusuyo huduma za jamii kama masoko, shule, makanisa, hospitali na hali halisi ya huduma hizo.

Dodoso la majengo lilikuwa na maswali 30. Haya yalilenga kudadisi umiliki wa nyumba, ukubwa wake, idadi ya watu wanaolala, na ubora wa nyumba pia kujau aina ya nyumba.

Kwa hiyo, sensa ni sayansi pana, siyo kujua tu kwamba watu ni wangapi.

Hata ukiwa nyumbani kwako, unahitaji kujua una watu wangapi, wa hali gani, hadhi gani, na mahitaji gani na ni wangapi wanatarajiwa kuja/kuzaliwa ndipo upange mipango ya muda mfupi, wa kati na ujao.

Tatizo kuna watu hudhani kwamba kila mradi serikali inafanya hauna maana zaidi ya upigaji
Kuna mtu nchi hii hajui hali ya uchumi nk nk.
 
Unaelewa maana ya mifumo? Wizara ya mifugo ina Takwimu zote hizo hata kabla ya sensa..

Ukielewa maana ya mifumo inayofanya Kazi kuanzia ngazi ya mtaa huko Wala huwezi umiza kichwa,haihitaji hizo billions of money Mzee..

Nchi nyingine za Africa huwa sensa wanafanyeje? Usilete mambo ya ukihiyo hapa! Unawaza tu bilioni 400! Nenda katafute za kwako!
 
Hao watu ni wachache Sana kwa kuwaweka kwenye mtawanyiko..

Karibu kuchukua idadi ya shule afu gawanya utaona impacts yao ni insignificant..

Utumie Bil.450 kuwatafuta watu laki 4? Una akili timamu?
Hiyo ni idadi ya watu wa manispaa zisizo majiji..sensa haihesabu watu tu Kama mfugaji na ng'ombe wake,pili Kama serikali/taifa huwezi fanya mambo kwa kukadiria
 
Mtoa Mada ndo wale watu Ccm inajivunia kuwa nao hawana Muda wa kudadisi Wala kuhoji Mambo ya Msingi anamekalili kuwa sensa nikuhesabu watu to! Inaumiza Sana hakika nchi ina watu Mbumbumbu wengi
 
Sensa ni mchakato wa kukusanya takwimu za watu na hali zao kiuchumi na kijamii.
Takwimu hizo zinahusisha siyo tu kujua idadi ya watu bali pia hali za kiuchumi, ajira, kazi, afya, kujua vituo vya kutolea afya vipo vingapi na vina hali gani.

Ndiyo maana ikaitwa sensa ya watu na makazi.

Sisi tuliokuwa makarani, tulikuwa madodoso kadhaa. Dodoso kuu lilikuwa na maswali zaidi ya 100.

Kikubwa kwenye hilo dodoso ni kudadisi hali za watu katika jamii. Na hapa ndipo ujue kwamba karani husimama kama mdadisi.

Mimi pia nilifanya udadisi kama nilivyoelekezwa na taarifa ndizo hizo unasikia NBS wanasema wanazichakata.

Dodoso la jamii nalo lilikuwa na maswali yahusuyo huduma za jamii kama masoko, shule, makanisa, hospitali na hali halisi ya huduma hizo.

Dodoso la majengo lilikuwa na maswali 30. Haya yalilenga kudadisi umiliki wa nyumba, ukubwa wake, idadi ya watu wanaolala, na ubora wa nyumba pia kujau aina ya nyumba.

Kwa hiyo, sensa ni sayansi pana, siyo kujua tu kwamba watu ni wangapi.

Hata ukiwa nyumbani kwako, unahitaji kujua una watu wangapi, wa hali gani, hadhi gani, na mahitaji gani na ni wangapi wanatarajiwa kuja/kuzaliwa ndipo upange mipango ya muda mfupi, wa kati na ujao.

Tatizo kuna watu hudhani kwamba kila mradi serikali inafanya hauna maana zaidi ya upigaji
Unataka kuniambia serikali inayohudumia vituo vya afya haijui idadi yake? Shule haijui idadi kila siku inahudumia? Tabu za maji, umeme na barabara mbovu haioni, hali za watu kuwa masikini haioni? Wacha porojo wewe
 
Back
Top Bottom