NBC yachangia kituo cha afya cha Mt. Benedict Kitunda, Dar


Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Likes
137
Points
160
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 137 160
03.JPG


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kushoto) akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, Dr. Norbet Mtega (kushoto) wakati wakitembelea jengo jipya la Kituo cha Afya cha Mt. Benedict katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho ambako Benki ya NBC kupitia Mshauri wake wa Mambo ya Habari, Redemptus Masanja (kulia) ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 zitakazotumika kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo hicho. Wa pili kulia ni Sr. Maria Agnesia OSB wa kituo hicho. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

01.JPG
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 10 kutoka kwa Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja zilizotolewa na NBC kama sehemu ya mchango wake kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichoko Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. NBC pia imefungua akaunti maalumu kupata fedha zitakazosaidia kufanikisha ununuzi huo. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, Dr. Norbet Mtega na wa tatu kushoto ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Mt. Agness la watawa Wabenedictini, Sr. Maria Shukrani Mkonde OSB.02.JPG
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza kabla ya kupo mfano wa hundi ya shs milioni 10 kutoka kwa Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (kulia kabisa nyuma) zilizotolewa na NBC kama sehemu ya mchango wake kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichoko Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, Dr. Norbet Mtega na kulia ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Agness la watawa Wabenedictini, Sr. Maria Shukrani Mkonde OSB.

04.JPGWacheza ngoma ya asili wakitoa burudani katika hafla ya uzinduzi
wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict hafla ambayo Benki ya NBC ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa gari la wagonjwa wa kituo hicho. NBC pia imefungua akaunti maalumu ili kukusanya fedha zitakazotumika kukamilisha ununuzi hu. I cant imagine, they were dancing Lizombe, Ligwamba or Chihoda? Just curiosity.
 
K

Kana Amuchi

Member
Joined
Jul 21, 2009
Messages
70
Likes
0
Points
0
K

Kana Amuchi

Member
Joined Jul 21, 2009
70 0 0
we acha masihara lizombe Kitunda? Ritungu hilo!! huoni shingo zilivyokaa?
 

Forum statistics

Threads 1,236,316
Members 475,099
Posts 29,254,003