Nbc mnafanya nini na dola za watu.

Nbc mnafanya nini na dola za watu.

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Wandugu.

Nimezunguka kwa wateja wangu kama watatu hivi ninaowafanyia consultation ya Forex Risk Management na nimebaini Bank ya NBC Inawafanyia kitu mbaya sana wateja wake kwenye malipo ya Dolali wanazofanya.

Malipo kwa Mfumo wa TISS yanapaswa kumfikia mlipwaji siku hiyo hiyo, na hii ni kwa Mujibu wa Press Release iliyotolewa na BOT tarehe 15/03/2010.

Kwa uzoefu, malipo haya huwa hayawafikii walipwaji siku hiyo hiyo karibia kwa bank zote lakini huwafikia ndani ya masaa yasiyozidi ishirini na nne kama ikishindikana, hata NBC naamini wanafanya namna hiyo isipokuwa mpaka nilipojionea kitu cha hajabu kidogo, hasa kwenye malipo ya dola sababu nimefuatilia malipo ya shilingi hayana tatizo hata kidogo kwa mujibu wa data nilizotumia kutoka kwa wateja wangu hawa.

Kwa wale wanaotuma Dola ama kupokea transaction hiyo inachukua siku zisizopungua nne, mpaka kumfikia mteja, na chanzo cha tatizo kiko NBC sio the other banker.


Ni Kwanini Mnafanya hivi?

Ni wafanyakazi ndio wanachezea Dola za watu, au Ni Bank imeamua kutumia fursa?
 
Unawafahamu makaburu lakin?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Inamaana kama walishalizwa ndio chanzo cha kuweka hyo delay ya siku4?
 
chezea kabulu wa SA. hd wafanyakaz nao wanajiona wapo SA..

Hii benk ht huduma zao hazna ushindani.. japo ni benk kubwa.
 
chezea kabulu wa SA. hd wafanyakaz nao wanajiona wapo SA..

Hii benk ht huduma zao hazna ushindani.. japo ni benk kubwa.
 
Kwa mwanza benki zenye services bora kwa sasa ni Exim,Standard Chartered na Bank M na wasipoangalia Bank M na Exim zitakuja kutisha sana
 
Back
Top Bottom