Kwa muda mrefu saana ndani ya Atm ya Nbc Tazara hakuna taa. Wahusika wako wapi? Meneja wa tawi anafanya nini?
Haifai unaenda Atm unakuta giza totoro mpaka uwashe simu yako ndio uweze kuona namba kwenye atm. Haya ni maeneo mabaya kwa uhalifu nyakati za usiku. Mhalifu anaweza akaja kukukaba mle mle ndani ya Atm na mtu asijue ukizingatia polisi wanakaa upande mwengine kabisa na ziliko Atm.
Nbc mrekebishe hii hali.
Mi na kamchina kangu wala spati shida..nawasha katochi simu naing'ata mdomoni namulika kwenye keyboard mambo mswaaano kabisa..poleni wenye magalaxy..
Ukiona giza na unaogopa kukabwa,achana napo nenda ATM nyingine,
kwani si wanaona nakuelewa hali iliyopo?!!! Nafikiri wanasubiri adhma yao itimie ndipo wata weka hizo taa.
Hii ndiyo Tanzania,tuna jifunza baada ya matatizo.
Wanaweza wakakuachia kamchina kako halafu wakachukua mpunga uliotoa !Mi na kamchina kangu wala spati shida..nawasha katochi simu naing'ata mdomoni namulika kwenye keyboard mambo mswaaano kabisa..poleni wenye magalaxy..