Nay wa Mitego aitabiria kifo bongo fleva

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,505

Msanii Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa ndani ya miaka miwili au mitatu inayokuja anaona wazi muziki wa bongo fleva unakwenda kufa kama ambavyo tasnia ya filamu bongo ilivyokufa kwa kile anachodai wasanii wamekuwa wazembe na kutegemea kiki.

Nay wa Mitego amesema kuwa wasanii wengi wa bongo saizi wanategemea zaidi kiki kuliko kufanya muziki mzuri jambo ambalo anaona litafanya muziki wa bongo kufa muda si mrefu kama wasanii hao hawatachukua jukumu la kurudisha muziki kwenye mstari.

"Kusema kweli kuna kitu nakiona kwenye muziki wetu wa bongo fleva tunakibarua kikubwa cha kurudisha muziki kwenye mstari sababu saizi watu wanatengeneza kiki kubwa ila muziki mdogo, yaani kiki zimekuwa mbele muziki unasindikiza kiki miaka miwili mitatu ijayo naiona bongo fleva ikiwa imepotea kama bongo movie ambavyo imepotea kama tusipokuwa makini kuamua kufanya kazi kweli na kiki ziwe tu kusindikiza muziki, saizi watu wanatengeneza kiki hata hazielezeki wasanii tunajisahau tuamke, turudishe muziki wetu kwa sababu tunawalemaza hata mashabiki" alisema Nay wa Mitego


Muungwana
 
Mbona yeye mwenyewe anapenda 'kiki'...??.Lingine kitakachoua game ya bongo fleva ni ubunifu hakuna ....ubunifu ni tatizo kubwa kwa wasanii wa bongo....mmoja akifanya trap beat wote watafuata...mmoja akifanya reggae au dancehall wote watafuata eti ndo trendy hakuna trendy kwenye mziki wafanye mziki mzuri tu......!
 
Bora hata wewe ilieamua kujenga Kanisa lako utabaki salama, mana biashara ya kanisa inalipa ile kinyama chalii.
 
Mashabiki wenyewe ndo wanaoua muziki mzur sababu yakushabikia mambo ya timu timu sababu wasanii wanajitahid kutoa nyimbo nzur lkn kwakua hatoki upande wa timu yoyoye mashabiki haupi promo kiivyo lkn akitoa upande mmoja wa mwenye timu yake huo wimbo utapigwa sehem zote hata kama cyo mzur sana sisi kama shabik tunawavunja ngumu wasanii wengne kinachobak inabid watafute kiki ya lazima ..
 
Ukiongelea Bongo Movie kufa, mbona aijawahi kuwa hai. Lini? Au Kibisa cha Kanumba na Ray Kigosi ndio mnaita movie?
 
Kama bongo flava ikifa yeye ndio atakua mmoja kati ya wapuuzi waliharibu bongo flava yetu
 
Back
Top Bottom