Mkuu Pole Sana unachotaka kufanya ni idea nzuri ila am sure hutofanikiwa unachotaka kwa kutumia Dynamo ya baiskeli kwani zinatoa volt 6 kwa 12 na mzunguko wake unatakiwa uwe constant upate voltage zilizotulia. Unatakiwa uwe mzuri kwa hesabu ili usipoteze muda mwingi kwenye utafiti.
Lengo lako kama nilivyokuelewa ni Unataka Umeme wenye mzunguko wake wenyewe yaani free energy.
Tafiti Nyingi sana zinafanyika kuweza kupata free energy na katika zote zilizofanikiwa ya kwanza ni Umeme wa Maji ambao una gharama kubwa kuunda na una gharama kwenye service japo si kubwa kivile kwani faida yake ni kubwa.
Umeme wa bure mwingine ni wa Upepo ambao ndio kama wewe uutakao kwa maelezo yako. nao unahitaji eneo maalum lenye upepo wa muda wote... Tayari unatumika maeneo mengi Duniani.
Umeme mwingine free energy ni wa Solar power umeme jua huu gharama yake nayo ni kubwa sana upande wa vifaa vyake haswa panel na Battery zake. umeme huu wote wa Jua,Maji na Upepo ni bora na Rafiki wa mazingira na wote unatumia nguvu za asili kujiendesha upange wa power.
Kuna Umeme wa Gas za asili na za kutengeneza kama za Takataka n.k am sure wewe huitaji haya Twende kwenye nia yako
Dynamo unaweza tengeneza mwenyewe au zilizo tayari maana ni mfumo wa mzunguko wa Nyaya kwenye sumaku tu unapata umeme shida ni kuupatia ukae sawa.
Mimi nimekuwa nadadisi sana aina ya kuweza kuwa na free Energy ila Shughuli za kibinadamu zinanirudisha Nyuma.
Kama unaishi kwenye vyanzo vya Umeme kama nilivyoeleza hapo juu chagua kimoja uanze majaribio am sure utafanikiwa kama una nia.
kama upo karibu na mto ambao una maji yanayotembea utaweza pata umeme wa bure. na kama unaishi sehemu yenye upepo mkali pia utaweza pata umeme wa bure, Umeme wa Jua nao pia unaweza tengeneza panel zako au kununua panel tu utapata free energy.
Unahitaji vitu kadhaa kama Gundi,bati,Dynamo,Chain, sprocket kubwa na ndogo,bearing, bolti na nati wire battery voltage control, Battery charger n.k hadi ufanikishe zoezi.
Utengeneze bati kama pangaboi la kuchota upepo na hilo pangaboi una liset liweze zunguka pande zote ili upopo wa kusini ukisimama basi lizungushwa na upepo wa kaskazini,mashariki na Magharibi... pata picha hapo.
Pangaboi linapozunguka kuwe na hesabu za uwezo wa kuzungusha hiyo Dynamo na voltage unayoihitaji kwa kazi unayoitaka kutumika. uunganishe sprocket sambamba na pangaboi linapozunguka either liwe na excel au mbananisho na sprocket nyingine inapokea chain na kuleta mzunguko ambao unaweza unganisha dynamo yako izunguke ili upate umeme utakao charge battery yako or direct power. Pia kuna Pangaboi unaweza iset sambamba na pangaboi ikazungushwa hapo hapo. wewe ukashusha wire tu zipeleke umeme kwenye battery ichajiwe. Aina ya Wind power ndio hutumika hivyo.
Kuna Umeme unaojiendesha wenyewe kwa kutumia Sumaku huo ukifanikiwa ndio utasaidia mno kupata umeme wa bure
Yaani zile sumaku huwa ukizisogeza karibu zinakumbiana na kuna pande zake ukizisogeza zinashikana sas hapo kuna hesabu zake watu wamefanya zinaleta mzunguko basi majaribio yaliweza kutengeneza umeme ila ndio wanaendelea na research kuweza pata free energy kwa kutumia Sumaku.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.