Nawezaje kutatua tatizo la kupata choo kwa mtoto mchanga wa miezi sita

Joachimb

Member
Jul 23, 2017
62
63
Kuna ishu inanisumbua hapa,mwanangu anapata shida ya kunya , akitoa choo kinatoka kigumu sana kinamuumiza analia na wakati mwingine kinatoka na damu, pia anakula ila anaweza kupata choo baada ya siku sita na ni kigumu anapiga kelele sana.

Kuna dawa gani inaweza kumsaidia au naweza kufanyaje akawa anapata choo ya kawaida bila kuumia na maji anakunywa pia lakini choo bado ni ngumu na inamuumiza sana.

Naomba msaada wa kitabibu tafadhali.
 
TATIZO LA KUKOSA CHOO KWA WATOTO WACHANGA


kukosa choo watoto.jpg


Mzazi yeyote furaha yake ni kuona mtoto wake ana furaha na anapata kila anachotakiwa kupata kama mtoto.

Kukosa choo kwa watoto wachanga ni swali ambao huwapa wamama wengi maswali na hofu .

Kukosa choo kwa mtoto mchanga hasa anayenyonya maziwa ya mama tuu ni kitu cha kawaida wala mzaz hutakiw kupata wasiwasi .

Mtoto anayenyonya maziwa ya mama anaweza kukosa choo mpaka week au zaid hasa baada ya week ya 4 mara baada ya kuzaliwa .

Hii ni kwasababu maziwa ya mama ni maziwa mtoto anayohitaji hivyo kuna muda yanatumika yote kwa ajil ya ukuaji wa mtoto na kubaki kidogo sana kwa mtoto kutoa kama haja kubwa.

Sikuzote hajakubwa huwa ni chakula ambacho mwil haukihitaji ndio hutolewa kama haja kubwa.

Mtoto anayenyonya maziwa ya mama tuu huwa hapati constipation ,

Kupata choo kwa mtoto anayenyonya maziwa ya mama tuu hutegemea mtoto na mtoto kuna kuna wanaopata haja kubwa kila baada ya mlo ,

Wengine mara moja kwa siku na wengine mara moja kwa week .

Mara nying mtoto hupata shida ya kukosa choo pale unapoanza kumpa kitu kingine zaid ya maziwa ya mama.

Swali jingine ambalo wamama wengi huwa na wasiwasi ni pale mtoto anapojikamua wakati anapata haja kubwa na watoto wengine hulia kabisa ,

Wengi huzan kuwa watoto wao wamekuwaconstipated,

Kama mama mtoto wako ananyonya maziwa yako tuu na ukaona hii hali hutakiw kuwa na mawazo hii ni kwasababu misuli ya njia ya haja kubwa ya mtoto hairelax au kujiachia kwa muda ule mtoto anaotaka toa haja kubwa kwa hiyo mtoto inabid asukume kwa nguvu kwa kutumia misuli ya tumbo na hufanya hiv mara nying mpaka atakapofanikiwa toa hiyo haja kubwa.

MAMBO YA KUFANYA KUMSAIDIA MTOTO AMBAYE AJAPATA CHOO MUDA MREFU

Mama jitahid kula vyakula vya maji maji .

Massage tumbo la mtoto kwa mafuta au maji ya vuguvugu.

Mfanyishe mtoto mazoez ya kuendesha baiskeli.

Muweke kwenye maji ya vuguvugu muda anaojikamua anapotaka pata haja kubwa.

Ukipitia post za nyuma nimeelezea zaid tatizo la mtoto kukosa choo hasa baada ya kuanza pewa vitu vingine.
 
Kuna ishu inanisumbua hapa,mwanangu anapata shida ya kunya , akitoa choo kinatoka kigumu sana kinamuumiza analia na wakati mwingine kinatoka na damu, pia anakula ila anaweza kupata choo baada ya siku sita na ni kigumu anapiga kelele sana...
Bila shaka umepata muongozo
 
Nimetafuta post zako za nyuma kuhusu mtoto aliyeanza kula vyakula vingine nimeikosa, naomba unitag kama hutojali mkuu.
Mtoto miezi 6 mpaka 12

Mpaka wa 6, mtoto anaweza kulala muda wa masaa 3 wakati wa mchana na kulala zaidi ya masaa 9 hadi 11 wakati wa usiku. Katika umri huu, unaweza kumuacha alie usiku, hii ni kwa watoto wachanga ambao huamka na kulia wakati wa usiku.

Wazazi wanaweza kuwapatia watoto muda kidogo watulie na kujirudisha kulala wao wenyewe bila kubembelezwa. Kama huwezi kumwacha mwanao akilia basi mbembeleze bila kumbeba kwa kumuongelesha akiwa kitandani huku unamsugua (rub) mgongoni kidogokidogo, alafu muache uondoke akijua kwamba anatakiwa kurudi kulala - isipokuwa kama anonekana kuwa mgonjwa. Watoto wagonjwa wana haja ya kubebwa na kutunzwa. Kama mtoto wako haionekani mgonjwa na anaendelea kulia, unaweza kusubiri kwa muda mrefu kidogo, kisha rudia tena kumwacha ajibembeleze yeye mwenyewe atakapolia tena.

Kati ya miezi 6 na 12, wasiwasi wa kutengana toka kwa mama humpata mtoto, hii ni kawaida na ni sehemu ya ukuaji ya mtoto. Sheria ni ileile, jaribu kutombeba mtoto wako, kutomwashia taa, kutomwimbia, kutomwongelesha, kutocheza nae, au kulisha mtoto wako wakati anatakiwa alale. Hizi zote hazitamruhusu mtoto wako kujifunza kulala mwenyewe na ataendelea kuamka usiku.

Watoto chini ya miaka 3

Kuanzia mwaka 1 hadi 3, wengi wachanga kulala masaa 10 hadi 13. Kujitenga wasiwasi, au tu hamu ya kuwa pembeni na mama na baba (ili asimiss kitu), inaweza kuwahamasisha mtoto kukaa macho.

Wazazi wakati mwingine kufanya makosa ya kufikiri kwamba kumwacha mtoto asilale mapema kutamfanya mtoto alale zaidi usiku. Kiukweli, ingawa, watoto wanaweza kuwa na wakati mgumu kulala kama wamechoka sana. Ingawa watoto hulala kidogo mchana, usimlazimishe alale mchana kama hataki, lakini ni muhimu kuwa na ratiba ya muda wa utulivu kwa mtoto, akae chumbani kwa mda hata kama kataki kulala mchana.

Kuanzisha utaratibu wa kwenda kulala husaidia watoto kupumzika na kuwa tayari kwa ajili ya usingizi. Kwa mtoto, utaratibu unaweza kuwa toka dakika 15 hadi 30 na ni pamoja na shughuli za kutulia kama vile kusoma hadithi, kuoga, na kusikiliza muziki laini.

Chochote utakachofanya, mwanao anatakiwa ajue ni usiku na anatakiwa alale, usibadilishe mpangilio ulouweka kila siku kabla ya kulala. Kila inapowezekana, mruhusu mwanao achague nini anataka usiku huo, yaani kama ni hadithi, ama kuimbiwa, nguo gani ya kulalia anataka, toy ipi ya kulala nayo anataka, nyimbo iipi, hadithi ipi n,k ilimradi bado mtafuata mpangilio uleule kila siku. Hii inamfanya anaona ana udhibiti kwenye huu mpangilio.

Lakini hata mtoto mlalaji huwa anaamka mara moja moja. Kuota meno kunaweza kumuamsha pia ndoto. Ndoto huanza katika umri huu, na kwa watoto wadogo, ndoto inaweza kuwa ni kutisha. Jinamizi ni hasa inatisha kwa watoto, ambao hawawezi kutofautisha mawazo na ukweli. (Basi kuwa makini kuchagua programu gani mwanao anaangalia kabla ya kwenda kulala)

Kuwafariji na kushikilia mtoto wako kwa nyakati hizi. Kuwa na majadiliano juu ya ndoto kama yeye anataka, na kukaa hadi mtoto wako ni atulie. Kisha muhimize mtoto wako arudi kulala mapema iwezekanavyo.
 
LISHE YA MTOTO WA MIEZI 6-12

Kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:

Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.

Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako.

Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti.

Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu.

Wakati gani Uanze Vyakula Vingine

Mtoto wako akifikisha miezi 6 unaweza kuanza kumpatia vyakula vingine kidogo kidogo ( Kuna ambao kutokana na sababu Fulani daktari huwashauri kuanza mtoto akiwa na miezi 4 hivyo ni vyema ukiwasiliana na daktari wako kwanza). Mtoto akianza kupewa vyakula nje ya maziwa mapema kabla ya miezi 4 ni hatari kwa afya yake maana mfumo wake wa kusaga chakula unakuwa bado haujawa tayari. Unapoanza kumpa vyakula vingine hauachi kumnyonyesha, unyonyeshaji unaendelea hadi miaka miwili na nusu.

Dalili kuwa mtoto wako yupo tayari kuanza vyakula vingine ni:

Amefikisha miezi 6

Anaweza kushikilia kichwa juu ( shingo imekaza)

Anaweza kukaa kwa kuwekewa kitu ( mfano kiti chenye mkanda)

Unapompa chakula na kijiko anafungua mdomo kutaka kupokea au anageuza uso kwa kukataa

Akipokea chakula anakiweka mdomoni na kujaribu kumeza na sio kukisukuma nje na kuacha mdomo wazi.

Hakikisha mtoto wako yupo tayari kabla hujaanza kumpa chakula na usimlazimishe sana anapoanza maana anaweza kuchukia chakula, inawezekana hapendi chakula ulichompa jaribu kubadilisha uone anapenda nini. Kila mtoto ni tofauti na mwingine hivyo usimlinganishe mtoto wako na mwingine la muhimu ni kuhakikisha kuwa anauzito kulingana na umri wake na anaongezeka kwa kupanda chati.

Mnapokuwa mnakula mezani mtoto naye awe hapo ili kumpa hamu ya kula na sio kila wakati akila anakuwa peke yake. Mpe chakula akiwa na furaha na pia akiwa na njaa ili aweze kufurahia chakula chake. Kabla ya kubadilisha aina ya chakula mpe kwa siku 3-4 mfululizo ili aweze kukizoea na kama kitamletea madhara ujue hasa ni chakula gani. Usimchanganyie vyakula maana hutajua anapenda nini na kuchukia nini na pia kama kuna kitu kitamdhuru ukichanganya hautagundua kwa urahisi.

Miezi 6-9

Endelea kunyonyesha na anza kumpa vyakula vyenye madini ya chuma. Mtoto alishwe kwa ratiba inayoeleweka kila siku na katika ratiba hiyo hakikisha angalau mara moja kwa siku muda wake wa kula unakuwa sawa na muda wa familia yote ili muweze kula pamoja. Vyakula vyake viwe vimepondwapondwa kabisa ikiwezekana tumia blender na hakikisha anapata mlo kamili yani matunda, mbogamboga, mbegu, nafaka, nyama na samaki. Inashauriwa kutokuchanganya aina tofauti za nafaka kwenye unga mmoja unapomtengenezea uji, uwe na unga wa mahindi, ulezi,mchele n.k tofauti tofauti. Pika aina moja ya uji kwa wakati unaweza kufanya kwa wiki au vyovyote utakavyopenda.

Unapompa mboga au matunda anza na tunda moja moja kwa wakati. Osha vizuri matunda yako na katakata vizuri na kuponda ponda kisha mpe kiasi kidogo kwa wakati na kikibaki usikiweke, mtengenezee kile atakachokula tu. Matunda kama papai, parachichi na embe ni mazuri kwa kuanzia. Chemsha maharage, njegere au mboga za majani na kumpa supu kidogo kidogo, usiweke chumvi nyingi kidogo sana inatosha. Usimpe juisi za madukani, hakikisha unamtengenezea juisi wewe mwenyewe na usichanganye matunda mbalimbali kwenye juisi moja, na usiweke sukari kabisa.

Miezi 9-12

Katika umri huu mtoto anakuwa tayari amezoea ladha tofauti tofauti za vyakula mbalimbali nje ya maziwa. Anauwezo wa kukaa na kushikilia kitu kwa mikono yake na kuweka mdomoni hivyo anza kumpa matunda laini mkononi aanze kujifunza kula mwenyewe. Hakikisha vipande sio vidogo sana anavyoweza kumeza ili kuepuka hatari ya kukabwa. Kwa sababu pia atakuwa ameanza kuota meno atakuwa anapenda sana kutafuna tafuna. Katika umri huu pia unaweza kuanza kumpa kiini cha yai, ute wa yai hadi afike umri wa mwaka mmoja. Endelea kumnyonyesha ila kwa sasa anakula kwanza kisha ndio ananyonya maana akinyonya sana anaweza akakataa chakula. Usimpe chakula kimoja mfululizo kwa muda mrefu maana atakinai na kuanza kukataa chakula, mpe vyakula tofauti tofauti ili aendelee kupenda chakula.

Jinsi ya Kutengeneza Chakula cha Mtoto

Ni rahisi sana kutengeneza chakula cha mtoto nyumbani kwako. Osha mikono yako vizuri kabla ya kuandaa chakula na hakikisha unatumia vyombo visafi.

Matunda na mboga mboga: osha mboga zako vizuri kwa maji safi ( ya uvugu vugu) na kisha katakata na kubandika jikoni kwa chumvi kidogo sana bila mafuta. Ikichemka isage kwenye blender au ponda ponda iwe laini kabisa kisha mpe mtoto. Matunda osha pia kwa maji ya uvugu vugu, toa ganda la nje na kata vipande vikubwa kama unataka ale kwa mikono yake mwenyewe au ponda ponda na upe kwa kijiko.

Nyama na Samaki: Chemsha vipande vya nyama na maji kidogo na iive kwa moto wa kiasi hadi ilainike kabisa kisha isage kwenye mashine (food processor) na umpe na ile supu. Samaki vile vile ila samaki hakuna haja ya kuisaga maana ikiiva inalainika sana na ni rahisi kwa mtoto kula bila taabu (Kuwa makini sana na mifupa!).

Mbegu: Hapa nazungumzia maharage, kunde, choroko, njegere n.k Pika hadi ziive kabisa na kulainika kisha pondaponda na kumpa mtoto. Pia viazi na ndizi vinafaa sana kwa watoto, unaweza ukachanganya na supu ya samaki / nyama au na maziwa.

Nafaka: Usichanganye nafaka tofauti tofauti kwa ajili ya uji wa mtoto, inashauriwa kuwa na unga tofauti kwa kila nafaka. Unapopika uji unaweza kuweka karaga zilizosagwa ili kuongeza mafuta na vitamin kwenye lishe ya mtoto.

Usalama katika Kula

Hakikisha haumuachi mtoto mdogo na chakula au kinywaji bila uangalizi hata kama ni maziwa ya chupa asije akapaliwa. Usimpe mtoto chakula au maziwa akiwa amelala, analia au anacheka.

Usimpe chakula ambacho kinaweza kumkaba au kumpalia kama karanga, maindi, zabibu n.k

Kabla ya kumpa mtoto chakula hakikisha umekiangalia joto lake usije ukamuunguza mdomo.

Usafi wa mtayarishaji, mlishaji na mlishwaji ni muhimu san asana.

Mfano wa Ratiba ya Mlo wa Mtoto

Ratiba hii ni ya mfano tu, vyakula vilivyotenganishwa na / inamaana nikimojawapo kati ya hivyo. Hakikisha vyakula havichukui nafasi ya maziwa maana ni ya muhimu kwa afya ya mtoto wako.

MUDA MIEZI 6 – 9 MIEZI 9 – 12

Alfajiri (saa 11-12
) Maziwa ya mama Maziwa ya mama

Asubuhi (saa 1-2) Maziwa ya mamaUji ( Cerelac)

Tunda la kupondwa pondwa

Maziwa ya mamaUji ( Cerelac)

Tunda la kupondwa pondwa

Kabla ya mchana (saa 4-5) Maziwa / Kipande cha mkateMaji Maziwa / andazi / chapatti laini / Kiini cha yaiMaji

Mchana (saa 6-7) Ndizi / Viazi / Wali vya kupondwa pondwaSupu ya mboga ya majani / mbegu / samaki / nyama

Tunda la kupondwa pondwa

Ndizi / Viazi / Wali / UgaliMboga za majani / Nyama / Mbegu / Samaki

Kipande cha Tunda


Alasiri ( Saa 9-10)
Maji Maji

Jioni (saa 12-1) Uji / CerelacSupu ya mboga / mbegu / nyama / samaki Uji / CeleracMboga / Mbegu / Nyama / Samaki

Usiku ( muda wowote) Maziwa, Maziwa.
 
Back
Top Bottom