Nawezaje kupata visa ya masomo kama sina vyeti vya elimu?

Mantheman6

Member
May 30, 2020
41
125
Habari zenu ndugu wana JF poleni na majukumu ya kila siku

Naombeni kufahamishwa ni njia gani naweza kutumia ili nipate visa ya masomo kwa nchi kama Canada, USA, China au Japan maana nimejaribu kufuatilia kwenye tovuti za vyuo inaonekana ili uweze kupata visa ya masomo basi ni lazima uwe na documents zote zakielimu kama o- level certificate na cheti cha diploma ndipo uapply na baada ya chuo kuona unakidhi vigezo ndipo watume taarifa kwenye balozi husika ili uweze kupatiwa

Sasa mimi sina cheti cha diploma ila nina cha form four na nimepanga kwenda kutafuta maisha nje ya nchi je ni njia gani nitumie?
 

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,324
2,000
Sio rahisi kihivyo kwa njia ya elimu iko very clear ata ungekuwa na vyeti bado ungehitaji confirmation letter kutoka chuo cha nje. Pia utahitaji kuwasilisha mfazili wako/scholarship ama bank statement yako ama wazazi ikionesha kwamba wanamudu garama za wewe kusoma nje.

Njia za kwenda ni nyingi ila hakuna njia iliyo rahisi kwa kila mtu kutumia usifemoyo hakuna linaloshindikana penye nia na juhudi.
 

Mantheman6

Member
May 30, 2020
41
125
Sio rahisi kihivyo kwa njia ya elimu iko very clear ata ungekuwa na vyeti bado ungehitaji confirmation letter kutoka chuo cha nje. Pia utahitaji kuwasilisha mfazili wako/scholarship ama bank statement yako ama wazazi ikionesha kwamba wanamudu garama za wewe kusoma nje.

Njia za kwenda ni nyingi ila hakuna njia iliyo rahisi kwa kila mtu kutumia usifemoyo hakuna linaloshindikana penye nia na juhudi.
Nashukuru sasa njia mbadala ni zipi endapo nina ndugu kwenye mataifa kama Japan au Canada na nahitaji niende kumtembelea kisha nizamie mazima?
 

LITA2019

JF-Expert Member
Dec 18, 2019
216
500
Huwez kupata visa ya masomo kama huna admission letter kutoka chuo unachotaka kusoma, kwanza uombe chuo, upate then ndio wanakutumia docs zinazokuwezesha wew kuomba visa ya masomo mkuu. Kama una ndugu anaweza kutumia invitation,ambapo mara nyingi yeye ndio hutakiwa kuweka docs nyingi zakuthibitisha wew kwenda, ukialikwa, nyaraka nyingi zitatakiwa kwa yule anaekualika, ukitoroka unampa msala na yeye, ndio maana hadi wanakukubalia, assessment huwa ya kina sana

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 

Mantheman6

Member
May 30, 2020
41
125
Huwez kupata visa ya masomo kama huna admission letter kutoka chuo unachotaka kusoma, kwanza uombe chuo, upate then ndio wanakutumia docs zinazokuwezesha wew kuomba visa ya masomo mkuu. Kama una ndugu anaweza kutumia invitation,ambapo mara nyingi yeye ndio hutakiwa kuweka docs nyingi zikuthibitisha wew kwenda, ukialikwa, nyaraka nyingi zitatakiwa kwa yule anaekualika, ukitoroka unampa msala na yeye, ndio maana hadi wanakukubalia, assessment huwa ya kina sana

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
Sawa na hii suala la invitation huwa lipo kwa nchi zote au baadhi tu? Kama una ndugu China au Japan anaweza kukualika?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom