KimpaGhasha
JF-Expert Member
- Jun 21, 2020
- 327
- 464
Habari zenu wadau wa JF,
Bila shaka mnaendelea vyema na majukumu ya kila siku kwenye kutafuta riziki. Moja kwa moja niende kwenye hoja husika. Binafsi nilipata changamoto ya ugonjwa wa wasiwasi/ uoga uliopitiliza ambao nilidumu nao kwa miaka mingi takribani 14.
Ni ugonjwa ulionipa wakati mgumu sana hasa kwenye suala zima la kuchangamana na watu. Nilikuwa mwenyewe na nilifanya kila jambo mwenyewe sikuwa na mtu wa karibu hata mmoja.
Kipindi hicho ilikuwa mtu akijipendekeza kuwa karibu na mimi namkwepa mita100; yaani huo mkwepo hatakuwa na hamu tena na mimi.
90% ya muda wangu nilitumia kuwa mwenyewe tu na nikiwa kwenye kundi la watu mzee huniskiii chochote kutoka kwangu. Nilikuwa nikikaa na mtu halafu akaja mtu mwingine najisepesha kiaina yani. Lakini pia nilikuwa msiri kupitiliza aisee hata class yani we uje ujue nimepata maksi ngapi kwenye paper inabidi ufanye kazi ya ziada.
Lakini pia ilikuwa naweza kuingia class asubuhi mpaka tunatoka jioni sijawahi kuongea na yeyote aisee na inaweza kukata tu hata wki mzima.
Yaani ni mengi mnoo aisee lakini kubwa zaidi ni kwamba nimejitahidi kujinasua kwa namna fulani kwenye hiyo na bila shaka kwa asilimia nyingi nimefanikiwa sana.
Kwahiyo sasa hivi napata hamu na ari ya kutengeneza ukaribu na watu hasa niwe na marafiki wa karibu maana saivi naona umuhimu wa kufanya hivyo.
Wadau ambao wanaweza kunipa mbinu za kufanikisha hili naomba mnisaidie tafadhali.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu
AHSANTEENI