Nawezaje kumsaidia huyu binti aachane/apunguze na haya?

Shozylin

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
297
607
Wakuu kwema.

Moja kwa moja kwenye mada. Nina mdogo wangu 20-24 yrs, mtoto wa mama angu mdogo. huyu dogo kamaliza Chuo cha Kati huko mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Wakati yupo huko kadanganya wazazi kwa visa mara vya kupoteza laptop, maa kuibiwa simu nia yake ilikua ni kuwapiga mzinga wazazi wake tu. Bahati nzuri ananiamini mimi. Mimi ni kaka yake na ni rafiki yake pia, nikimaanisha huwa ananichana ukweli na kunisihi nisiseme ukweli huo kwa maza.

Kamvuta baba yake zaid ya 600,000 na mimi juzi kama wiki moja nimekaa kwao nimeona hali halisi ya uchumi wao, mzee kwa sasa hana hela na analalamika mtoto wake kumzidishia matumizi.

Kamaliza chuo karudi nyumbani, jana kaaga kuwa anakuja home kwetu kwa mama yake mkubwa, lakini kumbe kuja kwetu ni gia tu ya kwenda kwenye mambo yake. Bahati mbaya wazazi wake walimruhusu kwakua wanajua anakokwenda ni sehemu salama.

Dogo kafika home kakaa kama masaa mawili ya kuzuga kisha akamuaga mama yangu kuwa kuna mkaka kaongea naye amtafufie kazi kwaiyo ndiyo anataka akamuone, mama kamruhusu dogo katoka nyumbani mchana karudi usiku saa 7.

Siku ya leo dogo kaaga kwamba anakuja kwangu kunitembelea maza kamruhusu dogo kaja, kwakuwa mimi ni kaka yake na rafiki yake akanambia alikokuwa kaenda jana.

Dogo alikwenda kwa mshikaji wake mpya anafanya kazi kitengo flan T@. Wakati huo ana bwana wake wa kitambo alinambia ndiyo atamuoa na mimi nilimchukulia kama shemeji.

Sasa ajabu wakati yupo kwangu kapigiwa simu na rafiki yake wakaanza kupeana umbea wa wanayo yafanya. Dogo kamwambia alivyo hongwa, mara wanasimuliana mabwana zao mara huyu mara yule, mara huyu hawezi mara yule hanipi pesa.

Tukapiga story za maisha nijue plan zake, maana before niliongea na baba yake akanambia plan anazo kusudia kwa dogo punde tu atakapo rejea home. Nia yangu ni kutaka oanisha plan za dogo na za mzee.

Baadae nikamuuliza kuhusu shemej yangu alie nambiaga kuwa ataolewa nae, anadai kamtema kwakua hampi pesa za kutosha.

Nikamuuliza kwaiyo kipaumbele chao ni pesa? Mara ooh hamna.

Kiukweli sina ubavu wa kuonya kwa anayo yafanya kwakua si dada angu tumbo moja lakini natamani japo nitumie lugha flani ya kumshauri isiyo haribu urafiki wangu mm na yeye.

Namuonea huruma dogo, sjui kama anatambua kama anayo yafanya asipo kua makini yanaweza kuharibia kesho yake. Bahati mbaya wazazi wake pia age imeenda hawana nguvu ya maonyo na makanyo maana tayari uzee umewakamata.

Na mimi ni kaka yake wa karibu wadau ni fanyaje ili huyu dogo nimtoe huko alikopotelea.?
 
Kaka ... Kikubwa unacho weza kufanya nikuwa wazi usifumbie macho ilo swala

Kuhusu ukarbu wako na yeye lazma uteteleki haswa atapojua wamuingilia Mambo yake..

Kama unaweza zungumza na wazaz wake waelezee ukwel bint yao anapotea watajua lakufanya

ukiona hilo halitoshi kae na uyo binti uone changamoto za malezi ... Ki uhalisia utatumia nguvu kubwa kumuelekeze Ni ipi njia salama ikiwa umri wake na dam bado Ina changamka....

Tumia busara maana si kila apoteaye anapotea wengine wanapitia funzo flani.
 
Naomba namba zake nimuonye Kiutu uzima.
Mm ni mstaafu lakini bado ninaweza kukanya mtu yeyote.
Narudia tena tuma namba tumkanye huyo binti.
 
Wewe ni kijana wa ovyo yaani mdogo wako unashindwa kukaa naye na kumkanya

Waite wazazi wake ongea nao kuhusu tabia za binti yao. Mkae chini mumkanye

Kakija kutiwa mimba au kakapata magonjwa ya zinaa ni hasara kwa familia yenu
 
Kaka ... Kikubwa unacho weza kufanya nikuwa wazi usifumbie macho ilo swala

Kuhusu ukarbu wako na yeye lazma uteteleki haswa atapojua wamuingilia Mambo yake..

Kama unaweza zungumza na wazaz wake waelezee ukwel bint yao anapotea watajua lakufanya

ukiona hilo halitoshi kae na uyo binti uone changamoto za malezi ... Ki uhalisia utatumia nguvu kubwa kumuelekeze Ni ipi njia salama ikiwa umri wake na dam bado Ina changamka....

Tumia busara maana si kila apoteaye anapotea wengine wanapitia funzo flani.
Sawa mkuu, nawaza kila nitakapo ongea nae niwe nampa ushauri juu ya mstakabari wa maisha yake.
 
Nakuona kabisa ukiingia kwenye lawama kwasababu uliaminika na wazazi wake tena umekua kisingizio chake kikubwa.

Acha unafiki kua muwaz kwa wazai wa binti pia kua muwazi kwa uyo bint. Kama kwel unamhurumia basi utajali future yake kuliko urafiki wenu.

Njia prkee ya kumuokoa mtu kama uyo ni ukweli unaofuatiwa na ushauri usimfumbe usimpapase mkamate kabisa.

Bint hana huruma kama anadanga mpaka na t@ kuna haja gani tena ya kuwapiga mizinga wazee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom