Naweza toboa maisha kwa kutoa taarifa ya uwepo wa madini sehemu fulani?

Nguva Jike

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
853
1,005
Habari wana Jf.

Nimepewa taarifa na mzee Fulani aliyekuwa rafiki yangu sana zihusuzo upatikanaji wa madini katika eneo Fulani.

Nilithibitisha taarifa zake.Tatizo sijui nianzie wapi.Je nitafaidika na Kwa nani?
 
Halafu mnasema tumelaaniwa na nani.

Kweli unataka kutangaza siri?

Mali yetu hiyo hata wazungu wakipata madini mahali utasikia wanajenga kanisa au kusaidia Yatima ili mradi waibe

Wewe Jenga vibanda fuga kuku na mifugo anza kunyonya taratibu ukitaka mashine na vifaa vya kuangalia madini gold detectors au vyote wee uliza tu humu

Ila kama ni mzalendo peleka habari kwa wahusika ila akipewa muwekezaji uombe kazi ya ulinzi tena kama una uwezo wa security company sawa.

Maana utatimuliwa kama Paka
 
Usijekuta ni Yale madini kama ya wajeda wetu waliyakusanya kutoka congo (Zaire)walipokuwa wanalinda amani wakarudi nayo kwenye ndege wakawa wanaimba kwa furaha wametajirika. Walipofika bongo kwenda kuyauza wakaambiwa kilo elfu hamsini wakachoka.
 
Acha ujinga kama una uhakika eneo Hilo Lina madini nenda kajenge hata kakibanda fuga huku ukiwaliatiming tu wakigundua unasema eneo ka kwako muingie mkataba wa kamisheni

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
FUATA USHAURI HUU.
1. Chukua coordinates za eneo husika kisha peleka katika ofisi za mkoa za madini kwa ajili ya search and verification za umiliki.
2. Kama eneo lipo wazi utajulishwa ili masuala mengine ya leseni yaendelee.
3. Ukipata tu leseni yako mkononi ndio umemaliza na safari ya kuelekea mema inaanza.

Endapo haumudu gharama za kipengele 1 na 2 hapo juu, ni wakati wa kutumia akili na kutafuta mtu mwaminifu ambaye atatoa mchango wa fedha kwa ajili ya kudhamini mchakato huo kisha mkagawana umiliki(hisa) katika eneo husika.

Baada ya kumpata mbia huyo katika kufashili mchakato wa uchukuaji wa hiyo leseni utafuatia mchakato wa vibali vinginevyo kama vile barua amaa makubaliano na waliokua wamiliki wa ardhi kabla ya wewe kugundua madini iwe ni mtu binafsi ama kijiji, ripoti ya utunzaji wa mazingira, riport ya namna jamii itakavyonufaika, na mengineyo mengi.
Ukiisha kamilisha yote hayo ndipo uchimbaji uanze.

Endapo hauna mtaji wa kufanya uchimbaji basi hapo napo utahitaji ama mtahitaji kupata mbia ama mdhamini ambao mara nyingi mnagawana hisa katika uzalishaji wa mgodi husika ama akawa ndiye mnunuzi wa madini yanayozalishwa.

Hapa katika kupata mfadhili ama mbia wa uzalishaji huwa pako technical sana kwa masuala ya kiinjinia na kisheria, hakikisha unapata muongozo sahihi juu ya mikataba ya namna hii ili kuhakikisha wewe, mfadhili na nchi kila upande unanufaika na mali hiyo.

KUMBUKA:
Madini yote ardhini ni mali ya serikali na utaratibu wa utoaji wa leseni katika eneo husika itategemeana na atakayewahi kupeleka coordinates za eneo husika serikalini, kwa hiyo ikitokea umewahiwa ujue ndio imekula kwako.

Kila la kheri mkuu.
 
Nashukuru sana Kwa ushauri wako wa kina
FUATA USHAURI HUU.
1. Chukua coordinates za eneo husika kisha peleka katika ofisi za mkoa za madini kwa ajili ya search and verification za umiliki.
2. Kama eneo lipo wazi utajulishwa ili masuala mengine ya leseni yaendelee.
3. Ukipata tu leseni yako mkononi ndio umemaliza na safari ya kuelekea mema inaanza.

Endapo haumudu gharama za kipengele 1 na 2 hapo juu, ni wakati wa kutumia akili na kutafuta mtu mwaminifu ambaye atatoa mchango wa fedha kwa ajili ya kudhamini mchakato huo kisha mkagawana umiliki(hisa) katika eneo husika.

Baada ya kumpata mbia huyo katika kufashili mchakato wa uchukuaji wa hiyo leseni utafuatia mchakato wa vibali vinginevyo kama vile barua amaa makubaliano na waliokua wamiliki wa ardhi kabla ya wewe kugundua madini iwe ni mtu binafsi ama kijiji, ripoti ya utunzaji wa mazingira, riport ya namna jamii itakavyonufaika, na mengineyo mengi.
Ukiisha kamilisha yote hayo ndipo uchimbaji uanze.

Endapo hauna mtaji wa kufanya uchimbaji basi hapo napo utahitaji ama mtahitaji kupata mbia ama mdhamini ambao mara nyingi mnagawana hisa katika uzalishaji wa mgodi husika ama akawa ndiye mnunuzi wa madini yanayozalishwa.

Hapa katika kupata mfadhili ama mbia wa uzalishaji huwa pako technical sana kwa masuala ya kiinjinia na kisheria, hakikisha unapata muongozo sahihi juu ya mikataba ya namna hii ili kuhakikisha wewe, mfadhili na nchi kila upande unanufaika na mali hiyo.

KUMBUKA:
Madini yote ardhini ni mali ya serikali na utaratibu wa utoaji wa leseni katika eneo husika itategemeana na atakayewahi kupeleka coordinates za eneo husika serikalini, kwa hiyo ikitokea umewahiwa ujue ndio imekula kwako.

Kila la kheri mkuu.
 
Usijekuta ni Yale madini kama ya wajeda wetu waliyakusanya kutoka congo (Zaire)walipokuwa wanalinda amani wakarudi nayo kwenye ndege wakawa wanaimba kwa furaha wametajirika. Walipofika bongo kwenda kuyauza wakaambiwa kilo elfu hamsini wakachoka.

embu ielezee kwa undani hiiilikuwaje kuwaje??
 
Mzee mjanja anataka kuuza eneo..amalizie uzee wake kiulain hamna madini hapo ametumia nn kugundua kuna madini. .na je ni madini aina gani uskute niya tiles au madini ya chuma
 
Back
Top Bottom