Naweza kusomea nini baada ya kusoma CBG?

tupe source, taarifa umepata wapi? nachojua mimi ni kwamba assistant medical officer (AMO) ndo hiko cheo kimefutwa kqa msaad zaidi google au angalia website ya wizara ya afya
AMO imefutwa lini ikiwa watu wanaomba
 
iyo agronomy inahusu nn na ajira zake

Agronomy inahusu masuala mazima ya sayansi ya udongo, mbolea na vipando (mbegu na mengineyo). Kuhusu ajira zake unaweza ukaelewa kutokana na nilivyoeleza kwamba kozi inahusu nini.
 
Soma Pharmacology...hutojuta. Mi nilipiga science O - Level then EGM....if i had a second chance ningepiga CBG then medicine.

Ila yote maisha tu.
 
Nashawishika kukushauri sababu nilisoma CBG pia late 1990's (ni muda kiasi sasa na ushauri wangu waweza kukosa dondoo za hali za sasa).

CBG ni combination nzuri sana. Ipo katikati ya science na arts/social science. Ukifaulu vizuri waweza jiunga na coz nyingi tu vyuo vikuu.

Mimi nilisoma BScwGY (Geoloy/Geography double major...unatunukiwa ugeologist). Waweza kusoma pia coz kadhaa pale idara ya botany (udsm), hata BSc .wildlife unachukuliwa. Ipo BSc. General Science (sijui kama bado ipo), Environmental Science, etc, etc. Nyingi tu ilimradi ufaulu vizuri.

Mifano yote hapo juu ni kwa udsm bado kuna vyuo kama SUA wana kozi kadhaa za kilimo na mifugo unaweza dahiliwa.

Kipindi fulani ungeweza kusoma Medicines KCMC ila sasa sijui. Wakati wangu udahili pale ulizingatia ufaulu kwenye Biology na Chemistry. Chaguo ni lako tu.

Ila angalizo (japo ni mapema sana kukushauri hili), mafanikio maishani hayajalishi ulisoma kozi wala chuo gani. Ni namna tu utakavyojiandaa/utakavyoandaliwa kutumia hiyo platform kupambana na maisha. Usisome ili uajiriwe bali uajiri! Kila la heri.
 
Soma Pharmacology...hutojuta. Mi nilipiga science O - Level then EGM....if i had a second chance ningepiga CBG then medicine.

Ila yote maisha tu.

Hakuna degree program inayoitwa PHARMACOLOGY, niamini mimi. Labda kama ulitaka kusema PHARMACEUTICALS au PHARMACY
 
Back
Top Bottom