Nawaza! Uamuzi wa kuruhusu mikutano ya siasa una sababu moja ya msingi, kati ya hizi tatu!

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Udhaifu wa CCM ulipelekea kuweka zuio la mikutano ya vyama pinzani!

Na udhaifu huo huo ndio unaosababisha viongozi hao kuwa wakali dhidi ya ukosoaji na utoaji wa maoni kutoka kwa raia watanzania

CCM wanahofu mikutano na maoni mbalimbali ya watu kwani inaweka uchi udhaifu na uovu wao ambao ni janga kwa Taifa hili. Pia inaamsha watu kutoka katika ujinga wa kisiasa, hivyo kuwapa Ugumu CCM kwenye uchaguzi!

Kama ujuavyo ajenda kuu ya CCM Ni kushinda uchaguzi, na si maendeleo ya Nchi! Hapo kila wanachofanya wanataka wasifiwe ili wapewe kura!

Ikumbukwe mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwa upinzani, kwa kubeba majimbo mengi,
Hivyo upepo ule uliwapa hofu CCM kwa chaguzi zijazo, na ndio maana wakaona waamue kuwapiga pin wanasiasa wapinzani iwe kwa jua au mvua!

Je, hofu yao Sasa imekwisha hata waamue kuwapa Uhuru wapinzani kueneza upupu kwa watanzania dhidi yao?

Je, CCM Ni wema Sasa hata wajiamini?

Jibu Ni HAPANA!
Hofu yao haijaisha na wala hawana wema kwa Watanzania
Yes! Wenyewe wanajua hilo na ndio maana kila kukicha wanajimwagia sifa kwa mambo mengi ya kipuuzi!

CCM wanahofu Sana Sasa juu ya 2025 kuliko kawaida,
Wabunge wengi hawana tumaini la kutoboa 2025
Hali ilivyo mtaani Ni mbaya Sana Sasa kuelekea 2025 kuliko ilivyokuwa msimu wa JK kuelekea 2015

Msimu wa JK kuelekea 2015 ulikuwa na Neema mitaani lakini wapinzani waliula kwa ajenda moja tu ya Ufisadi!
Je, itakuwaje sasa kuelekea 2025 kwa ajenda za Ugumu wa maisha, tozo, mikopo, machinga, ajira, umeme, maji na kifo cha JPM?

Nawaza kuwa uamuzi huu wa CCM umegubikwa na Siri zifuatazo!

1.Huenda Kuna njama za kumuondoa Dkt. SSH asigombee 2025, hivyo kupitisha uamuzi huu ili vuguvugu la kupinga utawala huu litapotikisa Nchi wapate kigezo Cha kumuomba apumzike

2.Huenda Dkt. SSH anataka apumzike 2025, au amehisi kupumzishwa 2025, hivyo ameamua aweke historia yake ya Demokrasia na Katiba mpya!

3.Huenda Kuna msukumo wa kimataifa wa kutaka zuio liondolewe!

Kwa sababu kiongozi huyu hawezi kusimama kwa miguu yake dhidi ya pressure za mataifa ameona Hana namna, au pengine Kuna mchongo wa mkopo some where, na dili linagoma kutiki kwa sababu ya tatizo la zuio la mikutano ya siasa!

Acha tuendelee kuzitazama sarakasi hizi!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Umewaza vyema. Hata mimi nilikuwa nawaza hivi hivi..

Yaani uko mlemle.

Iwapo ataachia..shida iiko hapo ..wa kuchukua kijiti chake ni nani?

Majaliwa?, Mwinyi?.
 
Moja ambalo ni kubwa na umeliacha kwa makusudi au kutokujua ni kwamba Profesa wa siasa za CCM ( Mzee wa Msoga) yawezekana Kesha mshauri Mama awaachie wapinzani mapema waanze kutema upupu wao mapema ili ifikapo 2025 Mama atakaposimama kugombea Urais basi watakuwa hawana jipya!

Mikutano ya Wapinzani itaweza kufunikwa hata na mikutano ya Kingwendu Kingwendulile!

Cheza na Msoga wewe!!
 
Akiminya nongwa, akiruhusu nongwa!
Yote heri lakini.
Mimi na mzee wa ubwabwa tunajiandaa kuja na kishindo cha kauli mbiu ya #Sembe kilo moja, shilingi elfu moja.
Lazima wakae
 
Udhaifu wa CCM ulipelekea kuweka zuio la mikutano ya vyama pinzani!
Na udhaifu huo huo ndio unaosababisha viongozi hao kuwa wakali dhidi ya ukosoaji na utoaji wa maoni kutoka kwa raia watanzania...
Chukulia simple tu mikutano imeruhusiwa na Mhe. Rais, wapinzani wanadi sera na CCM waanike mafanikio ya nchi. Maneno mengi hayana maana yoyote. 🙏🙏🙏
 
Udhaifu wa CCM ulipelekea kuweka zuio la mikutano ya vyama pinzani!
Na udhaifu huo huo ndio unaosababisha viongozi hao kuwa wakali dhidi ya ukosoaji na utoaji wa maoni kutoka kwa raia watanzania...
Namba 3 ni sahihi
 
Wapinzani gani unaowaongelea?!! Hawa waliokuwa wakijiuza kuunga juhudi wakati wa Rais Magufuli!
Tanzania bado hatuna wapinzani Bali kuna wachumia tumbo tu!

Unadhani mtu kujiuza ni kukosa hoja? Sio kila mtu asiye na uwezo wa kuvumilia shuruba hana hoja. Kama kweli CCM ingekuwa na uwezo isingetemea vyombo vya dola, na kuzuia wapinzani wao kuongea.
 
Mh Rais ni jasiri sana kuruhusu mikutano ya kisiasa ambayo iliipa CCM relief kubwa licha ya kuzuiwa kinyume cha katiba!Uamuzi wa mh Rais uheshimiwe na kila mtendaji asiwepo mtu yeyote wa kukwamisha nia njema ya mh Rais ya kukuza demokrasia kwa vitendo.Naomba mtu yeyote atakayekuwa na mawazo ya kihafedhina ya kuzuia mikutano kinyume na kauli ya mh Rais mamlaka inayosimamia imchukulie hatua mara moja.
 
Back
Top Bottom