Nawaza sana, John Bocco anachezeshwa Simba na kuitwa Taifa stars kwa kiwango kipi?

Jibu ni hakuna mchezaji namba sita anayemshinda Nungunungu. Huyo Lwanga ni mirafu tu muda wote.
Nungunungu kazi yake ni kurudisha mpira nyuma au kupiga pasi za juu ambazo hazina madhara, muda wake umeisha, Simba ina kazi kubwa ya kusafisha hawa wazee, waende kula pension sehemu nyingine.
 
Huyo huyo ndio alikuwa top score.

Kama mnataka kumtoa tengenezeni Wafungaji wamzidi.
 
Simba hakuna strikers, wote walikuwa wanabebwa na ubora wa Chama, mwamba wa Lusaka aliisadia Simba kutengeneza nafasi nyingi sana hata angekuwa Sarpong angewika, tulilalamika wakati wa dirisha la usajili walete striker wa ukweli tukaonekani ni haters, acha tufunzwe tu kwa sasa.

Wengine watakuja kusema Mugalu ana ahueni, Mugalu alikuwa anakosa magoli mengi ya wazi tena katika mechi kubwa za CAF, kuna tatizo la usajili Simba.
Yaani hakuna mtu aliyeinyima simba ushindi mwingi kama Mugalu,halafu akawa kipenzi cha Pablo,Pablo ,Motorola na benchi love la ufundi wapishe,scouting team yote ifumuliwe
 
Back
Top Bottom