Edo Kumwembe: Kesi ya Chriss Kope Mutshimba Mugalu ni ngumu, anahitaji kuvumiliwa

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,188
8,215
ALIPOFIKA nchini mtu mmoja wa Simba alininong’oneza kitu kuhusu mshambuliaji anayeitwa Chris Mugalu. Aliniambia; “Mugalu ni mchanganyiko wa John Bocco na Meddie Kagere kwa pamoja”. Hii ilikuwa kauli ya kurahisisha kwa mtu anayetaka kumjua Mugalu.

Niliambiwa kuwa aliyesema hivyo ni kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri ambaye huwa anawasaidia watu wa Simba kuwajua wachezaji waliowahi kucheza soka katika ardhi ya Zambia. Kumbuka kwamba Phiri yupo Zambia kwa sasa.

Mechi zake za kwanza nchini niliamini kilichosemwa. Alifunga mabao maridadi ya mshambuliaji halisi. Ungeweza kuamini kwa urahisi. Nilijua kwamba Simba ilikuwa imepata mtu ambaye anaweza kuwaweka benchi Bocco na Kagere.

Lakini sasa Mugalu huyu sio yule aliyefika nchini. Watu wa Simba wanamzomea. Anapitia wakati mgumu kuliko wakati mwingine wowote ule. Anatia huruma. Hata yeye mwenyewe anaonekana kuchanganyikiwa. Anakosa mabao ya wazi kupitiliza. Pambano la Simba dhidi ya Vita aligeuka kuwa kichekesho uwanjani baada ya kukosa mabao mengi ya wazi kisha akaondolewa.

Nyakati kama hizi kichwa cha Mugalu kinakuwa na mambo mawili. Kwanza kabisa kichwa chake kinakosa kujiamini. Mshambuliaji akikosa mabao ya wazi tena na tena anajikuta haamini tena katika uwezo wake, wakati mwingine anaogopa hata kujaribu kupiga.

Kwa wazungu, mshambuliaji wa aina hii huwa wanapambana na kichwa chake. Wanajaribu kumrudishia uwezo wa kujiamini ndani na nje ya uwanja. Wakati mwingine anapewa hata penalti yoyote inayotokea uwanjani ili mradi afunge kwa urahisi na aweze kujiamini tena.

Lakini kuna jambo jingine. Katika kichwa cha Mugalu kwa sasa anaweza kuwa anaamini kuwa amerogwa. Mara nyingi inatokea kwa wachezaji wa Afrika hasa wale ambao wanafika katika nchi kama Tanzania na kusikia simulizi hizi kutoka kwa mashabiki au wachezaji wakiwa kambini.

Hili la pili siliamini sana ingawa lipo na inasemwa kwamba hata katika vitabu vya dini imeandikwa kwamba uchawi upo. Sisi wengine sio kazi yetu kuamini katika hili, tunachojua ni kwamba ikitokea Mugalu akafunga bao moja tu basi ari ya kujiamini itarudi kwake.

Hauwezi kuwa mchezaji mbovu au mzuri kwa usiku mmoja. Haiwezekani Mugalu niliyemuona mimi katika siku za kwanza ghafla akawa mchezaji mbovu. Kuna washambuliaji walikuja nchini na tukajua kwamba hawana lolote kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho. Mmojawapo ni Yikpe.

Kile kiwango cha Mugalu wakati anafika hakikuwa cha bahati mbaya. Kile ndio kiwango chake halisi. Nadhani hata Simba walitumia pesa nyingi kumnasa baada ya kumchunguza na kujiridhisha kwa kauli ile ile niliyosema hapo juu kwamba “Mugalu ni mchanganyiko wa John Bocco na Meddie Kagere kwa pamoja”.

Kinachotakiwa kwa watu wa Simba kwa sasa ni kuendelea kumjengea imani. Inabidi wamshangilie kwa nguvu kwa namna yoyote ile. Wakati mwingine huwa tunawaua wachezaji wazuri kwa sababu ya kukosa busara. Hii ni kuanzia kwa mashabiki hadi viongozi.

Mchezaji wa aina ya Mugalu ni wa kupewa moyo na sio kuzomewa. Ni mchezaji wa kupigiwa makofi hadi anapokosea. Atakapoona watu wa Simba wamesimama nyuma yake ndipo uwezo wake wa kujiamini utakaporudi.

Vinginevyo kuna minong’ono mingi kwamba huenda Simba ikasaka mshambuliaji mpya. Hauwezi kubadilisha wachezaji kila siku. Hawa washambuliaji huwa wanapitia nyakati hizi na bado huwa wanapewa mikataba mipya. Kitu cha msingi ni kujua tu kwamba mshambuliaji wa aina yake anapokuwa fiti huwa anakuwa ni mchezaji wa aina gani.

Vinginevyo unaweza kujikuta unabadilisha wachezaji kila uchao. Haifai kuwa hivi. Labda kama mchezaji ataendelea kuwa na fomu mbovu kwa misimu miwili unaweza kujikuta katika nafasi ya kuachana naye. Ushauri wangu Simba wasifikirie kuachana na Mugalu kwa haraka haraka. Wafuatilie tu kitu kinachomsibu.

Pale mbele anawapa nguvu kubwa ya umiliki mpira hata kama hafungi. Ukame kama huu alionao huwa wanaupata akina Sergio Aguero, Pierre Emerick Aubameyang, Luis Suarez na washambuliaji wengine mahiri duniani.

Katika usajili wa wachezaji Tanzania nimegundua aina tofauti tofauti za wachezaji. Kuna mchezaji ambaye tangu siku ya kwanza mnahisi kwamba mmepigwa. Huyu ndiye kama Yikpe. Halafu kuna mshambuliaji ambaye anakaa katika uchunguzi zaidi. Huyu ni kama Michael Sarpong.

Kuna mchezaji ambaye anaonyesha makali yake tangu mwanzo lakini ghafla makali yake yanapotea. Huyu ndiye kama Mugalu. Kunakuwa na mambo mengi nyuma yake. lakini pia kuna mshambuliaji ambaye anaanza taratibu lakini baadaye akizoea anakuwa moto. Mfano ni Donald Ngoma.

Ngoma alipokuja Yanga alianza taratibu lakini makali yake yakaimarika kila uchao na baadaye akaibuka kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora nchini. Mwanzoni mashabiki wa Yanga walikuwa wakimfananisha na mshambuliaji wao wa zamani, Idd Mbaga. Baadaye walijikuta wakimuheshimu zaidi.

Hii kesi ya Mugalu ndio ambayo inakuwa ngumu zaidi. Mchezaji anaonyesha makali halafu ghafla anakuwa wa kawaida. Huwa ni kesi ngumu ambayo inawaacha wachambuzi, makocha, viongozi na mashabiki wakiwa hawana majibu ya moja kwa moja.

EDO KUMWEMBE
 
Magalu yeye na kipa anakosa tena mechi mbili muhimu.

Kukosa kwake magoli kama ndo ingekuwa mpaka mwisho wa mechi Simba amefungwa hakika lawama zote zingeenda kwake,ila kwasababu Simba mwisho wa siku inatoka na ushindi lawama zinakuwa 50/50/kama ilivyo sasa.
 
Mugalu Kuna kitu anapitia so bure.

Lakini Kuna goli alikosa akiwa na kipa ,Hilo forward yoyote angeweza kukosa!

Pale kipa wa Vita alipunguza Holi...kimsingi pale ilikuwa no uhodari was kipa!

Alichotakiwa kufanya Mugali ni kumpa aliyekuwa kushoto jwake afunge!

Hii ninkea mujibu uzoefu wangu was soka was darasa la tatu!
 
Naunga mkono hoja . Kwa mtu wa mpira ; anachopitia Mugalu ni vipindi huwakuta wachezaji wote duniani . Tunapaswa kuwa waelewa . Mugalu kwangu bado ni bonge la striker .Amefanya vizuri kwenye mechi nyingi alizocheza kuliko makosa ya kawaida mchezoni aliyofanya kwenye mechi chache . Watu tuwe fair na tumpe heshima na muda .

Atakaa sawa . Simba nguvu moja .
 
Mugalu kiwango chake ndo hicho na atabaki hivyo hivyo.

Nadhani umri umefika maana ni mzito kama jiwe.

Akifika golini anafumba macho kabisa.

Alipasiwa mpira yeye na goli, mita tano, kipa kasimama, Mugalu akapiga nje karibia na kibendela cha kona.

Mugalu anabebwa na mido za Simba, angekuwa Yanga angesha fungashiwa virago.
 
Lakini kuna watu wanasema ni "mshambuliaji mkabaji" na eti anawasumbua mabenki wa Timu pinzani, Sasa sijui kaletwa kuja kukababa? Tukienda na hoja hiyo, kwasasa Mugalu na Nchimbi wanatofautiana kidogo sana, maana hata Nchimbi nae huwa anawasumbua mabenki,ila shida yake ni kufunga tu.
 
Mugalu kiwango chake ndo hicho na atabaki hivyo hivyo.
Nadhani umri umefika maana ni mzito kama jiwe.
Akifika golini anafumba macho kabisa.
Alipasiwa mpira yeye na goli, mita tano, kipa kasimama, Mugalu akapiga nje karibia na kibendela cha kona.
Mugalu anabebwa na mido za Simba, angekuwa Yanga angesha fungashiwa virago.
Mkuu Una kitu na Mugalu labda sie hatukijui? Nadhani ni muda ukaweka wazi sasa, maana imekuwa too much Kwa mwanaume kutwa kumsema mwanaume mwenzio, imekuwa kila thread upite umseme mwanaume mwenzio seriously?

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Penati aliyokosa dhidi ya Prison kuna mshabiki wa Simba alifariki kwa presha.
Goli alilokosa dhidi ya AS Vita lile lililomgonga golikipa mshabiki wa Simba alifariki na presha.
Jumla kapoteza mashabiki wawili wa Simba.
Hatuwezi kumvumilia aendelee kumaliza washabiki wetu. Na hujui mimi nipo karibu vipi nao.
Endelea na mambo yako na uache kumshambukia binafsi mchangiaji.
Sio lazima sote tuwe wa kusifu na kuabudu.
 
Sasa mkuu unadhani kwa kumshambulia hivi ndio atakosa namba? Au atafukuzwa?

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
ALIPOFIKA nchini mtu mmoja wa Simba alininong’oneza kitu kuhusu mshambuliaji anayeitwa Chris Mugalu. Aliniambia; “Mugalu ni mchanganyiko wa John Bocco na Meddie Kagere kwa pamoja”. Hii ilikuwa kauli ya kurahisisha kwa mtu anayetaka kumjua Mugalu...
Wachezaji wa kibongo akili yao yote ipo kwenye kupiga misumari wagen, wakipewa nafasi wanakimbia kimbia like headless chicken, mfano Ajib! Mugalu kutakuwa na kichawi kinachezea miguu isione goli, si bure!
 
Ajirekebishe tu, anaumiza sana mashabiki huku mtaani.
Watu tuna hasira naye sana kuliko anavyofikiri.
Nadhani ujumbe umemfikia.
Sasa kama unahisi ujumbe umemfikia kuna haja gani ya kuendelea kumsema kila Uzi ata kama hujaanzisha wewe, brother kumbuka jamaa hapendi hayo anayopita na kukosa Kwa magoli haimaanishi ni mchezaji mbaya, labda nikukumbushe Tu mwaka huu kwenye ligi zote mchezaji ambae anaongoza Kwa kukosa nafasi za wazi ni Christiano Ronaldo kakosa nafasi 33 za wazi Hadi hivi sasa, kwahiyo nayeye wamuanzishie Uzi afukuzwe au asichezeshwe?

Mpira Yule ndio kazi yake, kumbuka wakati Mugalu anakuja alikua ni striker mwenye converting rate kubwa kuliko striker mwingine yoyote na kocha kumpa nafasi mbele ya kagere na bocco sio kwamba anampendelea Ila ni uwezo wake ambao anauonesha mazoezini na kufata anayoelekezwa na kocha wake hivo nyie mtaendelea kujaza server Tu Ila hambadirishi chochote, ungewekeza nguvu kushauri afanyie kazi finishing yake ungekuwa unamake sense Ila wewe umefanya kama imekuwa bifu sasa

mpira wa kibongo Una mambo mengi, acheni kumpa pressure ambazo hazina maana kama kufa mashabiki wa Simba wanakufa kila siku na sababu zingine pia, so akifa ujue ndio siku zake zimeisha na aliandikiwa kufa hivo, kuna shabiki mwingine alifariki pia chama alipofunga goal dhidi ya As Vita mwaka juzi kwahiyo nayeye tumseme aache kufunga dkk za lala salama maana mashabiki wanakufa

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama unahisi ujumbe umemfikia kuna haja gani ya kuendelea kumsema kila Uzi ata kama hujaanzisha wewe, brother kumbuka jamaa hapendi hayo anayopita na kukosa Kwa magoli haimaanishi ni mchezaji mbaya, labda nikukumbushe Tu mwaka huu kwenye ligi zote mchezaji ambae anaongoza Kwa kukosa nafasi za wazi ni Christiano Ronaldo kakosa nafasi 33 za wazi Hadi hivi sasa, kwahiyo nayeye wamuanzishie Uzi afukuzwe au asichezeshwe?....
Sawa Mkuu Nimekupata
 
Kuna ka ukweli.

Huyu Mugalu wakati alianza kupewa Dk 10 kila mechi na akawa anatupia kila mechi. Sio huyu wa sasa ambaye anakaribia kumfikia Saporng kwa kukosa mabao ya wazi.
 
Mkuu Una kitu na Mugalu labda sie hatukijui? Nadhani ni muda ukaweka wazi sasa, maana imekuwa too much Kwa mwanaume kutwa kumsema mwanaume mwenzio, imekuwa kila thread upite umseme mwanaume mwenzio seriously?

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Japo haujaniuliza mimi, naomba kukuuliza kitu pia, wewe una nini na Mugalu, mbona unaumia sana anaposemwa vibaya? Kila thread wewe unamkingia kifua, huoni kasoro zake kabisa.
 
ALIPOFIKA nchini mtu mmoja wa Simba alininong’oneza kitu kuhusu mshambuliaji anayeitwa Chris Mugalu. Aliniambia; “Mugalu ni mchanganyiko wa John Bocco na Meddie Kagere kwa pamoja”. Hii ilikuwa kauli ya kurahisisha kwa mtu anayetaka kumjua Mugalu.

Niliambiwa kuwa aliyesema hivyo ni kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri ambaye huwa anawasaidia watu wa Simba kuwajua wachezaji waliowahi kucheza soka katika ardhi ya Zambia. Kumbuka kwamba Phiri yupo Zambia kwa sasa.

Mechi zake za kwanza nchini niliamini kilichosemwa. Alifunga mabao maridadi ya mshambuliaji halisi. Ungeweza kuamini kwa urahisi. Nilijua kwamba Simba ilikuwa imepata mtu ambaye anaweza kuwaweka benchi Bocco na Kagere.

Lakini sasa Mugalu huyu sio yule aliyefika nchini. Watu wa Simba wanamzomea. Anapitia wakati mgumu kuliko wakati mwingine wowote ule. Anatia huruma. Hata yeye mwenyewe anaonekana kuchanganyikiwa. Anakosa mabao ya wazi kupitiliza. Pambano la Simba dhidi ya Vita aligeuka kuwa kichekesho uwanjani baada ya kukosa mabao mengi ya wazi kisha akaondolewa.

Nyakati kama hizi kichwa cha Mugalu kinakuwa na mambo mawili. Kwanza kabisa kichwa chake kinakosa kujiamini. Mshambuliaji akikosa mabao ya wazi tena na tena anajikuta haamini tena katika uwezo wake, wakati mwingine anaogopa hata kujaribu kupiga.

Kwa wazungu, mshambuliaji wa aina hii huwa wanapambana na kichwa chake. Wanajaribu kumrudishia uwezo wa kujiamini ndani na nje ya uwanja. Wakati mwingine anapewa hata penalti yoyote inayotokea uwanjani ili mradi afunge kwa urahisi na aweze kujiamini tena.

Lakini kuna jambo jingine. Katika kichwa cha Mugalu kwa sasa anaweza kuwa anaamini kuwa amerogwa. Mara nyingi inatokea kwa wachezaji wa Afrika hasa wale ambao wanafika katika nchi kama Tanzania na kusikia simulizi hizi kutoka kwa mashabiki au wachezaji wakiwa kambini.

Hili la pili siliamini sana ingawa lipo na inasemwa kwamba hata katika vitabu vya dini imeandikwa kwamba uchawi upo. Sisi wengine sio kazi yetu kuamini katika hili, tunachojua ni kwamba ikitokea Mugalu akafunga bao moja tu basi ari ya kujiamini itarudi kwake.

Hauwezi kuwa mchezaji mbovu au mzuri kwa usiku mmoja. Haiwezekani Mugalu niliyemuona mimi katika siku za kwanza ghafla akawa mchezaji mbovu. Kuna washambuliaji walikuja nchini na tukajua kwamba hawana lolote kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho. Mmojawapo ni Yikpe.

Kile kiwango cha Mugalu wakati anafika hakikuwa cha bahati mbaya. Kile ndio kiwango chake halisi. Nadhani hata Simba walitumia pesa nyingi kumnasa baada ya kumchunguza na kujiridhisha kwa kauli ile ile niliyosema hapo juu kwamba “Mugalu ni mchanganyiko wa John Bocco na Meddie Kagere kwa pamoja”.

Kinachotakiwa kwa watu wa Simba kwa sasa ni kuendelea kumjengea imani. Inabidi wamshangilie kwa nguvu kwa namna yoyote ile. Wakati mwingine huwa tunawaua wachezaji wazuri kwa sababu ya kukosa busara. Hii ni kuanzia kwa mashabiki hadi viongozi.

Mchezaji wa aina ya Mugalu ni wa kupewa moyo na sio kuzomewa. Ni mchezaji wa kupigiwa makofi hadi anapokosea. Atakapoona watu wa Simba wamesimama nyuma yake ndipo uwezo wake wa kujiamini utakaporudi.

Vinginevyo kuna minong’ono mingi kwamba huenda Simba ikasaka mshambuliaji mpya. Hauwezi kubadilisha wachezaji kila siku. Hawa washambuliaji huwa wanapitia nyakati hizi na bado huwa wanapewa mikataba mipya. Kitu cha msingi ni kujua tu kwamba mshambuliaji wa aina yake anapokuwa fiti huwa anakuwa ni mchezaji wa aina gani.

Vinginevyo unaweza kujikuta unabadilisha wachezaji kila uchao. Haifai kuwa hivi. Labda kama mchezaji ataendelea kuwa na fomu mbovu kwa misimu miwili unaweza kujikuta katika nafasi ya kuachana naye. Ushauri wangu Simba wasifikirie kuachana na Mugalu kwa haraka haraka. Wafuatilie tu kitu kinachomsibu.

Pale mbele anawapa nguvu kubwa ya umiliki mpira hata kama hafungi. Ukame kama huu alionao huwa wanaupata akina Sergio Aguero, Pierre Emerick Aubameyang, Luis Suarez na washambuliaji wengine mahiri duniani.

Katika usajili wa wachezaji Tanzania nimegundua aina tofauti tofauti za wachezaji. Kuna mchezaji ambaye tangu siku ya kwanza mnahisi kwamba mmepigwa. Huyu ndiye kama Yikpe. Halafu kuna mshambuliaji ambaye anakaa katika uchunguzi zaidi. Huyu ni kama Michael Sarpong.

Kuna mchezaji ambaye anaonyesha makali yake tangu mwanzo lakini ghafla makali yake yanapotea. Huyu ndiye kama Mugalu. Kunakuwa na mambo mengi nyuma yake. lakini pia kuna mshambuliaji ambaye anaanza taratibu lakini baadaye akizoea anakuwa moto. Mfano ni Donald Ngoma.

Ngoma alipokuja Yanga alianza taratibu lakini makali yake yakaimarika kila uchao na baadaye akaibuka kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora nchini. Mwanzoni mashabiki wa Yanga walikuwa wakimfananisha na mshambuliaji wao wa zamani, Idd Mbaga. Baadaye walijikuta wakimuheshimu zaidi.

Hii kesi ya Mugalu ndio ambayo inakuwa ngumu zaidi. Mchezaji anaonyesha makali halafu ghafla anakuwa wa kawaida. Huwa ni kesi ngumu ambayo inawaacha wachambuzi, makocha, viongozi na mashabiki wakiwa hawana majibu ya moja kwa moja.

EDO KUMWEMBE
Kwa ilipofikia simba kwa sasa inaweza kuvutia wachezaji wengi wazuri, replace mugalu kwa bwalya, kagere bado tina jambo naye
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom