Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Mwanamke gani kafanikiwa bila mkono wa mwanaume?Mimi ndio siwasikilizagi kabisa.wale wanawezeshwa.baada ya hapo wanavua pichu
Nitoe tu mfano,
Kuna mwanamke mmoja alikuwa ana pika chakula kama mama lishe, kila mteja aliyekuwa anaenda kula pale aliitwa shemeji na wahudumu wake, halafu ikitolewa elfu kumi change hairudi, kitumbua kinagawanywa kwa shift, siku mtu kama huyu atadanganya wenzake siku moja kwamba ni malkia wa nguvu. Hatari sana. Hii ni sawa na zile hadithi za kusema watu waliuza karanga mara kushona viatu kumbe kuna pazia lililoficha mengi.
 
Wengi wao ni watu wa kamba sana

Msome huyu

"Wasichana au wakina mama tunaweza kununua madira ya elfu 13,000 au Lipstick ya elfu 3,000 lakini tukashindwa kununua unga wa maandazi wa elfu 10,000, wasichana wengi wanaonea aibu biashara zao wakihofoa watachukuliwa na jamiii, Mimi mpaka kufika hapa nilianzia na mtaji wa elfu 20,000 tu lakini kwasasa nimekuwa chanzo cha ajira nyingi za watu" Selina Letara [HASHTAG]#MalkiaWaNguvu[/HASHTAG] wa mwaka jana ambaye ni Mmiliki wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa Hc Pads Tanzania

mwingine huyu hapa anaseama

"Mimi nilianza na mtaji wa laki moja (100,000) ambayo hiyo ukijumlisha na nauli ya kwenda na kurudi kariakoo ambapo nilikuwa nauza nguo za ndani kwa wanafunzi wenzangu chuoni, lakini kwasasa nina duka la nguo za kiume (Nguo za dukani) na Duka la nguo za kike (Nguo za Mtumba), Nauza kisamvu kwenye supermarkets, Popcorns na Spaghetti (Tambi)" Latifa Mohamed

mwingine huyu hapa

Bado kuna watu wengi ambao wanasoma Udaktari lakini mawazo yao yapo kwenye kuajiriwa wakimaliza masomo yao badala ya kuwaza ni kitu gani inabidi akifanya ili kusaidia jamii yake kwa kutumia elimu yake, Kuna watu wengi ambao ukiwapelekea mawazo yako wao wanayabeba na kufanyika kazi wao na hii isiwakatishe tamaa kwani wewe ndiyo unajua lengo la wazo lako ambalo ungetamani ulifanye na ulikuwa unalitazama kwa ukubwa ule" Juliana Busasu [HASHTAG]#MalkiaWaNguvu[/HASHTAG] 2017 ambaye ni mwanafunzi wa Udaktari mwaka wa tano na ni Mkurugenzi wa
Tanzania Health and Medical Education Foundation (TAHMEF)

mwingine huyu hapa

Mimi wakati nataka kuanza biashara yangu ya [HASHTAG]#Manjano[/HASHTAG] watu wengi walinikatisha tamaa lakini kwasababu nilijua nataka nini sikukubali kukatisha wazo langu, hata wakati nilipotaka kufungua Chuo cha urembo nilimfata 'Mental wangu' (Mshauri) na kumueleza wazo langu na alinishauri nifunge baadhi ya maduka yangu japo ilinitisha lakini nilifunga ili niweze kufungua chuo na kweli kwasasa nina chuo cha urembo na biashara zangu zinaenda vizuri" Shekha Nasser
Wengi ni fix yaani ni sawa na mie wakati nasubiri matokeo ya form 6 nilipiga kazi mbalimbali kama zile za kumwaga zege alafu nikifanikiwa najifanya nilianzia kwenye kumwaga zege wakati ukweli kule ilikuwa napita tu mara moja huku lengo langu ni kuendelea na masomo kuliko kupoteza miezi karibu 16 (enzi zile tulikuwa tunakaa zaidi ya mwaka kusubiri kwenda chuo)
 
Kila anayehojiwa na Mtangazaji ' Critical ' na ninayempenda na kumkubali kabisa Siza wa Cloudstv 360 on Saturday wakiwa ' mubashara ' kabisa kutokea Mlimani City kuwa aelezee Historia ya Mafanikio yake hadi leo wamefanikiwa Kimaisha unaona tu wanazunguka zunguka huku mengi tukifichwa.

Nikilitumia sana ' jicho ' langu Kali la ' Kisaikolojia ' na kwa jinsi ninavyowakodolea hawa Wanawake wakiwa ' mubashara ' wanatiririka na wanaserereka naona Shuhuda zao za Kimafanikio hayo waliyonayo zimejaa ' Unafiki ' mtupu hasa kwa wawili mmoja wapo akiwa anapatikana sana Millenium Tower Kijitonyama na mwingine akiwa mara kwa mara humkosi katika Vipindi vyake Channel Ten ambao ' Channels ' zao za hayo mafanikio yao zina mkono wa ' Kimahaba ' wa waliokuwa na Mamlaka yao / wenye Nyadhifa zao hapa Tanzania.

Wito tu Kwenu ambao huwa mnapenda ' Kutudanganya ' kuhusu mlivyopata hayo mafanikio yenu itapendeza sana na hata kutushawishi zaidi kama siyo kutufundisha endapo mtakuwa mnatupa zile Shuhuda zenu halisi hata kama zinatisha au kutia aibu kuliko kudhani kuwa huu uwongo wenu hatutaugundua haraka.

Ngoja niendelee kuwaangalia na nizidi Kudanganyika. Kazi ipo hakyanani!

Nawasilisha.
Hasa huyo anaejiita mchungaji.
Mavazi yake na muonekano wake...mhh..!!
 
ukisema mtaji mkubwa unakatisha tamaa maskini...

kuna biashara kwa mtaji mdogo zinawezekana kama kuuza juice... kwa kuwapa moyo maskini lazma useme mtaji mdogo ambao hata wao wanao
 
Mkuu uwezi amini nilitaka kuanzisha mada kama hii ya hii dhana ya uongo au kuwadanganya watu kuwa kila aliyefanikiwa alianza na mtaji mdogo hasa kwa wana wake.....ngoja nikuletee nyama kidogo uweke hapo juu ...naleta nukuu zao
Mkuu unaweza kuwa ni mtizamo wako binafsi
Ila mimi pia ni mmoja wa hao walioanza na mtaji mdogo sana
Na unaendelea kukua.
Sijui ni kwa nini uone ni fake story!

Labda ungesema backups na changamoto za kurudisha mtu chini hazikosekani.
 
Back
Top Bottom